namtafuta rafiki yangu wa kitambo

namtafuta rafiki yangu wa kitambo

huzayma

Senior Member
Joined
Mar 14, 2011
Posts
126
Reaction score
31
Namtafuta.
sijuwi nitamuona wapi na vipi, nikiwa msichana wa miaka 16 tulikutana kariakoo ZANZIBAR kwenye viwanja vya sikukuu, siku ya pili tulikutana hapo hapo na kuelekea alikokuwa akiishi, kunaitwa Kilimani, tokea hapo hatukuonana tena miaka mingi imepita.wakati huo hakukuwa na simu za mikononi , hatukuwa na mawasiliano tena na vile alikuwa mgeni pale ZENJ , alihama na kupotea moja kwa moja. hivi nitampata kweli ?
 
weka details zake huenda yumo humu, atakuPM. Kulikuwa na kipindi RFA cha kutafuta watu check huko pia; otherwise facebook pia husaidia sana kama uliweka details zako vizuri!
 
Nami namtafuta swahba wangu Juma Ngalanda,mara ya mwisho tuliachana Dodoma mwaka 2001
 
Sasa unamtafutaje mtu bila kumtaja jina? gender, kama unaenitafuta ni mie ? Nitajuaje ? Weka thread vizuri.
 
Nashauri watawala wa JF waangalie uwezekano wa kuunda jukwaa la 'Lost and Found' ambapo wanachama waliopoteana na watu wao wa zamani watafunguka huko.

Maana huwezi jua unaweza ukawa ulipotezana na mtu kwa muda mrefu na kumbe wote mkawa wanachama hapa JF.
 
Wazo zuri NYANI
Nashauri watawala wa JF waangalie uwezekano wa kuunda jukwaa la 'Lost and Found' ambapo wanachama waliopoteana na watu wao wa zamani watafunguka huko.

Maana huwezi jua unaweza ukawa ulipotezana na mtu kwa muda mrefu na kumbe wote mkawa wanachama hapa JF.
 
Namtafuta.
sijuwi nitamuona wapi na vipi, nikiwa msichana wa miaka 16 tulikutana kariakoo ZANZIBAR kwenye viwanja vya sikukuu, siku ya pili tulikutana hapo hapo na kuelekea alikokuwa akiishi, kunaitwa Kilimani, tokea hapo hatukuonana tena miaka mingi imepita.wakati huo hakukuwa na simu za mikononi , hatukuwa na mawasiliano tena na vile alikuwa mgeni pale ZENJ , alihama na kupotea moja kwa moja. hivi nitampata kweli ?

ungemtaja kwa jina labda ungepata msaada zaidi.....kama hayupo JF labda kuna mtu anamfahamu atamwambia.....
 
Nashauri watawala wa JF waangalie uwezekano wa kuunda jukwaa la 'Lost and Found' ambapo wanachama waliopoteana na watu wao wa zamani watafunguka huko.

Maana huwezi jua unaweza ukawa ulipotezana na mtu kwa muda mrefu na kumbe wote mkawa wanachama hapa JF.

hapo umeongea.
 
ungemtaja kwa jina labda ungepata msaada zaidi.....kama hayupo JF labda kuna mtu anamfahamu atamwambia.....

namtafuta rafiki yangu anaitwa preta. Mara ya mwisho tuliona tar 18 dec 2011 saa 7:18pm kwa saa za africa mashariki. Atakayemuona anijulishe. Ahsante.
 
Hivi kwa nini lakini we Mwajuma? Yaani huwezi kujizuia kuchakachua sredi za watu....
 
Duuh mi pia nimekutafuta sana, 2lipoachana 2 nilipelekwa songea, ila kwa sasa naishi mbeya, waweza kunipata kwa anuani zifuatazo
1. Box no. 232 Mbeya.
2. Simu no. 0655049650
3.au barua pepe; mtalingolo@gmail.com...
 
Nashauri watawala wa JF waangalie uwezekano wa kuunda jukwaa la 'Lost and Found' ambapo wanachama waliopoteana na watu wao wa zamani watafunguka huko.

Maana huwezi jua unaweza ukawa ulipotezana na mtu kwa muda mrefu na kumbe wote mkawa wanachama hapa JF.

TRUE NYANI yawezekana hata mkawa mna'shere nae comment wakati hamjijui !
 
Ndio mimi unayenitafuta. Kumbe bado wanikumbuka eeeenh!
 
namtafuta rafiki yangu anaitwa preta. Mara ya mwisho tuliona tar 18 dec 2011 saa 7:18pm kwa saa za africa mashariki. Atakayemuona anijulishe. Ahsante.

na mimi namtafuta Husninyo,mara ya mwisho nilikuwa naye Namnani gest sinza.
 
Back
Top Bottom