platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,424
- 11,320
Mo ni Mtu ambaye ungetegemea anavijua vizuri hivi vilabu vya Simba na Yanga, achana na historia zao ila siasa zake.
Siku niliposikia Mo anataka kununua hisa 49% za Simba nilipata mshangao sana. Kwamba anashindwa kujua kuwa kwa mazoea ya vilabu hivi na aina ya Viongozi na Wanachama nani yupo tayari kukuachia uendeshe timu kisasa.
Ni rahisi sana wao kufurahia habari ya bilioni ishirini na ufadhili lakini sio kuweka structure kibiashara! Watafurahia sana kusikia umetoa fedha mfukoni na kuwapa wachezaji au kusafirisha mashabiki na Viongozi na si namna gani hiyo fedha itarudi au kuongezeka.
Simba na Yanga hazipo kuendeleza 'mpira' ila kwa ajili ya furaha ya mashabiki kama sisi (usiniulize habari ya furaha itapatikanaje bila pesa) na siasa za mpira.
Nakumbuka enzi za Manji, kuna wakati nikamwambia rafiki yangu na shabiki mwenzangu wa Yanga, hivi unafikiri Manji atatoa kila siku bila na yeye kufaidika?!! Never.
Na niwaulize mashabiki na Wanachama wa Simba, hivi kuna mwekezaji gani makini wa biashara atawekeza bila kujua asset na nyaraka zote za kampuni ili kujiridhisha pale anapowekeza?
Yaani umwambie 'Masawe' nataka kuwekeza kwenye biashara yako ya magari halafu akwambie nakupa 49% ya hisa kwa bilioni moja ila kadi za magari hutakiwi kuona!! Ila nitoe tu 'mpunga'
Kama hali itaendelea hivi basi wa kulaumiwa ni Mo mwenyewe. Ni mzoefu kwenye 'siasa' za vilabu vyetu hivi vikubwa lakini akajitosa.
Namshauri aachane na mambo ya hisa abaki na ufadhili, ufadhili hauna faida ya moja kwa moja ila una faida ya 'publicity'. Na kama anaendelea na mambo ya hisa basi atumie mbinu nyingine na kujifanya 'mjinga'.
Toa bilioni 20 kwa masharti kuwa fedha zote zinawekezwa kwenye hati fungani (kama ambavyo alishawahi kuzungumzia) halafu ikiiva unachukua kabisa mpunga kulingana na shea zako halafu utakuwa unatoa kidogo kidogo kama ufadhili ili mashabiki sisi makapuku tupate burdani, mambo ya utajiri wa klabu waachie akina Barcelona.