Namuomba Rais Samia amsaidie huyu dada aliyekuwa muigizaji

Namuomba Rais Samia amsaidie huyu dada aliyekuwa muigizaji

Sina hakika kama imeshaletwa huku au laa, ila mimi ndio nimeiona leo. Nikaona niilete hapa ili mwenye kuweza kusaidia matubabu ya mwigizaji Carina asaidie. Pengine hata tukimega pesa kidogo toka kwenye yale magoli ya Mama si mbaya sana, asaidiwe apelekwe hata India tu. Maelezo kamili yapo chini kwenye video


Wanaringia sana raia hata kusalimia wanaona kinyaa ila wakiumwa wanakuja kutembeza bakuli.
 
She calls out to the man on the streets....
Sir can you help me!...
It's cold and I've nowhere to sleep...
Is there somewhere you can tell me?
He walks on, doesn't look back!...
He pretend he can't hear here!....
Start to whistle as he crosses the street!....

Tujaribu kuchangia pale tunapoweza wakuu....jikune pale mkono unapofikia....nimetoa 1,000...

Think twice.... there's another day for me and you in Paradise!....

🎶Itika anapokuitaa ....Saidia unapoweza...dunia...yabadilika hujui lini utaanguka!🎶....

As a music lover.....ujumbe wangu nimeusindikiza na lyrics zenye kuchoma moyo....!🙏
 
Mungu amfanyie wepesi ni video queen aliyenivutia sana na kisura chake cha upole,
 
Sina hakika kama imeshaletwa huku au laa, ila mimi ndio nimeiona leo. Nikaona niilete hapa ili mwenye kuweza kusaidia matubabu ya mwigizaji Carina asaidie. Pengine hata tukimega pesa kidogo toka kwenye yale magoli ya Mama si mbaya sana, asaidiwe apelekwe hata India tu. Maelezo kamili yapo chini kwenye video


Pole zake na Mungu tunaomba umponye. Ila haya mambo inatakiwa tuyaangalie kwa upana wake. Kwa nini unaona huyu msanii ndiye mwenye haki ya kusaidiwa wakati kuna watanzania wengi wenye matatizo kama haya? Ni kigezo gani umetumia? Kwa vile alikuwa msanii? Mbaya zaidi hawa wasanii ndiyo wanatumika kuwasaliti wananchi kwa kujigeuza machawa wa watawala? Jamani haya mambo ya kupinga utawala mbovu bila kushirikiana wote ni suala la muda tu, kila mtu litamfika kwa wakati wake. Watawala wetu wangekuwa ni watu wa kujali wagonjwa kama hawa kungekuwa na utaratibu wa kuwashughulikia bila kuomba msaada. Hebu tuungane kudai uwajibika ili kuepuka mambo kama haya. Inasikitisha sana kuona dada mwenye umri mdogo kama huyu anateseka wakati kuna fedha zinachezewa kwa kununua magari ya kifahari na kulipa wabunge wa mchongo wasiona faida yoyote kabisa. Hivi fedha zote zilizotumika kulipa hao covi-19 si zingeweza kutumika kusaidia wagonjwa kama hawa?
 
Loftins! Unataka kuona video ya mwenzio akiteseka ndio utume mchango wa matibabu!
Huwezi amini kwenye Thread ya jamaa hapo juu naona maelezo tu hadi sasa.
Ila naziona za comment #9 na #11

Anyway Mungu ni wetu sote atainuka siku moja
 
Back
Top Bottom