Nampongeza Rais Samia kwa kukubali kuwa Mkuu wa Machifu Tanzania

😂😂😂😂
 
Hatua itayofuata ni kuwapa Machifu wenzake uwezo wa kazi za kijamii na kuwa washauri wakuu wa mipango ya kimkakati itakayo saidia katika kurudisha na kuhudumisha utamaduni mila na desturi za watu wa Tanzania na kuwaelimisha vijana wa kesho kuhusu umuhimu wa kuwa na Utamaduni uliokuwa na miguu!
Hii ni ishara nzuri kutoka kwa Mh. Raisi na ushindi mkubwa kwa watu wa Afrika.

Aluta Continua
 
😍
Siempre Chief Hangaya
Siempre JMT

Aluta continua💪
 
Hujaeleweka jazia nyama
 
Mwl. Nyerere enzi za uhai wake ulituasa kuwa umuhimu wa mambo ya ukabila ikijumuisha na hayo ya uchifu yamebakia katika masuala ya kutambika tu. Sijui sasa hata huo uchifu Madam President atautumia sehemu gani!
Matumizi yake yanajulikana maana wewe siyo chifu utamtumbuaje boss wa PPRA wakati aliyekalia kiti cha PPRA ni mshirka wa machifu
 
Kukemea mapepo ni maombi ya vita ambayo yanaweza kuangamiza mapepo na muhusika kama alikuwa anayatumia na kuendelea kuyangangania unless ametubu na kuachana na njia hizo. Machief walimfata ama aliwafuata?
Hujajibu nikichokuuliza, halafu ukichojibu sijakuuliza.

Kwani kukemea mapepo hakuwezi kuendana na kumuombea mtu hekima na ulinzi?

Wewe tatizo lako ni lipi hasa katika maigizo haya?
 
Kuna ukweli kuwa ingekuwa vema itangazwe kuwa ni chief wa eneo walilomsimika. Ingeleta heshima zaidi. Kusema ni wa nchi mzima, wamekosea, yeye ni Raisi wa nchi yote lakini uchief ni wa eneo eneo na kabisa fulani.
Labda kama hao machief wa makabila yote walikaa na ku-deliberate hilo.
Tuwe makini, si kila jambo linamuinua mama yetu. Mengine asifiwe yaishie hukohuko.
 
Hujajibu nikichokuuliza, halafu ukichojibu sijakuuliza.

Kwani kukemea mapepo hakuwezi kuendana na kumuombea mtu hekima na ulinzi?

Wewe tatizo lako ni lipi hasa katika maigizo haya?

Hakuendani Uislamu umekataza shiriki. Ambako ndiko msamiati ushirikina ulipozakiwa.
 
Hakuendani Uislamu umekataza shiriki. Ambako ndiko msamiati ushirikina ulipozakiwa.
Wewe unaelewa kwamba kwa wasioamini Uislamu, Uislamu kwao hao unaweza kuwa shirki?

Kwa nini Uislanu uwe special?

Ushirikina na Uislamu zote ni imani kwenye supernatural powers zisizoweza kuthibitishika, unakubali hilo?
 
Mh ni muumini wa dini ipi kati ya hizi unazoongelea.
 
SSH Rais ,akasome why walifutwa enzi za mwalim , lengo ulikua nini,??
 
Naomba kuuliza, hivi ktk historia na utamaduni hasa wetu wa Kitanzania, tuna Machief Wanawake?
 
Hujui kitu wanawake machifu usukumani waliwahi kuwepo. Kawaulize wazee wa kwenu watakueleza ukweli. Mfano utemi wa Buhungukila wilaya ya Kwimba uliwahi kuwa na mtemi mwanamke. Aidha mtemi wa mwisho wa Urambo ni Kibete binti wa Mtemi Milambo. Nenda kajifunze zaidi umekurupuka.
 
Mh ni muumini wa dini ipi kati ya hizi unazoongelea.
Unajuaje mtu ni muumini wa dini fulani au anasema tu kuwa ni muumini wa dini fulani?

Na kwa nini uumini wake uwe muhimu katika muktadha wa hoja yangu?

Ikiwa 1 ni 1, na si 2, muheshimiwa akiamini 1 ni 2 atabadilisha ukweki na kufanya 1 iwe 2?
 
Ikiwa ni 2 ni 2 na si 1, basi 1 na 2 zote zitabakia kuwa ni namba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…