Ok, tujadili hizo hoja.
Hiyo hoja ya kwanza ya kusema kuwa filamu haifanyi vizuri hivyo yeye kuchanganya filamu na bongo fleva haina uhalisia kwa sababu hujaeleza ni kwa jinsi gani kutokufanya vizuri kwa filamu za Tanzania kutafanya yeye ashuke katika bongo fleva. Au watu watasema “fvck! Nandy ameanza kuigiza!? Mimi sipendi bongo movie kwa hiyo kama nandy ameanza kuigiza basi sifuatilii muziki wake” (kitu ambacho hakina uhalisia). Au atawekeza sana kwenye filamu na atapotesa focus kwenye muziki? Hii nayo haonekani kufanya kazi kwa sababu sidhani kama nandy yupo serious sana filamu kiasi a’risk bongo fleva yake.
Tuje kwenye hiyo hoja ya pili kuwa bongo fleva na gospel ni falme mbili tofauti (giza na mwanga) hivyo kuchanganya ni kupambanisha falme mbili tofauti.
Kwanza kabisa, mimi siamini katika hayo mambo ya giza na mwanga, shetani sijui dhambi. Siamini katika hizo mambo so pia siamini kama hiyo vita unayoiongelea inaweza kutokea. Lakini pia dhana ya kuwa kuna madhara ya kuchanganya bongo fleva na gospel haifanyi kazi kwenye uhalisia kwa sababu kila muziki una maudhui yake na una sehemu yake. hivi kwa mfano mchungaji na mkewe wakiwa faragha, mke wa mchungaji akaamua kumuimbia mme wake wimbo wa nandy (let say ‘ninogeshe’) huku akicheza mbele yake, atakuwa anapambanisha falme mbili tofauti kwa kuwa yeye ni mke wa mchungaji na anaimba wimbo wa bongo fleva? Au nandy akiamua kutenga muda wake kuimba wimbo wa kumsifu Mungu atakuwa anapambanisha falme mbili tofauti kwa kuwa yeye anaimba bongo fleva?
Kuamini kuwa muziki wa bongo fleva ni muziki wa giza (au wa kishetani) na mziki wa gospel ni muziki wa mwanga (Mungu) ni dhana ambayo haipaswi kuendekezwa kwa sababu haina uhalisia. Watu tunapitia hali tofauti na tunahitaji mahitaji tofauti kukidhi hali hizo tofauti. Kuna wakati mtu atahitaji kusikiliza nyimbo za mapenzi na kuna wakati mtu anahitaji kusikiliza gospel. Sasa kama mtu mmoja anaweza kusikiliza bongo fleva na gopel kwa nyakati tofauti kuna ubaya gani msanii mmoja akafanya gospel na bongo fleva kwa nyakati tofauti? Na pia umeonyesha kuwa ili nandy afanikiwe ki bongo fleva anatakiwa aachane na gospel na kulingana na mtizamo wako (wa giza na mwanga) unamshauri amwache Mungu ili afanikiwe katika shetani. Wewe ni nani unayehimiza watu wafanikiwe katika shetani? Hakuna uhalisia.
Simaanishi kuwa nandy hawezi kushuka kimuziku (bongo leva) kwa kuchanganya hivyo vitatu, lakini hoja ulizoweka sidhani kama zinafanya kazi, hazina uhalisia.
Njia pekee ambayo itamshusha nandy kwa kuchanganya vitu hivi vitatu ni kama atakosa focus, kwamba leo kaacha bongo fleva kahamia kwenye gospel, muda kidogo baadaye anaacha gospel na kuhamia kwenye filamu, baada ya muda tena anaanza kufanya vyote vitatu nk nk.