Nanauka: Serikali inatazamia kuanzisha benki ya Vijana

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka amesema serikali inaendelea na utafiti wa kuanzisha Benki ya Vijana itakayolenga kutoa huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya vijana Nchini.

Amesema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuweka msingi imara wa taasisi maalum ya kifedha itakayowawezesha Vijana kupata mitaji kwa urahisi.

Soma kuhusu Bajeti: Wizara ya Vijana yaomba Tsh. Bilioni 35.9 kuimarisha Maendeleo ya Vijana 2026/27

“Dhamira ya Serikali ni kuweka msingi wa mfumo wa kifedha unaoendana na mazingira na uwezo wa vijana wengi, hususan wale wanaoanza shughuli za kiuchumi, ili kuondoa vikwazo vilivyopo katika upatikanaji wa mitaji.

Benki ya Vijana, itakayoanzishwa, itakuwa chombo muhimu cha kimkakati kitakachowezesha upatikanaji wa huduma za kifedha zilizo rafiki kwa vijana, kuchochea ubunifu wa bidhaa za kifedha zinazolingana na mahitaji yao, kupanua wigo wa uwekezaji wa vijana, na hatimaye kuongeza ajira na mchango wa vijana katika kukuza uchumi shindani na jumuishi wa Taifa,” Nanauka - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana.

Your browser is not able to display this video.

​
Michango ya Wabunge kuhusu Bajeti ya Vijana:
 
😊😃😁😀😅😆😂😄😎😎Watanzania Siyo Wajinga
 
Hawa watu mbona wanaongea ujinga san...

What happened kwenye benki ya Wakulima
Nliwahi kwenda hapo,zamani za 2017 nlivyomaliza advance tu,nlipewa hisabati za hatari na mdada flani hivi mwenye figa tata,ni kama walikuwa wananifukuza kabisa hivi!!!
 
Huyo sio waziri, ili mtu awe waziri lazima achaguliwe kuwa mbunge.

Sasa huyo Nanauka kachaguliwa kwenye uchaguzi upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…