Namuonea huruma mume wake

SIPIYU30

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,751
Reaction score
2,437
Kuna mdada nilifahamiana naye, kazini kwake siyo mbali na kwetu, so kwenye pita pita ndo nikamfahamu, kuna wakati changamoto za usafiri huwa nampa lifti baadhi ya siku. Kama ujuavyo wanaume, nikachokoza nione vp atakubali au la.

Akaniambia yeye ameolewa na ana mtoto. Nikaendelea kumbana akasema hawezi kwa sababu pia anafahamiana vzuri na mke wangu so likitokea lolote itakuwa soo mbaya sana. Alivyosema vile sikuona haja ya kufukuzana naye, hata hivyo urembo wake haukuwa wa kunikatisha usingizi kivile.

Tukabaki tunawasiliana hapa na pale. Sasa siku za karibuni nikaona amejiunga tiktok kwa jina lingine tofauti na nililozoea, ila katupia picha kadhaa mle. Nikawa nawaza hizi picha mbona kama zake? Na mimi nikafungua akaunt tiktok na mimi nikaweka ID fake na sikuweka picha. nikamuunga, tukaanza kuchat tiktok.

Taarifa zote alizonipa kumuhusu nyingi zilikuwa sahihi kasoro tatu tu. Uongo wa kwanza, akasema yeye yupo tu mtaani hafanyi kazi yoyote. Pili, akadanganya kuwa yeye hajaolewa, aliolewa ila mumewe alifariki kwaajali. Hii iliniacha hoi maana mumewe hadi kazi yake naijua. Tatu akadanganya jina lake kakomaa na hilo jina lililopo Tiktok.

Sasa nikamtongoza humo humo. Amenikubalia, ila anataka nimtumie picha anione ndo tukutane. Nikamuomba namba amenipa ile ile niliyo nayo. Tukichat yaani kama namchelewesha mpaka vijiwe vya kwenda kuburudika tumekubaiana sasa anashangaa mbona simuiiti? Sasa mimi nimeamua picha simtumii, na simu simpigii maana namba zangu anazo.

Namuonea huruma mume wake siku akijua mkewe kashamtamkia kifo tena ya ajali wakati yupo na anadunda mtaani.
 
Nawewe ni mume wa mtu TikTok unafuata nini🤣🤣🤣
 
Huyo ni Malaya anajiuza.
Malaya aliyebahatika kuingia kwenye taasisi ya ndoa,na hawa ndiyo wanaifanya hii taasisi ionekane haina maana.

Pia kuna umuhimu mkubwa wa vijana wanaotaka kuoa kuwashirikisha wakubwa zao wawasaidie jambo hili,ukimuuliza mumewe huyu historia ya kukutana kwao atakwambia walikutana chuo au kazini which is hizi siyo sehemu sahihi za kukutana na mke pia wale wanaokaza sana kuhusu suala la wanaume kuoa bikra waungwe mkono.
 
Kabisa mkuu
 
adulterer
 
Sasa mkuu uongo wake na wako hapa una tofauti gan? Maana na wewe una id fake
 
Mimi namuonea huruma mke wako.
 
Nakazia
 
Unaweza Kuta hata masela wengine wanaomzagamua mke wako wanakuonea huruma pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…