Namuanzaje mamamkwe???

Kama humuamini basi mpigie simu mama mkweo umuulize, halafu uone impression unayotengeneza. Unashauriwa vya maana lakini hutaki. Hata kama kipato ni kidogo bado hiyo laki 5 hainunui kiwanja, so ni pesa ndogo bado!

hapo kwenye red hapo,hainunui kiwanja wapi?wakati huku kwetu unapata heka moja kabisa,jamani msidhani dar ndo TANZANIA pekee.
 
ebwana ikaushie hyo pesa ,itakupunguzia heshima kwa mama mkwe,ila ungoe na mchumba wako mueleweshe ili asiludie tena.
 
msamehe ila usirudie tena,na hili liwe funzo kwa watu wanaojitia kupenda kuliko wenzio
 
sio hoja kuwa na uchumba wa miaka 3,dunia ya sasa watu wanabadilika
 
Mkuu hii kesi yako kwa watu ambao hatuachi jiwe juu ya jiwe, nisingeweza kuipotezea ati kwa sababu tu labda huyo mama mkwe mtarajiwa ataniona wa ajabu! Kuna uwezekano mkubwa huyo bidada ametumia njuluku zako kuboresha maupendo na kisharobaro kingine! Na kama kweli mama kachukua kwa maagizo kuwa usiambiwe, yeye ndiye hana heshima kwako so hakuna la kuogopa. Kujibu swali lako; Nachukulia kuwa unajulikana kwao na msichana, piga simu kwa mama mkwe, mpe pole kwa changamoto aliyopata kazini kwake,kama hakukuwa na issue ya hivyo atashtuka kama mwanaye na atakuuliza why unampa pole. muulize; kale kamzigo kalimaliza matatizo huko kazini kwake?! Akikubali mwambie ulipata habari na ukawa verry concerned kama yataisha salama na umefurahi kuwa yamepita! Kumbuka iachie hewani hivyo, wala usijidai kumwambia kuwa asilipe! Kama itakuwa kweli kuwa alichukua utajua kuwa huyo mama hajiheshimu vya kutosha, na kama binti kakudanganya utaamua mwenyewe kama uko tayari kuoa na kuishi na kibaka wa kike! Seriously kama kisa hiki ni cha kweli, pamoja na makosa uliyofanya kumuachia mchumba atm yako, Utafanya makosa makubwa sana kupotezea sasa kwa kutaka kujionyesha kuwa wewe si bahili au kwa huo uongo kuwa hiyo ni hela ndogo sana! Hata ingekuwa laki moja how comes aitumie bila kukushirikisha??
 
Kwanza una moyo kumwachia mchumba wako hiyo kadi ya benki..Ukiacha yote, angekwambia amemsaidia mama hiyo ingependeza zaidi..inabidi ujikaze na kumuamini mama mkweo aliomba msaada..
Lakini na wewe umemwachia majaribu sana, kadi ina mapesa na wala mchumba hahangaikii kutafuta hizo pesa??!!!
 
Hahahah! it ain't funny but bare with my laughter, kama unataka mke we piga kimya tu mkuu ukirudi bongo utajua ukweli wa mambo ila kama unataka zogo na wedding date kusogezwa mbele au kukosa kabisa mke fanya kuulizia huo mkwanja sahizi.
 
...Kama unampenda huyu binti kiasi cha kuwa tayari kufunga naye pingu za maisha basi sahau tu hizo laki 5 ila umwambie asitoe pesa katika account yako bila ruhusa yako.
 
Unataka kumdai mama mkwe kwa nini wewe ndo ulimpa?vuta subra wasipokulipa potezea utapata nyingine tu!BTW unapima uaminifu wa mtu kwa kumpa pesa?pesa haina mwenyewe umekosea sana kumpa mchumba wako ATM card yako umejiamini nini kiasi hicho?
 
Haya mapenzi ya ukubwani yana shida sana, kupeana ATM card nayo ipo, dah uchumba huo kusema kweli siwezi, katika vitu confidential pesa ndo namba moja sasa itakuaje ukae na card yangu, nazan right person kugusa my ATM ni my mother as hata akitumia vipi haitoniuma as nimeshamtumia vya kutosha toka nipo tumbon 9 months mpaka naota ndevu, mambo ya atm na bank accounts kila mtu akae na ya kwake as long tu atimize majukumu yake... Laki 5 sio pesa nyingi but ni nyingi kutumika bila maelekezo na kama ni kidogo kwake kwa nini asitafute zake mwenyewe akampa mama yake...

Kuoa ni baadae sana kwa mwendo huo
 
Mkuu usisikitike sana kama hujalipa/kumalizia mahari uwaambie wakate kwenye hiyo laki 5.,hii ndiyo inaitwa "mateso bila chuki"
 
Mmmmhhh BM unaanzaje kuwakatia mpunga wazazi wa msichana kabla hujamwoa,wazazi nao wanaanzaje kupokea pesa toka kwa 'rafiki' wa binti yao?

alipofikia na huyo mdada kutoa mpunga kwa wakwe inahusu amekabidhi hadi ATM unafikiri mchezo
 
Kama wataka mke hizo laki 5 samehe tu mkuu....ni hela ndogo sana kulinganisha na thamani ya huyo ulienae....pia fanya haraka urudi na uchukue ATM yako....

hoja sio mke..hoja ni uaminifu kama mkeo mtarajiwa kakupiga bao laki 5 tu huko mbeleni mkishaoa atakufanyia nini kikubwa zaidi??
 
Bora ungamwachia maza huko bush ATM card pesa zikiisha anapanda mwenyewe Town kuliko kumwachia mwanamke amini mke ni rafiki na si ndugu.
 
kaka sahau icho kitu. Shukuru Mungu ni hela "ndogo" hiyo. Wengine utakuta na kadi katupa baada ya kukwangua chungu chote.

Aidha nalo hilo ni Jaribu Kaka, Lishinde!

Bazazi ni Bazazi!
 
Na sisi wanaume bana, tunakuwaga wa ajabu saa nyingine kwenye mapenzi. Yani ukaacha ndugu zako wote, yani wote, ukamuamini mchuchu, ha ha, bro umeliwa!

Hebu jiulize mpaka mama yake aje kufahamu ulimuachia bintiye ATM card? In short mpaka anajua walianzaje hayo maongezi na mwanae?

Wamama wengine huwa wanaongea na mabinti zao, huwauliza kama jamaa anamkwanja binti akajimwaga.

Cha ajabu, kwa nini mama amwambie mwanae asiseme? Kwani kama ni kwa nia nzuri na wewe si kama kijana wake? Kinachomfanya achukue pesa yako then usijue ni nini? Hapo kuna kitu kinaendelea kati yao, hebu chunguza hiyo familia vizuri, hao watakuwa ma-gold diggers aisee, ukioa ndo unakabidhi kila kitu kwa mkeo, sasa kwa utaratibu wa kutofahamishana unadhani ukitoa budget ya home kwako si nyingine itakuwa inapigwa panga kinyemela inapelekwa kwa maza?

Huyo mama muangalie vizuri, tena accountant? Anajua jinsi ya kumfundisha mwanae aisee. Next time acha kabisa kumuamini binadamu hata mkeo bana. Pesa yako, unaitafuta kwa shida na manyanyaso leo eti wakuambie huyo ndo mkeo mtarajiwa ni haki yake? Hakuna kitu kama hicho, we cheza na wanawake utakuja kuniambia kaka! Hao mwalimu wao ni kipofu pia ukute ana kijamaa chake ndo amekipa hizo hela nakuambia. Yaliwahi kunikuta, nipo German kimasomo nikamsainisha demu mshahara wangu by that time tulikuwa tunachukua cash kwa accountant wa shirika, kumbe yeye kanunua kiwanja kwa jina lake na akapata kibwana kikawa kinamsugua. Dada yangu ndo kunifunua akili nikamzuia ila alikula pesa ya kutosha. Ila mpaka leo tukionana nami kwa hasira huwa lazima nimdinye kupunguza machungu maana analalamika eti alikosea kuolewa na bwanake, sasa unadhani nitamsaidiaje? Napumua then akakioshe kwake mie maisha mazuri kama kawa kama dawa, nimsaidiaje sasa?

We subiri umuoe ndo utajuta, waswahili husema ukicheka na nyani utavuna mabua. We ngoja uvune zero balance ndo utaelewa.

Pigia simu mama mkwe msalimie halafu jifanye unataka umtumie pesa maana umesikia amepatamatatizo ofisini umsikie kama ata-confess.

Tafakari, chukua hatua!
 

MKUU UMEnENa ! Binafsi naKubaLiana 100% ulichosema!
 
Mkuu achana na hiyo laki 5. Wala usiidai. Kingine kama ulimwamini mchumbako kiasi cha kumwachia ATM card si vizuri kum audit na kumuuliza kuhusu natumizi mara kwa mara. Lastly, Guys trust is erned, hata kama unampenda mtu haiguarantee uaminifu wake.Kama ukimzoea mtu na kumuamini basi ndo umkabaidhi. Not because u love her but because u trust her. usichanganye mapenzi na uaminifu. Coz hata mzazi anampenda mtoto wake ndio ila anakiri wazi kuwa uaminifu ni 0 kama mtoto si mwaminifu. Pia hiyo ni njia nzuri ya kujua una mke wa namna gani coz inaonesha fedha za familia atazitumiaje
 
Kama wataka mke hizo laki 5 samehe tu mkuu....ni hela ndogo sana kulinganisha na thamani ya huyo ulienae....pia fanya haraka urudi na uchukue ATM yako....

Ni kweli mke ni wa thamani kuliko mkwanja BUT hii pia inaweza ikawa ndio njia ya kuonyesha kiwango cha uaminifu kati yao. Yaani mama anirubuni nichukue mkwanja kwenye account ya mwenzangu /haja kama ni ya joint pasipo kusema? Hii haijakaa vema kwa kweli. Mbona ni kitu cha kawaida kusaidia kama hivi?

Samahani mniite mchonganishi au vipi but ni alarm kubwa kwangu............... wakianza sasa hivi katika hili, litafikia hata lile la kuwa na figa la pembeni, usimwambie mumeo.
 
Unamuachia "mchumba" ATM card??????? Je na yeye ni mfanyakazi kama wewe? Mimi naona wewe ndiye mwenye makosa ya kumtia majaribuni huyo so "called" mchumba wako.

Mimi binafsi ilinichukuwa muda mrefu sana (takriban miaka nane hivi) kufungua joint account na Mke wangu halali wa ndoa (na kila mtu ana ATM yake) na anajua kuwa akifanya kosa lolote la kukosa uaminifu kinyume na tulivyokubaliana basi hiyo arrangement itakuwa terminated with immediate effect.

By the way huyo wa kwako ni mama mkwe au ni mama mkwe mtarajiwa?
 
Reactions: Sal
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…