Mkuu hii kesi yako kwa watu ambao hatuachi jiwe juu ya jiwe, nisingeweza kuipotezea ati kwa sababu tu labda huyo mama mkwe mtarajiwa ataniona wa ajabu! Kuna uwezekano mkubwa huyo bidada ametumia njuluku zako kuboresha maupendo na kisharobaro kingine! Na kama kweli mama kachukua kwa maagizo kuwa usiambiwe, yeye ndiye hana heshima kwako so hakuna la kuogopa. Kujibu swali lako; Nachukulia kuwa unajulikana kwao na msichana, piga simu kwa mama mkwe, mpe pole kwa changamoto aliyopata kazini kwake,kama hakukuwa na issue ya hivyo atashtuka kama mwanaye na atakuuliza why unampa pole. muulize; kale kamzigo kalimaliza matatizo huko kazini kwake?! Akikubali mwambie ulipata habari na ukawa verry concerned kama yataisha salama na umefurahi kuwa yamepita! Kumbuka iachie hewani hivyo, wala usijidai kumwambia kuwa asilipe! Kama itakuwa kweli kuwa alichukua utajua kuwa huyo mama hajiheshimu vya kutosha, na kama binti kakudanganya utaamua mwenyewe kama uko tayari kuoa na kuishi na kibaka wa kike! Seriously kama kisa hiki ni cha kweli, pamoja na makosa uliyofanya kumuachia mchumba atm yako, Utafanya makosa makubwa sana kupotezea sasa kwa kutaka kujionyesha kuwa wewe si bahili au kwa huo uongo kuwa hiyo ni hela ndogo sana! Hata ingekuwa laki moja how comes aitumie bila kukushirikisha??