Mimi ni shabiki lialia wa muziki wa Hiphop (Rap). Kuanzia rappers wa ndani hadi wale wa America. Kimsingi Hiphop ni muziki wangu pendwa zaidi. Simu yangu ina nyimbo za Sugu, Kalapina, N2N, Prof Jay & HBC, Nay Trueboy, Naziz, biso na biso, Zay B, Missy Eliot, Dr Dre, Jay Z, 2pac, Dmx, na wakali wengine wengi.
Leo nachukua nafasi hii kumpongeza Nay The Trueboy kwa kuachia ngoma yenye utata ambayo imesababisha BASATA wamhoji.
Binafsi naona ni hali ya kawaida tu kwa mwanamuzikiwa hiphop kupata mikwaruzo ya hapa na pale. Ila nampongeza zaidi kwa kuwasaidia CHADEMA kupata agenda ya kusogeza siku baada ya ile ya bandari kubuma.