Sipati picha first day sabaya ndio anapokelewa na wafungwa wenzake gerezani na kuanza kutumikia miaka yake 30 jela ,
At first anakutana na wale aliowabambikia kesi wkt akiwa kwenye nafasi mbali mbali za uongozi
Ikumbukwa kwamba kabla hajawa DC huyu mtu alikuwa ni m/k wa umoja wa vijana, alikuwa diwani, pia alikuwa na kitambulisho feki cha mwewe, kote huko lazima tu kuna watu aliwaumiza kwa jinsi kariba na utashi wake unavyoonekana.
Sasa wale ambao waliumia kupitia yy ndio mnakutana huko hali inakuaje?
Funzo: tunapokuwa na nafasi aidha ya madaraka au fedha, tujaribu kuwaza na kesho yetu, haya maisha tunaishi tu lkn hatujui kitu gani kitatokea dk 10 zijazo.
Yupo mmoja aliwahi kutamka kwamba yy ni raia anaye kula raha kuliko mtanzania yoyote hapa nchini, aliesema hayo kipindi akiwa na madaraka ya kulevya.
Lkn sasa inasemekana anaishi kama digidigi haonekani mtaani, mda wowote anaingia nyavuni, kama siyo system basi wale aliowatendea ndivyo sivyo, hana amani tena ,
Tuishi vizuri kwenye ardhi hii sote ni wapitaji tu.