Namuombea Fiston Mayele afanye vuziri kimataifa

Namuombea Fiston Mayele afanye vuziri kimataifa

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Leo nimesoma comment za wakongo kuhusu Fiston Mayele. Pamoja na kuwa Mayele hapa kwetu tunamuona King wa Goals, kwao Kongo kule kuna watu hawamkubali kabisa na kila akifanya vizuri kazi yao ni kusema ligi ya Tanzania ni dhaifu ndo maana anafanya vizuri.

Ila kinachonishangaza Fiston Mayele kwenye ligi ya Kongo alifunga mabao 14 msimu mzima na kuwa mfungaji namba 2 wa ligi “ngumu”; sasa kwanini wanamuita dhaifu?

Any way nabii hakubaliki kwao. Hata Messi kuna kipindi alitaka kustaafu kwenye timu ya taifa kwasababu ya maneno ya ndugu zake.

Na kingine Kongo kuna ukabila sana. Watoka Kinshasa hawataki watoka Lubumbashi wawe juu na watoka Lubumbashi hawataki watoka Kinshasa wawe juu.
 
Tuwekee goli la mayele la kimataifa hapa ili mada yako iwe vizuri iendane na uhalisia.
Goli la kimataifa Alifungwa Kaseja mechi ya Tanzania vs DRC pale Kwa Mkapa, Mfungaji wa Congo DRC alikua Fiston Kalala Mayele.
 
Goli la kimataifa Alifungwa Kaseja mechi ya Tanzania vs DRC pale Kwa Mkapa, Mfungaji wa Congo DRC alikua Fiston Kalala Mayele.
Kwa hyo sasa hivi yuko team ya taifa utopolo bwana ndio maana mnaambiwa wenye akili ni wawili tu.
 
Drc ina ma professional players wengi mno dunia yote hicho ndicho kinachowachanganya baadhi ya wa congo kumuona jamaa wa kawaida lakini si hivyo..
Huyu mwamba angeipata chance aliyeipataga Samatta aston villa hakika tungeongea mengine hapa saa hii

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Huo ndiyo ukweli. Transfer kutoka AS Vita inayoshikilia nafasi ya 9 Africa kwenda kwenye Utopolo inayoshikilia nafasi ya 392 inadhihirisha hili jamaa limekuwa dhaifu kupindukia
 
Drc ina ma professional players wengi mno dunia yote hicho ndicho kinachowachanganya baadhi ya wa congo kumuona jamaa wa kawaida lakini si hivyo..
Huyu mwamba angeipata chance aliyeipataga Samatta aston villa hakika tungeongea mengine hapa saa hii

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
striker alitezidiwa magoli na George mpole
 
Tuwekee goli la mayele la kimataifa hapa ili mada yako iwe vizuri iendane na uhalisia.
Caf champion league group stage msimu 2019/20 akiwa na AS Vita Fiston Kalala Mayele anawafunga JS Kabile goli dk 70
Msimu 2020/2021 anawa wafunga Young buffalo goli 2 katika group stage anawafunga El Melek ya Sudani goli 1 Sasa unahitaji Nini kingine.
 
Kweli manara na kikwete ndo wenye akili mi nimekwambia goli la mayele akiwa yanga.
 
Naomba video ya goal mbili za Mayele ngao ya hisani zidi ya Simba
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom