Namshukuru Mungu nimeweza nimefungua Radio ya mtandaoni (online Radio)

JESUS NEWS RADIO

Senior Member
Joined
May 21, 2025
Posts
124
Reaction score
158
Kwa muda mrefu moyoni mwangu nimekuwa na tamanio moja kubwa – kuitumikia jamii kwa njia ya Injili kupitia vyombo vya habari. Leo hii naandika nikiwa na furaha kuu moyoni, nikimshukuru Mungu kwa kuniwezesha kutimiza ndoto hii: JESUS NEWS Online Radio imezaliwa na ipo hewani sasa!

Hii ni redio ya mtandaoni yenye kusudi moja kuu: Kumwinua Yesu Kristo kwa kila namna, kwa kila taifa, na kwa kila kizazi. Kupitia nyimbo za Injili, mahubiri yenye Neno la kweli, maombi ya kiroho, na vipindi vya kuinua moyo, tunalenga kuwa sauti ya tumaini kwa wale wote wanaohitaji faraja, upendo, na nuru ya Mungu katika maisha yao.

Ninakukaribisha kwa upendo mkubwa usikilize, ushiriki na utuunge mkono kwa maombi. Huu ni mwanzo tu – lakini kwa neema ya Mungu tunaamini yatatimia makuu.

Sikiliza moja kwa moja hapa: [Jesus News Radio]

Maoni yako ni ya muhimu – tujulishe umeisikiliza na umebarikiwa vipi.

Namshukuru sana Kigger kwa Post yake alinipa hamasa sana, lakini pia amenipa support kwa 100% hadi kukamilika Kwa Kituo hiki Mungu ambariki sana.

[Jesus News Radio]
 
Sasa mkuu wangu, unatumikia jamii ya watanzania kwa kiingereza?

Embu jifikirie kwenye hilo, kwanini usibadili maudhui kwenda kiswahili? Ni ushauri tu
 
Mkuu sio Jesus News ni Jesus’s news.
Sasa kama hata jina la radio yako umekosea kweli embu fanya marekebisho au andika kwa kishwahili tu.
 
Sasa mkuu wangu, unatumikia jamii ya watanzania kwa kiingereza?

Embu jifikirie kwenye hilo, kwanini usibadili maudhui kwenda kiswahili? Ni ushauri tu
maudhui yake ni kwa kiswahili Mkuu. Ila kwenye upande wa nyimbo kuna muda wa Nyimbo za Kiingereza,kiswahili, zaki-naija n.k
 
Kwa muda mrefu moyoni mwangu nimekuwa na tamanio moja kubwa – kuitumikia jamii kwa njia ya Injili kupitia vyombo vya habari. Leo hii naandika nikiwa na furaha kuu moyoni, nikimshukuru Mungu kwa kuniwezesha kutimiza ndoto hii: JESUS NEWS Online Radio imezaliwa na ipo hewani sasa!

Hii ni redio ya mtandaoni yenye kusudi moja kuu: Kumwinua Yesu Kristo kwa kila namna, kwa kila taifa, na kwa kila kizazi. Kupitia nyimbo za Injili, mahubiri yenye Neno la kweli, maombi ya kiroho, na vipindi vya kuinua moyo, tunalenga kuwa sauti ya tumaini kwa wale wote wanaohitaji faraja, upendo, na nuru ya Mungu katika maisha yao.

Ninakukaribisha kwa upendo mkubwa usikilize, ushiriki na utuunge mkono kwa maombi. Huu ni mwanzo tu – lakini kwa neema ya Mungu tunaamini yatatimia makuu.

Sikiliza moja kwa moja hapa: [Jesus News Radio]

Maoni yako ni ya muhimu – tujulishe umeisikiliza na umebarikiwa vipi.

Namshukuru sana Kigger kwa Post yake alinipa hamasa sana, lakini pia amenipa support kwa 100% hadi kukamilika Kwa Kituo hiki Mungu ambariki sana.

[Jesus News Radio]
Usisahau kumshukuru na Mama pia, ni muhimu
 
Back
Top Bottom