Jiko Koa
JF-Expert Member
- Jan 7, 2023
- 248
- 825
Huyu mpenzi wangu nilitaka nimuoe ila nimeahirisha. Kila nikiacha hela asubuhi, hata kama ni nyingi, lazima aitumie yote.
Mfano; Leo niliacha elfu 50 na ndani kuna shehena za unga, mchele, maharagwe, mafuta ya kupikia, unga wa ngano, viungo vyote vya mboga n.k. Lakini nimerudi nakuta imetumika yote.
Halafu vitu vinavyoonekana alinunua leo ni maziwa ya unga 400g, cocoa ya elfu 5 na tea masala ya elfu 5. Eti elfu 50 imeisha. Kwanza hivyo vitu vina umuhimu gani zaidi ya kuchezea hela tu? Yaani halafu kwao ni maskini, hauwezi amini kwanini haheshimu pesa.
Nikimuuliza, ananipandishia sauti. Nimewaza nimkatae tu.