Nandy, Mafiga matatu yatakuponza

Nandy, Mafiga matatu yatakuponza

Kila mtu ana kipawa, talanta na kipaji chake , lakini kati ya hivyo vitatu kimoja ndio hujitokeza zaidi na kwa baadhi viwili ndio huonekana zaidi

Talanta na kipawa hivi viko kiroho na kiimani zaidi huku kipaji kikiwa kiko kimwili na kidunia zaidi. Kwenye hii dunia kuna falme kuu mbili , ufalme wa Nuru na ufalme wa giza...ufalme wa nuru uko kiimani zaidi kwa maana ya Kimungu na ufalme wa giza uko kidunia zaidi kwa maana ya shetani ...hizi ni falme mbili zisizochangamana

Nandy binti mwenye kipaji cha uimbaji kupitia nyimbo zilizomtambulisha za kidunia alianza na kufanya vema sana kwenye hii kaliba, lakini sasa anapotea..anachanja mbuga kuelekea porini...Pengine kwakuwa jasiri muongoza njia hayupo tena..

Pressure ya kubaki kileleni, mashindano ya vipaji vipya na ugumu wa soko huku akiwa hana washauri wazuri vinaweza kuwa matokeo ya yale anayofanya sasa

Nandy kashindwa kushika moja, anachanganya mambo matatu kwa wakati mmoja
Bongo fleva
Bongo movie
Gospel
Hivi vitu vitatu huwa kamwe havipikiki chungu kimoja hata siku moja...kila kimoja kina chemistry yake, ladha yake na mashabiki yake... Lazima ujitambulishe na kukubalika kwenye moja ya makundi hayo

Kuchanganya bongo fleva na bongo movie ni kujiua kisanii kwakuwa iko wazi kabisa kuwa sisi wabongo na haya mambo ya sinema za kisasa tumefeli big time..HATUWEZI.. Sisi tuko vizuri kwenye mziki walau kwasasa

Kuchanganya bongo fleva na gospel ni sawa na kuzipambanisha falme mbili zenye kutofautiana kwenye kila kitu....leo uombe nogesha kesho uimbe Mungu ni mwema ...HUTAELEWEKA KAMWE... Utajimaliza mwenyewe

Figa tatu alizochagua Nandy hazirandani asilani..anatawanya na kupoteza nguvu zake bila kujua.....Na hapaswi kutafuta mchawi kwenye hili zaidi ya washauri wake

Shetani akizeeka huwa malaika.. Usitake kuwa malaika kabla hujazeeka. Yuko wapi Stara Thomas? Mzee Yusuph ndio huyo anatanga na njia sasa...Kuna wakongwe kama Cosmas Chidumule na Mzee Makassy hawa walipoamua kuipa dunia kisogo na kumgeukia Mungu hawakuyumba wala kurudi nyuma.

Kina TID wameamua kuingia bongo movie kwakuwa hawana nafasi tena kwenye soko la mziki...huko wanalazimisha tuu...ili walau siku zisonge

Kwa umri wake Nandy na kipaji kilichomtoa cha bongo fleva angejenga mhimili imara kwanza huko.... Wakati anahangaika na bongo movie kina Zuchu wanampiku kwenye chart za umaarufu...!!!

All in all kama kaamua moja la kumrudia Mola wake na kuimba Gospel katika umri huo , awe na nia thabiti ya kiroho asije akageuka na kurudi alikotoka...ataishia kuchanganyikiwa... Kumrudia Mungu ni vita sio bata... Amuige Hafsa Kazinja...

Kama anashaurika basi atulie na kuanza upya na ashike moja tuu kwakuwa mshika mawili moja humponyoka...sasa yeye kashika matatu kwa mpigo...!!!

Nadhan suala la kumuimbia na kumsifu Mungu halina mpaka kwa sababu yeye ndo muweza wa kila kitu , wengine tunaroga usiku kucha ila Mungu pia tunamuomba kwa kuwa ndie muweza wa yote

Nadhan kwa anayopitia sasa hiv kaamua kujifariji kwa kumtukuza Mungu ukizingatia nandy katokea familia ya kidini na zaman alikua anaimba kwaya kanisani, hizi nyimbo za dunia yupo kibiashara tu
 
Ebwanae umeongea vzr sana sina neno la kutia,Nandy nafikiri katokea kwny familia za zilizoshika dini sasa huenda kuna msukumo kutoka katika familia unaomkosoa kufanya nyimbo za kidunia,so kuacha ameshindwa na kuamua kushika vyote,
Hata hivyo Mungu amekataza michanganyo ya hivyo,Nusu kwenye dunia nusu unamtumikia
Kuna mistari kwny biblia inasema bora kuwa wa baridi au moto kuliko kuchagua vuguvugu
Nandy anachofanya nikuamua kuwa vuguvugu.
Nadhan suala la kumuimbia na kumsifu Mungu halina mpaka kwa sababu yeye ndo muweza wa kila kitu , wengine tunaroga usiku kucha ila Mungu pia tunamuomba kwa kuwa ndie muweza wa yote

Nadhan kwa anayopitia sasa hiv kaamua kujifariji kwa kumtukuza Mungu ukizingatia nandy katokea familia ya kidini na zaman alikua anaimba kwaya kanisani, hizi nyimbo za dunia yupo kibiashara tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila bongo dah.. hakika tunaijua dini kuliko walioileta.. kiusanii, leo ndio nasikia msanii fulani akiimba aina fulani ya muziki hapaswi kuimba aina hii..

Ni mara mia moja hata huyu Nandy kaamua kumkumbuka Mungu, atakuwa na jambo la kusema ktk sanaa yangu nilimtukuza Mungu kwa kuitumia sauti yangu kufikisha neno lake kwa watu, hawa wasanii kaka ukiyajua maisha yao na wanayopitia, itoshe kusema hongera Nandy.

Mimi sioni tatizo, hili jambo lipo sana sana tu, mkuu Tasha Cobbs ana ngoma kafanya na Nicki Minaj na Nicki kachana tu fresh, na ngoma ni kali tu je Tasha Cobbs kazingua kuupeleka muziki wa dini ktk muziki wa kidunia (rejea mwonekano na maisha ya Nicki)?

Kwahiyo kwa maoni yangu binafsi sioni shida, rejea Luka 5:31 - 32

Yesu akawajibu, “Wenye afya hawamhitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”
 
Una kipaji cha kuandika[emoji23], Hapo nikisamaraizi natoka na aya moja.
 
Nandy fanya yote ndani ya uwezo wako,kuna time itafika YOU CAN'T DO SHIT,utabaki i could have done this or that..hapo umezeeka, fanya YOTE sema kuwa ORGANISED ,and consistent...
 
Binafsi mimi namwelewa sana nandy kwa sababu mimi ni moja ya watu ambao ni mult-talented. Kwa yeyote mwenye vipaji zaidi ya kimoja atanielewa. Hauwezi kusema ukiache kimoja au viwili ili ubaki na kimoja....kamwe huwezi. Kipaji ni aina flani ya ulevi, hauwezi kukitelekeza kipaji kimoja kirahisi hivyo hasahasa kama vipaji hivyo vinahusiana kwa ukaribu. Unaweza kuwa umelala usiku na ukapata wazo zuri sana la kimojawapo kiasi kwamba unaona kama usipolifanyia kazi utakuwa unajikosea mwenyewe.

Tazito kubwa linalowakumba watu wenye vipaji vingi ni kukosa focus. Watu hawa huwa wana unfinished projects kwenye kila kipaji chake na kufanya asiendelee. Lakini kama mtu husika akiwa na focus na kuamua kupangilia vipaji vyake na kifanya kila kimoja kihusiane na kingine....maaan., anakuwa mtu flani mwenye mafanikio sana.

Mfano wa kesi ya nandy, akipangilia kwamba; bongo fleva ikawa ndo kipaumbele chake cha kwanza (kwa maana ya kuwekeza zaidi muda na raslimali nyingine), gospel akaifanya kama sehemu ya kupumzika na kuvuta pumzi wakati akiandaa project nyingine za bongo fleva na kuigiza akawa anafanya just for fun. Hii itamfanya ku keep in touch na mashabiki na kujiongezea mashabiki kwa sababu wapo ambao hawapendi ubongo fleva wake lakini watapenda u gosple wake. Na pia wapo wasiopenda ubongo fleva wake na u gospel wake lakini watapenda u bongo muvi wake.

Katika maisha, kitu kikubwa ambacho binadamu tunaishi kukitafuta ni furaha. Kama kuna kitu ambacho unaamini ukikifanya kitakupa furaha, we fanya tu bora usivunje sheria na kanuni za maadili za jamii husika bila kujali wengine watasema nini kwa kuwa hajui kina cha furaha yako. Kama ni makosa kila mtu hufanya.

Mimi sio shabiki wa muziki wa bongo fleva hivyo siyo shabiki wa nandy pia lakini nimejaribu kuongea katika mtazamo wa asili ya watu wenye bipaji zaidi ya kimoja.
Kwa hiyo leo aonekane jukwaani na kichupi akiimba bebi nipe ukuni nimeshalowa mwenzio halafu kesho anaimba Yesu nibeebee, Yesu ni mwamba na tegemezi langu au siyo??
 
Kila mtu ana kipawa, talanta na kipaji chake , lakini kati ya hivyo vitatu kimoja ndio hujitokeza zaidi na kwa baadhi viwili ndio huonekana zaidi

Talanta na kipawa hivi viko kiroho na kiimani zaidi huku kipaji kikiwa kiko kimwili na kidunia zaidi. Kwenye hii dunia kuna falme kuu mbili , ufalme wa Nuru na ufalme wa giza...ufalme wa nuru uko kiimani zaidi kwa maana ya Kimungu na ufalme wa giza uko kidunia zaidi kwa maana ya shetani ...hizi ni falme mbili zisizochangamana

Nandy binti mwenye kipaji cha uimbaji kupitia nyimbo zilizomtambulisha za kidunia alianza na kufanya vema sana kwenye hii kaliba, lakini sasa anapotea..anachanja mbuga kuelekea porini...Pengine kwakuwa jasiri muongoza njia hayupo tena..

Pressure ya kubaki kileleni, mashindano ya vipaji vipya na ugumu wa soko huku akiwa hana washauri wazuri vinaweza kuwa matokeo ya yale anayofanya sasa

Nandy kashindwa kushika moja, anachanganya mambo matatu kwa wakati mmoja
Bongo fleva
Bongo movie
Gospel
Hivi vitu vitatu huwa kamwe havipikiki chungu kimoja hata siku moja...kila kimoja kina chemistry yake, ladha yake na mashabiki yake... Lazima ujitambulishe na kukubalika kwenye moja ya makundi hayo

Kuchanganya bongo fleva na bongo movie ni kujiua kisanii kwakuwa iko wazi kabisa kuwa sisi wabongo na haya mambo ya sinema za kisasa tumefeli big time..HATUWEZI.. Sisi tuko vizuri kwenye mziki walau kwasasa

Kuchanganya bongo fleva na gospel ni sawa na kuzipambanisha falme mbili zenye kutofautiana kwenye kila kitu....leo uombe nogesha kesho uimbe Mungu ni mwema ...HUTAELEWEKA KAMWE... Utajimaliza mwenyewe

Figa tatu alizochagua Nandy hazirandani asilani..anatawanya na kupoteza nguvu zake bila kujua.....Na hapaswi kutafuta mchawi kwenye hili zaidi ya washauri wake

Shetani akizeeka huwa malaika.. Usitake kuwa malaika kabla hujazeeka. Yuko wapi Stara Thomas? Mzee Yusuph ndio huyo anatanga na njia sasa...Kuna wakongwe kama Cosmas Chidumule na Mzee Makassy hawa walipoamua kuipa dunia kisogo na kumgeukia Mungu hawakuyumba wala kurudi nyuma.

Kina TID wameamua kuingia bongo movie kwakuwa hawana nafasi tena kwenye soko la mziki...huko wanalazimisha tuu...ili walau siku zisonge

Kwa umri wake Nandy na kipaji kilichomtoa cha bongo fleva angejenga mhimili imara kwanza huko.... Wakati anahangaika na bongo movie kina Zuchu wanampiku kwenye chart za umaarufu...!!!

All in all kama kaamua moja la kumrudia Mola wake na kuimba Gospel katika umri huo , awe na nia thabiti ya kiroho asije akageuka na kurudi alikotoka...ataishia kuchanganyikiwa... Kumrudia Mungu ni vita sio bata... Amuige Hafsa Kazinja...

Kama anashaurika basi atulie na kuanza upya na ashike moja tuu kwakuwa mshika mawili moja humponyoka...sasa yeye kashika matatu kwa mpigo...!!!
Hata mimi nashangaa sana.
Mtu anaimba bongo fleva na gospel kwa wakati mmoja.
Michanganyo Mungu hapendi.
Achague kuwa moto au baridi,,hakuna ulinganifu Kati na nuru na giza.
Watu wanapenda kumchezea sana Mungu.
 
Kwa hiyo leo aonekane jukwaani na kichupi akiimba bebi nipe ukuni nimeshalowa mwenzio halafu kesho anaimba Yesu nibeebee, Yesu ni mwamba na tegemezi langu au siyo??
Masahihisho
Neno 'tegemezi' kwenye sentensi yako haliendani na ujumbe ambao nahisi unataka kuuwasilisha. Neno linalofaa hapa ni 'tegemeo'.

Tuje kwenye swali lako......

Jibu ni ndiyo.

Kama ingekuwa watu wasingeruhusiwa kushiriki kazi za kikanisa au kidini kisa tu wamevunja maagizo ya dini sidhani kama kanisani na misikitini kungekuwa na watu, hata hao mapadri, wachungaji na mashekbe nao pia wasingekuwepo. Dini zote zimekataza uzinzi, lakini si wote tunazini kila wakati na ikifika siku ya ibada tunaenda kanisani kusali.

Vitabu vya dini vimetaja kabisa kama uzinzi ni dhambi (japo mimi siamini kama kuna dhambi) lakini unazini na kisha unaenda kanisani. Lakini hakuna kitabu cha dini kikichotaja kuwa kucheza na kuchezs na kichupi jukwaani ni dhambi na bado unataka asiinbe nuimno za dini, kwa nini? Nandy hafanyi kosa kwa kuwa jamii yetu inakubali kazi anayoifanya kuwa haivunji kanuni za msinhi za kimaadili kama tu ilivyokubali uzinzi holela.

Huwa sipendi tabia ya kunyoshea watu vidole kwa kutumia jina la dini au Mungu kwa sababu kama kweli dhambi ipo na na moto upo basi hii dunia yote yenye watu 7b hakuna hata mmoja atakayeiona pepo, wote tutachomwa. Tuache kuwasimanga watu kwa kutumia jina la dini au Mungu, ni upuuzi.

Binafsi huwa sipendi kutumia kauli hii ila kunawakati inabidi tu, watu wengi wanaojifanya washika dini ni wanafiki wa kutupwa. Kwenye hivyo vitabu mnavyotumia kusimangia watu kuna simulizi kuwa yesu aliwaambia watu kuwa kama kuna ambaye ana uhakika kama hana dhambi awe wa kwanza kumpiga mawe mtu aliyekuwa yupo mbele yao. Hii inamaanisha, we have to stop being fvcking judgemental.
 
Nandy mwacheni aishi vile anataka yeye, hata akiwa na mafiga manne bado ni maamuzi yake na maisha yake. Amefika pale kwa juhudi zake mwenyewe, tatizo la bongo kila mtu ni mjuaji.
 
Ila bongo dah.. hakika tunaijua dini kuliko walioileta.. kiusanii, leo ndio nasikia msanii fulani akiimba aina fulani ya muziki hapaswi kuimba aina hii..

Ni mara mia moja hata huyu Nandy kaamua kumkumbuka Mungu, atakuwa na jambo la kusema ktk sanaa yangu nilimtukuza Mungu kwa kuitumia sauti yangu kufikisha neno lake kwa watu, hawa wasanii kaka ukiyajua maisha yao na wanayopitia, itoshe kusema hongera Nandy.

Mimi sioni tatizo, hili jambo lipo sana sana tu, mkuu Tasha Cobbs ana ngoma kafanya na Nicki Minaj na Nicki kachana tu fresh, na ngoma ni kali tu je Tasha Cobbs kazingua kuupeleka muziki wa dini ktk muziki wa kidunia (rejea mwonekano na maisha ya Nicki)?

Kwahiyo kwa maoni yangu binafsi sioni shida, rejea Luka 5:31 - 32

Yesu akawajibu, “Wenye afya hawamhitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”
Bible ukiisoma vipande vipande utapotosha wengi ni vema kusoma aya mzima ili kupata maana kamili...hebu angalia mistari iliyofuata inasema nini...zingatia 36-39

33 Baadhi ya watu wakamwuliza Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga na kusali mara kwa mara. Mbona wanafunzi wako wanakula na kunywa tu?”

34 Yesu akawajibu, “Je, inawezekana wageni walioalikwa har usini kufunga wakati wakiwa na Bwana Harusi? 35 Lakini wakati utafika ambapo Bwana Harusi ataondolewa. Wakati huo ndipo wataka pofunga.

36 Yesu akawapa mfano akawaambia: “Hakuna mtu anayechana nguo mpya ili apate kiraka cha kuweka kwenye nguo kuu kuu. Akifa nya hivyo ataharibu ile nguo mpya na ile kuu kuu itaonekana mbaya zaidi ikiwa na kiraka kipya. 37 Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vilivyochakaa; ukifanya hivyo, hivyo viriba vitapa suka na divai yote itamwagika. 38 Divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya. 39 Na pia hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai iliyoiva vizuri. Kwa maana husema, ‘Hii divai iliyoiva siku nyingi ni bora zaidi
 
Ila bongo dah.. hakika tunaijua dini kuliko walioileta.. kiusanii, leo ndio nasikia msanii fulani akiimba aina fulani ya muziki hapaswi kuimba aina hii..

Ni mara mia moja hata huyu Nandy kaamua kumkumbuka Mungu, atakuwa na jambo la kusema ktk sanaa yangu nilimtukuza Mungu kwa kuitumia sauti yangu kufikisha neno lake kwa watu, hawa wasanii kaka ukiyajua maisha yao na wanayopitia, itoshe kusema hongera Nandy.

Mimi sioni tatizo, hili jambo lipo sana sana tu, mkuu Tasha Cobbs ana ngoma kafanya na Nicki Minaj na Nicki kachana tu fresh, na ngoma ni kali tu je Tasha Cobbs kazingua kuupeleka muziki wa dini ktk muziki wa kidunia (rejea mwonekano na maisha ya Nicki)?

Kwahiyo kwa maoni yangu binafsi sioni shida, rejea Luka 5:31 - 32

Yesu akawajibu, “Wenye afya hawamhitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”
Kwahiyo huo mstari Yesu alikuja ili watu watubu na waendelee na uovu au siyo?

Yaani ndio unasikia leo kwamba haipaswi kuchanganya bongo fleva na Gospel??
Wewe huwa unasali kweli na Biblia huwa unaisoma vizuri??

Hembu usiishie kusema wabongo tunajidai kuijua dini!
To hoja zako kimaandiko ..

Kama hamna cha kucomment mkaage kimya.
Mshana yupo sahihi kabisa mujibu wa Biblia Takatifu ambayo hata mimi naijua.
 
Kupitia hii mada nimegundua wengi ni wakristo jina walio na uelewa wowote na maandiko lakini cha kushangaza zaidi hata wapagani bandia nao wamenizodoa bila hoja bali vioja
 
Wakristo jina+wanaocomments kwa chuki zao tu kwako,pia mashabiki mihemko wa huyo wa kujiita Nandy.
 
Eti ooh multi-talented sijui bla bla kiba!
Kwa Mungu hakuna mchanganyiko wa kachumbari namna hiyo..
Gospel na Bongo fleva havikai pamoja..ni sawa lilivyo giza na nuru,Nuru inapoingia giza hutoweka na giza linapoingia nuru hutoweka.
Mliwahi ona wapi giza na nuru vikakaa pamoja nyie binadamu?
Achezi ushabiki wa kijinga hadi kufikia mnataka kubadili ukweli wa Maandiko Sasa kwa hoja zenu za kijinga.
 
Back
Top Bottom