Namshangaa sana mtu anayeishabikia CCM

Namshangaa sana mtu anayeishabikia CCM

Msukuma Original

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2018
Posts
928
Reaction score
3,330
Huwa najiuliza, hivi mtu kabisa na akili zako timamu unashabikia CCM? Binafsi nina amini wanaoshabikia CCM ni wale wenye maslahi binafsi otherwise uwe taahira. Chama kilichoisababishia nchi ufukara na matatizo lukuki unakishabikia kwa lipi?

At least JPM alipoingia tulianza kuona matokeo kiduchu ya kimaendeleo lakini bado hai-justify ufukara na matatizo lukuki yaliyosababishwa na hiki chama.

Wanawake, watoto wachanga kibao wamepoteza maisha kwa kukosa huduma bora za afya miaka nenda rudi. Huduma ya maji safi na salama vijijini na mijini bado shida, ajira kwa wahitimu hakuna, matatizo chungu nzima.

Jamani hebu nisaidieni labda kuna kitu sikielewi, hivi mnaoipenda CCM nnaipendea nini? Wale wenye maslahi binafsi kwenye chama kama watoto wa mawaziri, wabunge na wateule wa rais kwenye nyadhifa mbalimbali wana sababu ya kuipenda CCM, sasa hawa wengine raia wa kawaida naomba mnisaidie, CCM mnaipendea nini?

mama D johnthebaptist Magonjwa Mtambuka jingalao barafuyamoto YEHODAYA Stroke Kinuju MOTOCHINI Pulchra Animo
 
Mkuu shda Ni matumbo Yana njaa Sana!

Nakukumbusha TU, ya kuwa tuko uchumi wa Kati wa kitanzania!
 
Wasioishabikia CCM wamekosa kabisa uwezo na ushawishi japo ule wa kufanya kitu kitakachowabadili wale wanaoishabikia CCM

Fanya mambo wakuelewe, njoo na matatatizo na ushauri kuhusu kuyamaliza hayo matatizo. Ukija na malamiko tuu CCM WATAENDELEA KUCHUKUA NA NA KUWEKA WAAAAA

MUNGU IBARIKI TANZANIA 🙏
 
Hata Chadema wanaipenda CCM kwa sababu inawapa ruzuku na kuwanunua kama bidhaa!
Wewe ni mshabiki kwa kuwa ugali unatokea pale geti kijani sio,hivyo hata wafanye uovu gani hutaona kwa kuwa sasa tumbo linafanya kazi ya ubongo.
 
Kushabikia kashabikie timu za mpira, Vyama vya Siasa vya Tanzania ambavyo havina tofauti ya ideology bali ni platform za mtu kupiga siasa zake vyote ni vilevile tu.

Cha maana inabidi usiwe na ushabiki wa Simba na Yanga bali uunge mkono au upinge vitu individually, ushabiki means unameza yote hata pumba, hivyo kwa maoni yangu ushabiki wa vyama za siasa husasan bongo hauna tija.
 
Kwa hiyo Tanganyika ilianza na hayati JPM?

Kwa hiyo Tanzania ilianza na hayati JPM?

Yaani toka uhuru mpaka anakuja JPM hakuna MAENDELEO?🤣🤣🤣

Kweli wewe ni SAKALA
Kweli wewe ni HOBOBO
Jibu swali. Mbona swali rahisi tu. Au kusoma na kuelewa hujui?
 
Wasukuma wote wangekuwa kama wewe, hii nchi ingepata ukombozi wa kweli mapema sana!

Kushabikia ccm ni sawa tu na kujigeuza na kuwa msukule! Unless otherwise uwe kwenye mfumo wa ulaji. Maana ccm ni kikundi tu cha watafunaji wachache wa keki ya Taifa.

Wanarithishana tu kitoka kizazi kimoja kwenda kingine. Mifano ni mingi, muda ni mchache.
 
Kushabikia kashabikie timu za mpira, Vyama vya Siasa vya Tanzania ambavyo havina tofauti ya ideology bali ni platform za mtu kupiga siasa zake vyote ni vilevile tu.

Cha maana inabidi usiwe na ushabiki wa Simba na Yanga bali uunge mkono au upinge vitu individually, ushabiki means unameza yote hata pumba, hivyo kwa maoni yangu ushabiki wa vyama za siasa husasan bongo hauna tija
Sawa, lakini hawa wenzetu wanaoitetea na kuilinda CCM huwa wana sababu gani hasa? achana na wale waliokulia kwenye mfumo wa ccm kama watoto wa viongozi.
 
Ninaipenda na kuishabikia CCM kwa kuwa haina sera za majimbo

Hebu angalia Ethiopia inavyoendelea kuteketea kwa sababu ya sera yao ya majimbo

Watigrinya wa Tigray ni 6% ya raia wote nguvu za kiuchumi, kijeshi na kiushawishi walizonazo zilitokana na kubebwa kimajimbo, leo wanatwangana wanataka kujitenga wanataka waanzishe taifa lao

CCM iliyaona hayo muda mrefu ndio maana huoni katika ilani zao za uchaguzi wanaweka sera za majimbo

Sasa hebu watafakari chadema na sera zao za majimbo

#Kaziiendelee
 
Back
Top Bottom