Nampongeza Nabii Geordavie kwa kazi yake iliyotukuka

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Kipekee kabisa Mungu akubariki sana mtumishi wa Mungu.

Una moyo wa kipekee sana, sina shaka ndiomana una marafiki wa dini zote hapa nchini na ulimwenguni, nafuatilia matukio yako na kazi zako zote za utumishi na wema wako kwa watu mbalimbali.

Nimewiwa kukupa pongezi za dhati kwa tunu ya pekee ya kukubalika na mashekhe toka DSM waliokuja Arusha kukupa nguvu na kukutia moyo.

Usiogope tupo pamoja nawe katika hali zote. Kipekee pia nikupongeze kwa kuwa mwenye utii wa mamlaka za nchi na serikali tukufu. Panapo Majaliwa inshallah nitakuja Arusha kutoa ushuhuda wa namna unavyotuweka karibu na Mungu na matokeo chanya mimi nikiwa mfano wa kuigwa.

Ndimi kondoo wako mdau wa jamii forums.

wadiz
Email: shazwadiz@gmail.com
 
Weka basi kitu kimoja alichofanya?
 
Mkuu mpaka email unataka uitwe ukapewe ka IST...hakuna kitu pale ni nabii wa uongo kama manabii wengine wa uongo..
 
Unasifia Ujinga.Kwanza wale siyo Masheikh na mbaya zaidi si Waislam,wamenunuliwa kanzu na kofia kuhadaa umma,kwamba ni waislamu,hakuna muislam wa kweli kuja kudhihaki Dini yake kuja kumsifia kafiri anayekula wake za watu.
Matapeli tu wale,2,3 nawajuwa physical wazushi tu

Ova
 
Unaweza kusema ni yupi kati ya wale ni Sheikh hapa Dar ......?!
 
Unaweza kusema ni yupi kati ya wale ni Sheikh hapa Dar ......?!
Wakati pale kuna mmja anaitwa mussa embe alikuwaga mwenyekiti wa serikali ya mtaa kinondoni
Hana cha usheh wala nini
Wasaka Tonge tu,nchi hii ina wajng wengi sana

Ova
 
Unaweza kusema ni yupi kati ya wale ni Sheikh hapa Dar ......?!
Ni mashekhe Kwa imani zao, na wamejitambulisha hivyo tuheshimu imani yao na njia ya Pepo yao na uhuru katika nchi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…