Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mama yetu hajui ashike lipi na aache lipi, kila kona wamejaa machawa, ambao wako kumtumia tu, wakiwa gizani wanamdharau, wanamtukana, kumhujumu na kumchafua.
Kwa sasa hajui nani ni rafiki na nani ni adui, ni vurugu tupu. Mama Samia pamoja na kuwapa vyeo vya dezo bado watu wale wamekosa shukrani, wanamnanga balaa.
Sasa wameanza kuumbuana, kutajana na kuchomeana utambi, muda sio mrefu huenda wakaanza kuangamizana.
Wenye hekima, mapema sana tulimwambia mama afanye haya kabla mabaya hayajamkuta:
1. Awape watanzania katiba mpya (Hatajuta milele)
2. Ateuwe watu wapya, makini na wasafi (Watamsaidia sana)
3. Aache kabisa kukumbatia makupe, chawa na waovu (Hao watu ni sumu)
4. Asikilize sana watanzania wanasema nini (hasa walalahoi, wapinzani, taasisi za kiraia nk)
5. Asikubali kutishwa na kubabaishwa na makada wa CCM (Yeye ni rais kamili, hakuna mwenye nguvu au mamlaka ya
kuingilia maamuzi yake kikatiba)
Mama yetu akashupaza shingo, ngoma sasa imewamba, inataka kupasuka.
Muda bado upo, nafasi ya kurekebisha bado anayo, watanzania wazalendo wakumuunga mkono tupo ikiwa atabadilika.
Pole mama Samia!