Namtafuta sana anayewadanganya Mashabiki wa Simba SC kuwa Kaizer Chiefs FC ni 'wepesi' na 'utopolo' mno kama walivyo Yanga SC

Namtafuta sana anayewadanganya Mashabiki wa Simba SC kuwa Kaizer Chiefs FC ni 'wepesi' na 'utopolo' mno kama walivyo Yanga SC

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwa kuwafuatilia Kwangu kwa Jicho la Kiufundi naliomba Benchi la Ufundi la Simba SC lifanye Maandalizi makubwa ikiwezekana hata kuliko yale waliyoyafanya ilipocheza na Al Ahly hapa Dar es Salaam.

Wana Winga zao ( Viberenge ) Wawili ambao nina uhakika Siku hiyo akina Kapombe na Tshabalala wajipange kweli kweli kwani 'Jamaa' wanateleza na Chaki hadi hatari.

Wana 'Mido' yao moja hiyo ni 'Fundi' hasa hata huyu Chama wetu anasubiri na anajua kusambaza mipira huku akiichezesha vyema Timu yake vile atakavyo.

Wana 'Hitman' wao Mmoja huyu Yeye katika mipira ya Krosi Mitano Mitatu lazima akuumize na ana uwezo kwa Kukunjuka kwa Kupiga Miwa ( Mashuti ) ya maana kokote pale na ikawa imo.

Hata hivyo Udhaifu wao mkubwa upo sana katika Beki zao za Kati na Beki wao wa Kushoto ambao kama Simba SC itayatumia vyema haya Mapungufu tunaweza Kufanikiwa.

Simba SC tunajisifu kwa Kucheza Pira Biriani ( Mpira Burudani ) ila kwa hawa Kaizer Chiefs FC huu sasa ndiyo Mchezo wao na wakati huku Tanzania tukimsifia Bernard Morrison kwa kuwa na 'Udambwidambwi' huko Kaizer Chiefs FC karibia Wachezaji wao wote ndiyo Mabingwa wa hii tena hasa pale wakiwa wanaongoza.

Ni kweli kwa miaka ya karibuni Kaizer Chiefs FC haijafanya vyema kivile ila tusijisahau kuwa Ligi ya Afrika Kusini ( PSL ) ni Kubwa na inaizidi yetu ya VPL tena kwa mbali mno hivyo hata Kiviwango wapo juu na hili tusilibishie kwani ndiyo Ukweli wenyewe.

Wakati huku Simba SC yetu tunaambiwa Mchezaji anayeoongoza kwa Kuchukua Mshahara mkubwa ni Bernard Morrison 11,000 USD ila katika Klabu ya Kaizer Chiefs Mshahara wa chini ( mwisho ) wa Mchezaji wao nimedokezwa ni 39,000 USD.

Na tukumbuke kuwa Ligi Kuu ya Afrika Kusini ( PSL ) ni miongoni mwa Ligi 'ghali' sana Duniani ndiyo maana hata Wachezaji wao wengi wakitakiwa na Vilabu vikubwa vya Nje huwa hawataki kwenda na wengi Wao husema kama ni Pesa nyingi hata Kwao Afrika Kusini katika Ligi Kuu yao huwa wanalipwa vile vile.

GENTAMYCINE sijaanzisha huu Uzi ili Kuwatisha Simba SC ( ambayo Mimi pia ni Shabiki wake ) ila nimeona nitahadharishe hili mapema tusije kuendelea 'Kudanganyana' halafu tukipata 'Vipigo' mfululizo Johannesburg ( Jozy au Gauteng ) na Dar es Salaam ( Bongo ) tukaanza kutafuta 'Mchawi' wakati ukweli ni kwamba Kudharau, Kubweteka na Kujiamini Kwetu kupitiliza ndizo zitakuwa sababu Kuu.

Yangu ni haya tu kwa hii leo akhsanteni.
 
Mpira wa Afrika kusini ni wa kawaida tulicheza na supersport mpaka wakamsajili Matola, tuliwatoa Santos wakiwa na kipa wao wa kombe la dunia beki za pembeni zinaweza kuwa tatizo lakini kocha ameshawasoma na kujua wapi atafanya nini.
 
Kaizer ni wepesi ila sio kama utopolo. Ni kuwavunjia heshima Kaizer kuwafananisha na utopolo na hakuna shabiki wa Simba au utopolo wenyewe wanaoamini kaizer ni level za utopolo.

Hata timu ambazo hazijafuzu quarter final bado ziko mbali mno kwa utopolo.
 
Jambo moja unaamini ufundi wa mashabiki au ufundi wa darosa na jopo lake lote?
 
Wasouth Africa kelele nyingi na wapo overrated na ligi yao PSL kuwa na umaarufu tuu, lakini uwezo mdogo sana kuanzua timu zao za taifa hadi vilabu kidogo mamelodi sikuhzi anajitutumua.. South kelele nyingi uwezo mdogo we angalia ule ubora wa ligi tunaosifia wanshindwa kufuzu AFCON,CHAN na ni jambo la kawaida kuona south kushindwa kufuzu
 
Back
Top Bottom