Nandy, Mafiga matatu yatakuponza

Ahsante nitapitia

BARIKIWA
 
TID si yupo bongo movie toka enzi za ile movie ya 'Girlfriend' wayback
 
Leo anaimba nyimbo video zake amevaa vichupi
Kesho yuko kwenye gospel kwakweli sio jambo jema kabisa huko ni kumjaribu Mungu
Achague Moja tu kama ni wa moto awe wamoto na kama ni wabaridi awe hivyo pia na sio vugu vugu
 
Ok, tujadili hizo hoja.
Hiyo hoja ya kwanza ya kusema kuwa filamu haifanyi vizuri hivyo yeye kuchanganya filamu na bongo fleva haina uhalisia kwa sababu hujaeleza ni kwa jinsi gani kutokufanya vizuri kwa filamu za Tanzania kutafanya yeye ashuke katika bongo fleva. Au watu watasema “fvck! Nandy ameanza kuigiza!? Mimi sipendi bongo movie kwa hiyo kama nandy ameanza kuigiza basi sifuatilii muziki wake” (kitu ambacho hakina uhalisia). Au atawekeza sana kwenye filamu na atapotesa focus kwenye muziki? Hii nayo haonekani kufanya kazi kwa sababu sidhani kama nandy yupo serious sana filamu kiasi a’risk bongo fleva yake.

Tuje kwenye hiyo hoja ya pili kuwa bongo fleva na gospel ni falme mbili tofauti (giza na mwanga) hivyo kuchanganya ni kupambanisha falme mbili tofauti.

Kwanza kabisa, mimi siamini katika hayo mambo ya giza na mwanga, shetani sijui dhambi. Siamini katika hizo mambo so pia siamini kama hiyo vita unayoiongelea inaweza kutokea. Lakini pia dhana ya kuwa kuna madhara ya kuchanganya bongo fleva na gospel haifanyi kazi kwenye uhalisia kwa sababu kila muziki una maudhui yake na una sehemu yake. hivi kwa mfano mchungaji na mkewe wakiwa faragha, mke wa mchungaji akaamua kumuimbia mme wake wimbo wa nandy (let say ‘ninogeshe’) huku akicheza mbele yake, atakuwa anapambanisha falme mbili tofauti kwa kuwa yeye ni mke wa mchungaji na anaimba wimbo wa bongo fleva? Au nandy akiamua kutenga muda wake kuimba wimbo wa kumsifu Mungu atakuwa anapambanisha falme mbili tofauti kwa kuwa yeye anaimba bongo fleva?

Kuamini kuwa muziki wa bongo fleva ni muziki wa giza (au wa kishetani) na mziki wa gospel ni muziki wa mwanga (Mungu) ni dhana ambayo haipaswi kuendekezwa kwa sababu haina uhalisia. Watu tunapitia hali tofauti na tunahitaji mahitaji tofauti kukidhi hali hizo tofauti. Kuna wakati mtu atahitaji kusikiliza nyimbo za mapenzi na kuna wakati mtu anahitaji kusikiliza gospel. Sasa kama mtu mmoja anaweza kusikiliza bongo fleva na gopel kwa nyakati tofauti kuna ubaya gani msanii mmoja akafanya gospel na bongo fleva kwa nyakati tofauti? Na pia umeonyesha kuwa ili nandy afanikiwe ki bongo fleva anatakiwa aachane na gospel na kulingana na mtizamo wako (wa giza na mwanga) unamshauri amwache Mungu ili afanikiwe katika shetani. Wewe ni nani unayehimiza watu wafanikiwe katika shetani? Hakuna uhalisia.

Simaanishi kuwa nandy hawezi kushuka kimuziku (bongo leva) kwa kuchanganya hivyo vitatu, lakini hoja ulizoweka sidhani kama zinafanya kazi, hazina uhalisia.

Njia pekee ambayo itamshusha nandy kwa kuchanganya vitu hivi vitatu ni kama atakosa focus, kwamba leo kaacha bongo fleva kahamia kwenye gospel, muda kidogo baadaye anaacha gospel na kuhamia kwenye filamu, baada ya muda tena anaanza kufanya vyote vitatu nk nk.
 
Stephano nashindwa kuendeleza mjadala nawe kwakuwa kuna mahali tuna maono tofauti
1. Si mfuatiliaji wa bongo muvi (hata mimi pia) lakini hujahangaika japo uone episode moja ama kusaka habari za mhusika na kaliba yake hiyo ya sinema...kwahiyo kwako hapa ni ngumu kujadili kile nilichoandika

2. Huamini katika mambo ya kiimani na kiroho , falme mbili za giza na mwanga, kitu ambacho kiko kwenye mada yangu..hapa ni ngumu pia kujenga hoja jadilika kwakuwa tayari nilichoandika hakina mashiko kwako

Ishu ya mke wa mchungaji kumwimbia mumewe chumbani sio hoja kwakuwa hayo ni mambo binafsi faraghani na hapa hatujadili faragha ya Nandy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikua natetea sana bangi ila kwa sasa naomba wazuie tu.
Hapo namaanisha hivi kweli uimbe bongo fleva umevaa vyupi, harafu upate nguvu za kuimba gospel umevaa kanzu.
 
Subiri matokeo ndo yatakuaminisha .....!!!
 
Nilikua natetea sana bangi ila kwa sasa naomba wazuie tu.
Hapo namaanisha hivi kweli uimbe bongo fleva umevaa vyupi, harafu upate nguvu za kuimba gospel umevaa kanzu.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]kuna watu wameshamfanya Mungu shemeji na babu yao kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyovyote vile iwavyo, linapokuja swala la vipaji vya sanaa, sidhani kama ni jambo zuri kumwambia mtu aache kufanya kitu fulani kwa sababu huwezi jua hicho kitu kina mizizi kiasi gani katika furaha yake. Ni vema kushauri namna bora ya kuvifanya katika namba ambayo haitaadhiri sanaa yake kuu ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo inayoleta chakula mezani.

Yeye mwenyewe akiamua kuachana na kitu fulani ni sawa kwa kuwa atakuwa amepima nakuona faida na hasara zake.
 
Ok thanks kwa mchango wako nimekupata vema[emoji1545][emoji1545][emoji1545]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofauti na zile cover songs mbili za gospel, kuna nyingine katoa?

Huyu hayupo kwenye gospel. Ni mwana bongo fleva na mkata mauno tu.
 
Ebwanae umeongea vzr sana sina neno la kutia,Nandy nafikiri katokea kwny familia za zilizoshika dini sasa huenda kuna msukumo kutoka katika familia unaomkosoa kufanya nyimbo za kidunia,so kuacha ameshindwa na kuamua kushika vyote,
Hata hivyo Mungu amekataza michanganyo ya hivyo,Nusu kwenye dunia nusu unamtumikia
Kuna mistari kwny biblia inasema bora kuwa wa baridi au moto kuliko kuchagua vuguvugu
Nandy anachofanya nikuamua kuwa vuguvugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…