Namungo FC: Tutavaa Jezi Nyeusi Jumatano Wageni wavae Njano au Kijani la sivyo watulipe Tsh Milioni 200 wavae zao Nyeusi

Namungo FC: Tutavaa Jezi Nyeusi Jumatano Wageni wavae Njano au Kijani la sivyo watulipe Tsh Milioni 200 wavae zao Nyeusi

Cognizant

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2022
Posts
626
Reaction score
1,409
Katika kuonyesha kuwa Klabu ya Namungo inaelewa Mchezo mzima wa Jezi Nyeusi za Timu Moja nayo imeweka wazi kuwa Jumatano itavaa Jezi zao Nyeusi na kama kuna Timu inataka Kuvaa Jezi Nyeusi za Mganga wao wa Kienyeji basi wawalipe Tsh Milioni 200.

Hata hivyo mpaka Mleta Uzi anaenda Mitamboni bado wapenda Kuvalia Jezi Nyeusi za Mganga wao wa Kienyeji walikuwa bado hawajaamua kama wakubali kutoa Kiasi hicho cha Fedha kwa Namungo FC ili Washinde wawaache Simba SC kwa Alama Nne au wasizivae kisha Wafungwe au Watoke Sare ili tofauti ya Alama iwe ni Moja au Mbili.
 
Kwa jinsi wanavyozitaka pointi 3, mtapewa angalau 100M.
Pesa sio tatizo JamiiForums mobile app
Na mpaka unaona Namungo FC wamewatega kwa hicho Kiasi Kikubwa cha Milioni 200 hao Watakaocheza nao Keshokutwa Jumatano Saa 1 Usiku Uwanja wa Ruangwa Majaliwa ni kwamba wanajua hawawezi Kulipwa hicho Kiasi kutokana na Ukata unaoikumba kwa sasa hiyo Timu ya Kupenda Kuvaa Jezi Nyeusi za Mganga wao Hatari wa Kienyeji.
 
Hivi Kanuni zinambeba au kanuni zinatambua jezi yako ya nyumban ni hipi na ya ugenini ni hipi? Mfano jezi nyeusi ya Yanga ni jezi ya 3 baada ya njano, 2 kijan na 3 nyeusi ila 1 ndiyo home kit
Official Jersey ya Yanga SC kwa Nyumbani ni Kijani na kwa Ugenini ni Njano na Nyeusi ni kama Dharula itokanayo na Mazingira japo kwa Kanuni za Ligi Kuu zinaipa Timu Mwenyeji Maamuzi ya Kuvalia Jezi waitakayo na ambaye waliiwasilisha TFF kabla ya kuanza kwa Msimu mpya wa Ligi.
 
Yanga imechukua ubingwa Kwa kucheza Michezo 30 mfululizo bila kupoteza.. Wala hawakuwa na jezi nyeusi..

Simba imepasuliwa ngao ya jamii mara mbili mfululizo na nusu fainali ya FA kule mwanza, Wala Yanga haikuvaa jezi nyeusi..
Yanga walivofungwa na Al Hila kule Sudan walikuwa wamevaa bukta nyeusi..

Hizi ni propaganda tu na Wala hakuna uhusiano wowote kati ya ushindi wa timu na rangi ya jezi.
 
Bongo nyoko sana huu ujinga wa matokeo ya Yanga umehamia kwenye jezi na sio bahasha tena kama ilivyokuwa awali[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
Hawa wanatumia vyote,uchawi na pesa.
Kuna mahali pesa inakataliwa,wanabakiza uchawi tu.
Kwa Ihefu pesa ilikataliwa,na jezi hawakuvaa,wakachezea koki,wakalowa

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Yanga imechukua ubingwa Kwa kucheza Michezo 30 mfululizo bila kupoteza.. Wala hawakuwa na jezi nyeusi..

Simba imepasuliwa ngao ya jamii mara mbili mfululizo na nusu fainali ya FA kule mwanza, Wala Yanga haikuvaa jezi nyeusi..
Yanga walivofungwa na Al Hila kule Sudan walikuwa wamevaa bukta nyeusi..

Hizi ni propaganda tu na Wala hakuna uhusiano wowote kati ya ushindi wa timu na rangi ya jezi.
Kwani uchawi mbafanyaje kwa mashehe wa Sudan?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Ila wewe jamaa hahahahahah
Huyu ndugu yenu kazi anayo! Kila ID anayokuja nayo humu jukwaani (baada ya ile iliyozoeleka kupigwa ban mara kwa mara kutokana na kutukana watu hovyo), ndani ya dakika 0 tu inakuwa imeshajulikana.
 
Back
Top Bottom