Nandy anazidi kupotea

WATU HAMKUJUA WAKATI NANDY ANAACHIA AUDIO YAKE NA KOFFI NA WCB NAO WAKAACHIA SCANDAL YA RAY NA PAULO WATU WAKKACHA KUONGELEA NANDY NA KOFII IKAWA RAY NA PAULO HATA HII VIDEO HAIWEZI KUSAIDIA KITU KWASABABU AUDIO HAIKUFA CHOCHOTE
Ila mzee umeongea kiukali sana. Hapo mtoa mada angekua jirani angekula kofi zito..
 
Yote 9, Kumi ebu tumshauri kijana mwenzetu. Maana akipotea yeye hujui wangapi wanakosa ajira nyuma yake.

Me naona hajachelewa, atulie atunge pini nyingine kali. Tena akifanya mwenyewe naona anaimba vizuri kuliko ata kukazana kushirikiana na majina makubwa mjini. Wimbo pekee alioshirikiana ukasumbua mtaani (ingawa mi sikuupenda) alioimba na Harmonize.

Pia video zake nyingi za indoor naona sio nzuri. Ajaribu na outdoors kama Kivuruge.
 
mkuu hakuna mafanikio bila changamoto, watu wenye mind za mafanikio daily hujitahidi kuziwin changamoto ili wafanikiwe zaidia

domo kapitia changamoto nzito sana kunako game bt 95% kaziwin ndo maana bado yupo pale juu, nandy anapaswa kuziwin challenge na sio kulalama/ kumtafuta mchawi
 
Ni wapi Nandy kalalama ??

Kama tukivyokuwa tunamtetea Diamond dhidi ya Ruge, hivyo hivyo tutamtetea Nandy, Harmonize, Alikiba au yeyote anayepambana.

Kuna mijitu mikatili ya nafsi, ilikuwa inamuona Ruge adui kumbe ni afadhali hata ya Ruge.

Maana Ruge ulikuwa ukikosana naye anakuacha tu, ila hata hii mishetani yenye midomo mipana kukubania tu haitoshi baali inatumia watu kupambana na wewe mpaka uvunguni.
 
Kipindi kile chini ya "Jasiri muongoza njia",nyimbo alikuwa anaandikiwa na melody anatungiwa kazi yake yy kugandamizia.

Sasa hivi hiko kitonga hakipo,cha msingi akae chini na waliokuwa wana mwandikia aingie nao mkataba wagawane asilimia,akifanya masihala atakuwa kama Baraka da Prince.
 

Kwanza nikwambie kwamba uelewa wako kimziki ni wa kawaida sana. Kama layman wengine. Pili kama unachambua mziki ki zembe hivi haina haja ya thread nyingine uliyohaidi maana itakuwa na hoja dhaifu kama hii.
Back to the point. Huwezi kupima ukubwa ama udogo wa msanii kwa kigezo You Tube Viewers. Utakuwa unamdhalilisha msanii na kazi zake. Kuna wasanii wengi wazuri sana Africa,America, Europe na Asia. Wanatoa nyimbo nzuri lakini Viewers ni kidogo. Je na wao wameshuka kimziki. Kuna vigezo ambavyo ni common kwa kupima ukubwa wa msanii kama
1. Shows Msanii kuandaa mwenyewe ama kuandaliwa shows na zikawa kubwa kwa uhudhuriaji wa shabiki hiki kigezo hutumika kwa wenzetu. Mahudhurio ya wadau kwenye shows huweza kumpandisha ama kumshusha msanii
2. Album, kutoa ,mauzo na umaarufu wa album aliyotoa .huweza kumpandisha ama kumshusha..kulingana nakala alizouza ama na kutoa.na umaarufu wake
3. Consistency & maintaining ya msanii toka alipojulikana mpaka muda anaoendelea kufanya mziki wake.
4. Endorsement ,ya msanii na brand yake local and international. Hizo ndo common..na nyingine nyingi ikiwemo na hiyo ya Viewers (minor)
..sasa hivyo vigezo Nandy vyote anavyo kwa ukubwa sana. Na hakuna msanii yeyote wa kike Tanzania kwa sasa mwenye. Endorsement na Shows kubwa kumzidi..anaandaa mwenyewe mara nyingi Nandy.
#Ameshafanya tour yake..na ikafanikiwa
#Matangazo ya mengi
Video zipo wazi

Najua wengi mtamzungumzia Zuchu..yes she hot and running the industry..lakini jiulize bila back up ya diamond anaweza kuwa hapo alipo. Kwa nandy alifariki mentor wake na ruge aliyekuwa anamsupport sana ...but still bado anafanya makubwa . Mpaka collable ya over 60s Tzs million. Akiondoka diamond Zuchu anaweza fanya hicho kitu. Absolutely nope.
Note:kabla ya kusema Nandy kashuka jiulize na kuangalia mambo mengi. Tanzania kwa sasa haina msanii wa kike mwenye kufikia uwezo wa Nandy.
 
mtu yeyote mwenye mafanikio/mwenye mind ya mafanikio anajua fika changamoto ndo njia ya mafanikio hivo unachoandika hapa kinadhihirisha maneno ya waliofail na kukata tamaa kimaisha maana watu wenye mind za mafanikio hawanaga mitizamo ya namna hii.
 
mtu yeyote mwenye mafanikio/mwenye mind ya mafanikio anajua fika changamoto ndo njia ya mafanikio hivo unachoandika hapa kinadhihirisha maneno ya waliofail na kukata tamaa kimaisha maana watu wenye mind za mafanikio hawanaga mitizamo ya namna hii.
Hata mwenye mafanikio ambaye ni msukule wa mtu.
 
Naungana na wewe kuhusu Nandy lakini Unajuaje kama zuchu akitoka hapo hawezi kufanya chochote? Kama umemtetea Nandy ambae amebebwa na Ruge muda mrefu n sijui umetumia kigezo gani kumshusha zuchu kwamba hawezi wakati uwezo wake umeukubali.
 
Kwa sasa yaani eti YouTube ndo kipimo cha muziki mzuri

Wangapi hawana smartphone ?
 
Bwana nyie wengine mnakua kama motivation speaker, Hamtaki nguvu ya muziki wa bongo upimwe kwa vigezo cha kupata watazamaji wengi youtube mnataka tupime kwa kigezo gani? kuingia kwenye charts za Billboard au?

Kibongo bongo kuna vigezo vya kupima nguvu ya muziki wa msanii husika na youtube pia ipo, ukitaka kuamini hata wasanii wenyewe wanaona ni achievement kupata watazamaji wengi huko. Vigezo vingine vipo lakini hiko hatuwezi kukiignore.

Nandy ni msichana mdogo, ana safari ndefu bado, akiharibu asaidie sababu akifulia mimi, wewe na mwingine hatutafaidika na chochote, zaidi atapata hasara yeye na kundi la watu aliowapa ajira za kudumu na za muda mfupi. Binafsi naona Nandy apambane kupata nyimbo zilizotungwa vizuri ili akiweka sauti yake inakuwa boom, hana way nyingine out. Infact wasanii wengi wadogo hata hao walipo WCB wapambane sana katika utunzi bila hivyo watu watawazoea na kuwapotezea. Kuimba nyimbo nyepesi nyepesi wamwachie Diamond, sababu kwa jina lake yule kinasikilizwa chochote hata kama ni utopolo. Waige kwa Zuchu, binafsi si shabiki ake lakini anasikilizwa sana sehemu nyingi unapopigwa mziki, Nandera apite humo humo kama ilivyokuwa zamani chini ya jasiri muongoza njia.
 
Siongei Kishabiki, Ila kiukweli Nandy ana sauti nzuri sana sana kuliko ata Zuchu

Ila Zuchu ana mashairi makali sana sana sana sana, hili halina ubishi
 
Siongei Kishabiki, Ila kiukweli Nandy ana sauti nzuri sana sana kuliko ata Zuchu

Ila Zuchu ana mashairi makali sana sana sana sana, hili halina ubishi
Na ukitaka kudumu kwenye mziki uwe na mashairi.Ruby ana vocal kali kuliko wasanii wote wa kike,ila hajui kutunga.

Yeye Nandy anatakiwa awatumie watu walewale waliokuwa wakimtungia zamani na awalipe vizuri,la sivyo atakuwa kama Ruby au Baraka da Prince.
 
Million 70 kwa wimbo gani au video gani?
Nandi alikurupuka kumshirikisha huyo kofi, pia aache kuimba kwa kubana pua
 
Million 70 kwa wimbo gani au video gani?
Nandi alikurupuka kumshirikisha huyo kofi, pia aache kuimba kwa kubana pua
Nandy habani pua dada yangu sauti yake ni natural ,tatizo lake ni moja sio mtunzi mzuri.
 
Basi hapo mmeanza kumshindanisha na mtu... Ovyo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…