Namuacha kwa sababu ana matumizi makubwa ya pesa

Namuacha kwa sababu ana matumizi makubwa ya pesa

Huyu mpezi wangu Nilitaka nimuoe ila nimeahirisha. Kila Nikiacha hela asubuhi, hata kama Ni nyingi lazima aitumie yote.

Mfano; leo niliacha elfu 50 na Ndani Kuna shehena za unga, mchele, maharagwe, mafuta ya kupikia, unga wa ngano, viungo vyote vya mboga n.k lakini nimerudi nakuta imetumika yote.

Alafu vitu vinavyoonekaza alinunua leo Ni maziwa ya unga 400g, cocoa ya elfu 5 na tea masala ya elfu 5 eti elfu 50 imeisha. Kwanza hivyo vitu vina umuhimu gani zaidi ya kuchezea hela tu? Yaani alafu kwao ni maskini hauwezi amini kwanini haheshimu pesa.

Nikimuuliza ananipandishia sauti. Nimewaza nimkatae tu.
Imeze hio pusita yake
 
Ila kuna watu mna gubu. Ulimwambia unamuachia hiyo pesa ni ya nini??

Ukute ulijifanya nyamiela don ukamwambia pesa ya matumizi hiyo. Bi dada akaamua kwenda kuitumia na yeye halafu unakuja kumuanzishia uzi hapa.
Kina dada wana mahitaji yao mbali ya kula ikiwemo pedi.

Lalamika endapo ulimwambia hii ni pesa ya matumizi ya nyumbani kwa siku kadhaa halafu urudi ukute kaitumia yote kabla.

Nyie ndio wale wa kuhesabu mpaka finyango za nyama.
 
Back
Top Bottom