Andiko LA Mwl Shija Samweli kutoka misungwi Mwanza;
RAIS AINGIZWA KINGI USUKUMANI
Ukweli ni kwamba,USUKUMANI hatujawahi kuwa na CHIFU wa jinsia ya kike na hatutarajii Kama atakuwepo kesho au kesho kutwa.
Usukumani hajawahi kuwepo CHIFU wa MACHIFU(ntemi o batemi) tangu mwanzo wa Zama za sukuma land (igunguli lya banhu ba sukuma).
Iko hivi;
1.kwa usukumani, cheo Cha UCHIFU hupewa wanaume tu(Ngosha)ndiyo maana tuna majina Kama CHIFU MALONJA,MASANJA NK
2.Wapo wanawake(bakima) waliowahi kupewa nafasi kubwa za "ulezi" wa ukoo(clan) ambapo cheo Chao waliitwa NGOLE(malikia).tunayo mifano kadhaa ya kina NGOLE wa kike Kama vile,MINZA,NGOLO,NG`WASHI,NKAMBA,NG`WISABI,na huyu NKWIMBA aliyepewa kuulea ukoo uliozaa jina la wilaya ya KWIMBA yenye mjumuiko wa wilaya za MISUNGWI na MAGU.
Ukikaa na msukuma yeyote,sikiliza salamu yake asubuhi.Utasikia maneno E-MINZA au E-NGOLO,E-NKWIMBA nk.hii ni heshima pekee inayotolewa kwa kuwakumbuka Hawa malikia kulingango na Koo zao na kamwe hautasikia msukuma anasalimia na kusema E-shija,E-magufuli,E-malonja au E-suluhu.
3.NGOLE/malikia(kiongozi wa kike) ni mlezi tu wa ukoo.mipango yote ya ulinzi na usalama hufanywa na NTEMI/ Chief akishirikiana na maakida/maaskali wakuu wa ikulu(bashilikale ba g'wi-kulu).
4. jina la HANGAYA Ni jina la nyota(sonda) inayong'aa Sana asubuhi ambapo mtu akizaliwa asubuhi Kabla nyota hiyo haijafifia anaweza kuitwa jina Hilo, haijarishi ni mwanamke au mwanume.usukumani hatujawahi kuwa na CHIFU wala NGOLE wa jina la HANGAYA.
5.ngoma za heshima za kumtawaza CHIFU(ng'oma ja milango) hazilii hovyohovyo Bali huandaliwa siku na utaratibu maalum tofauti na hiki kilichofanywa na UMT katika viwanja vya Redcross-magu.
Je,Ni Nani alishawahi kusikia "mkuu wa mkoa" wa "wakuu wa mikoa"?,au CHIFU wa MACHIFU?? Hiiiiiiiiii elelo twa lembiwa lemi nyange!!.tukisema rais ameingizwa kingi usukumani,hii ndiyo maana yake.
Hata Kama mna FURAHA,Fanyeni utafiti wa kutosha hasa kwenye matukio makubwa Kama haya.tofauti na hapo unaweza kushushwa hadhi bila kujua.
SHIJA ss SHIBESHI.
Misungwi.