Habari waungwana!
Namtafuta rafiki yangu kipenzi Rehema Abdallah Moris mara ya mwisho kuwasiliana nae ni mwaka 2011 kama sijasahu.
Tulikuwa na urafiki wa karibu sana mara nyingi nilikuwa namtembelea shekilango tunapiga stori zetu ubungu plaza hotel,stand shekliango au kwenye migahawa ya maeneo hayo pia alikuwa anakuja kwetu manzese.
Huyo binti nakumbuka alienda kusomea ualimu wa shule za msingi kwenye chuo kimoja kipo mtwara baada ya hapo akapangiwa kazi wilaya ya kilosa mkoani Morogoro
Akaja kuingia kwenye ndoa na kuzaa watoto mapacha,mama mkwe wake alikuwa anaishi Dodoma ,ndoa yake iliingia kwenye migogoro mingi sana Rehema akawa ananisimulia anayopitia kwenye ndoa mwishowe ndoa ilivunjika.
Mara ya mwisho tunawasiliana alikuwa na mpango wa kuhama toka Morogoro kuja kufundisha Dar es Salaam nafikiri ilikuwa wilaya ya Temeke.
Kwasasa mimi sikai Dar es Salaam naishi kigoma.
Nimemtafuta sana.............na naendelea kumtafuta.