Namshangaa Mo Dewji

platozoom

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
9,424
Reaction score
11,320
Mo ni Mtu ambaye ungetegemea anavijua vizuri hivi vilabu vya Simba na Yanga, achana na historia zao ila siasa zake.

Siku niliposikia Mo anataka kununua hisa 49% za Simba nilipata mshangao sana. Kwamba anashindwa kujua kuwa kwa mazoea ya vilabu hivi na aina ya Viongozi na Wanachama nani yupo tayari kukuachia uendeshe timu kisasa.

Ni rahisi sana wao kufurahia habari ya bilioni ishirini na ufadhili lakini sio kuweka structure kibiashara! Watafurahia sana kusikia umetoa fedha mfukoni na kuwapa wachezaji au kusafirisha mashabiki na Viongozi na si namna gani hiyo fedha itarudi au kuongezeka.

Simba na Yanga hazipo kuendeleza 'mpira' ila kwa ajili ya furaha ya mashabiki kama sisi (usiniulize habari ya furaha itapatikanaje bila pesa) na siasa za mpira.

Nakumbuka enzi za Manji, kuna wakati nikamwambia rafiki yangu na shabiki mwenzangu wa Yanga, hivi unafikiri Manji atatoa kila siku bila na yeye kufaidika?!! Never.

Na niwaulize mashabiki na Wanachama wa Simba, hivi kuna mwekezaji gani makini wa biashara atawekeza bila kujua asset na nyaraka zote za kampuni ili kujiridhisha pale anapowekeza?

Yaani umwambie 'Masawe' nataka kuwekeza kwenye biashara yako ya magari halafu akwambie nakupa 49% ya hisa kwa bilioni moja ila kadi za magari hutakiwi kuona!! Ila nitoe tu 'mpunga'

Kama hali itaendelea hivi basi wa kulaumiwa ni Mo mwenyewe. Ni mzoefu kwenye 'siasa' za vilabu vyetu hivi vikubwa lakini akajitosa.

Namshauri aachane na mambo ya hisa abaki na ufadhili, ufadhili hauna faida ya moja kwa moja ila una faida ya 'publicity'. Na kama anaendelea na mambo ya hisa basi atumie mbinu nyingine na kujifanya 'mjinga'.

Toa bilioni 20 kwa masharti kuwa fedha zote zinawekezwa kwenye hati fungani (kama ambavyo alishawahi kuzungumzia) halafu ikiiva unachukua kabisa mpunga kulingana na shea zako halafu utakuwa unatoa kidogo kidogo kama ufadhili ili mashabiki sisi makapuku tupate burdani, mambo ya utajiri wa klabu waachie akina Barcelona.
 
kabacholi janja sana,,,
nasajili wachezaji menyewe,, notoa becha ya usajili yeye menyewe na sika kalamu kuandika mekataba na pia na biga bicha ya selfee yeye menyewe,

Apana ita maswahili hata moja nehi,,maswahili pia na yenyewe ni janjajanja,maarkihe
 
MO alisema atajenga uwanja wa simba, sehemu ya kujenga ipo, kajenge sasa hataki. ndio maana watu wameanza kushtuka
 
Simba vunjeni mkataba na MO. ama la mtakuja lia huko mbeleni. tena kilio cha mbwa koko.
 
Yanga na Simba ni timu za kichawi ndo maana.

zinapingaje uwekezaji kama huu wa Mo kwa mfano?

au yule witch doctor Akilimali ameisaidia nini timu yake baada ya Manji kujiondoa?
 
masikini bhana mna kelele sana, lazima mtu kujua anawekeza wapi na kwenye nini kama ni hela mwambie hata baba ako anunue hisa za samba tuone kama atanunua 20% bila kujua mali na madeni ya simba
 
masikini bhana mna kelele sana, lazima mtu kujua anawekeza wapi na kwenye nini kama ni hela mwambie hata baba ako anunue hisa za samba tuone kama atanunua 20% bila kujua mali na madeni ya simba
Ndo hapo naposhangaa.
Yaani wanafikiri bilioni 20 ni pesa ya maembe. Hakuna mfanyabiashara atakayekubali ho ujinga
 
MO alisema atajenga uwanja wa simba, sehemu ya kujenga ipo, kajenge sasa hataki. ndio maana watu wameanza kushtuka
Unajua gharama za ujenzi.
Unajenga bila kujua nyaraka za Kampuni uliowekeza zikoje! Yaani useme tu thamani ya mali zangu ni bilioni bila kuona nyaraka!!
 
Karibu katika Jukwaa Jipya la Michezo..SokaTalk.
Hapa,utaweza kujisajiri,kuanzisha na kuchangia mada mbalimbali zihusuzo soka ulimwenguni kote.
Karibu Mdau!
 
Mi sijaelewa hao simba wanaogopa kumpa hati Mo kwa kuhofia nini? Yaani atauza timu na majengo au? Hizo hati saivi zinaisaidiaje simba?
 
Mpira wa simba na yanga ni kazi kubwa kushabikia hasa kwa watu wanaopenda maendeleo hasa ya hizi club,.. Wakati simba tumeanza kuingiza huu mfumo mpya, vikwazo vingi sana vilikuwepo na tuliweza kuvishinda tena kwa nguvu zote!! Vijana wapenzi wa simba tulipeana elimu juu ya huu mfumo mpya . Sidhani kama tunaeza shindwa kwa sehemu ilobakia never..!! Kipindi kile maadui walikuwa wengi but we defeated all of them.. Sasa Adui mmoja mpuuzi ndio atushinde hahhahaa itakuwa ajabu sana endapo viongozi tulowapa dhamana watakubali!! Mafanikio yana changamoto kubwa sana, maadui wasopenda success yako huwa wanaongezeka!! Jiulize kwanini timu ya TAIFA haifanyi vizuri na haiji fanya vizuri kamwe endapo tutakuwa na mtizamo hasi!! Mpira ni uwekezaji tena uwekezaji haswa, na mafanikio hayaji ndani ya siku moja never!! Usimba na Uyanga una haribu mpira !! Simba tumejitoa mhanga kwene hili , na tulikubaliana na hili !!
 
Wewe yanga acha upumbavu mbona manji mnambembeleza mpaka mlitaka kumchukulia Fomu?
 
Unajua gharama za ujenzi.
Unajenga bila kujua nyaraka za Kampuni uliowekeza zikoje! Yaani useme tu thamani ya mali zangu ni bilioni bila kuona nyaraka!!
Kwa hiyo hata akionyeshwa tu hizo nyaraka kisha asipewe ni sawa?
 
Siye washabiki ndiyo source ya ujinga wa vilabu hivi tungeweza visusia kutazama mechi zake yawezekana viongozi wangeamka kutafuta uwekezaji, ndiyo maana kuna timu inajiona fahari kuitwa timu ya wananchi kisa kutembeza bakuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…