Nandy, Mafiga matatu yatakuponza


Nadhan suala la kumuimbia na kumsifu Mungu halina mpaka kwa sababu yeye ndo muweza wa kila kitu , wengine tunaroga usiku kucha ila Mungu pia tunamuomba kwa kuwa ndie muweza wa yote

Nadhan kwa anayopitia sasa hiv kaamua kujifariji kwa kumtukuza Mungu ukizingatia nandy katokea familia ya kidini na zaman alikua anaimba kwaya kanisani, hizi nyimbo za dunia yupo kibiashara tu
 

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila bongo dah.. hakika tunaijua dini kuliko walioileta.. kiusanii, leo ndio nasikia msanii fulani akiimba aina fulani ya muziki hapaswi kuimba aina hii..

Ni mara mia moja hata huyu Nandy kaamua kumkumbuka Mungu, atakuwa na jambo la kusema ktk sanaa yangu nilimtukuza Mungu kwa kuitumia sauti yangu kufikisha neno lake kwa watu, hawa wasanii kaka ukiyajua maisha yao na wanayopitia, itoshe kusema hongera Nandy.

Mimi sioni tatizo, hili jambo lipo sana sana tu, mkuu Tasha Cobbs ana ngoma kafanya na Nicki Minaj na Nicki kachana tu fresh, na ngoma ni kali tu je Tasha Cobbs kazingua kuupeleka muziki wa dini ktk muziki wa kidunia (rejea mwonekano na maisha ya Nicki)?

Kwahiyo kwa maoni yangu binafsi sioni shida, rejea Luka 5:31 - 32

Yesu akawajibu, “Wenye afya hawamhitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”
 
Anatafuta huruma kwa waTanzania
 
Una kipaji cha kuandika[emoji23], Hapo nikisamaraizi natoka na aya moja.
 
Nandy fanya yote ndani ya uwezo wako,kuna time itafika YOU CAN'T DO SHIT,utabaki i could have done this or that..hapo umezeeka, fanya YOTE sema kuwa ORGANISED ,and consistent...
 
Kwa hiyo leo aonekane jukwaani na kichupi akiimba bebi nipe ukuni nimeshalowa mwenzio halafu kesho anaimba Yesu nibeebee, Yesu ni mwamba na tegemezi langu au siyo??
 
Hata mimi nashangaa sana.
Mtu anaimba bongo fleva na gospel kwa wakati mmoja.
Michanganyo Mungu hapendi.
Achague kuwa moto au baridi,,hakuna ulinganifu Kati na nuru na giza.
Watu wanapenda kumchezea sana Mungu.
 
Kwa hiyo leo aonekane jukwaani na kichupi akiimba bebi nipe ukuni nimeshalowa mwenzio halafu kesho anaimba Yesu nibeebee, Yesu ni mwamba na tegemezi langu au siyo??
Masahihisho
Neno 'tegemezi' kwenye sentensi yako haliendani na ujumbe ambao nahisi unataka kuuwasilisha. Neno linalofaa hapa ni 'tegemeo'.

Tuje kwenye swali lako......

Jibu ni ndiyo.

Kama ingekuwa watu wasingeruhusiwa kushiriki kazi za kikanisa au kidini kisa tu wamevunja maagizo ya dini sidhani kama kanisani na misikitini kungekuwa na watu, hata hao mapadri, wachungaji na mashekbe nao pia wasingekuwepo. Dini zote zimekataza uzinzi, lakini si wote tunazini kila wakati na ikifika siku ya ibada tunaenda kanisani kusali.

Vitabu vya dini vimetaja kabisa kama uzinzi ni dhambi (japo mimi siamini kama kuna dhambi) lakini unazini na kisha unaenda kanisani. Lakini hakuna kitabu cha dini kikichotaja kuwa kucheza na kuchezs na kichupi jukwaani ni dhambi na bado unataka asiinbe nuimno za dini, kwa nini? Nandy hafanyi kosa kwa kuwa jamii yetu inakubali kazi anayoifanya kuwa haivunji kanuni za msinhi za kimaadili kama tu ilivyokubali uzinzi holela.

Huwa sipendi tabia ya kunyoshea watu vidole kwa kutumia jina la dini au Mungu kwa sababu kama kweli dhambi ipo na na moto upo basi hii dunia yote yenye watu 7b hakuna hata mmoja atakayeiona pepo, wote tutachomwa. Tuache kuwasimanga watu kwa kutumia jina la dini au Mungu, ni upuuzi.

Binafsi huwa sipendi kutumia kauli hii ila kunawakati inabidi tu, watu wengi wanaojifanya washika dini ni wanafiki wa kutupwa. Kwenye hivyo vitabu mnavyotumia kusimangia watu kuna simulizi kuwa yesu aliwaambia watu kuwa kama kuna ambaye ana uhakika kama hana dhambi awe wa kwanza kumpiga mawe mtu aliyekuwa yupo mbele yao. Hii inamaanisha, we have to stop being fvcking judgemental.
 
Nandy mwacheni aishi vile anataka yeye, hata akiwa na mafiga manne bado ni maamuzi yake na maisha yake. Amefika pale kwa juhudi zake mwenyewe, tatizo la bongo kila mtu ni mjuaji.
 
Bible ukiisoma vipande vipande utapotosha wengi ni vema kusoma aya mzima ili kupata maana kamili...hebu angalia mistari iliyofuata inasema nini...zingatia 36-39

33 Baadhi ya watu wakamwuliza Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga na kusali mara kwa mara. Mbona wanafunzi wako wanakula na kunywa tu?”

34 Yesu akawajibu, “Je, inawezekana wageni walioalikwa har usini kufunga wakati wakiwa na Bwana Harusi? 35 Lakini wakati utafika ambapo Bwana Harusi ataondolewa. Wakati huo ndipo wataka pofunga.

36 Yesu akawapa mfano akawaambia: “Hakuna mtu anayechana nguo mpya ili apate kiraka cha kuweka kwenye nguo kuu kuu. Akifa nya hivyo ataharibu ile nguo mpya na ile kuu kuu itaonekana mbaya zaidi ikiwa na kiraka kipya. 37 Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vilivyochakaa; ukifanya hivyo, hivyo viriba vitapa suka na divai yote itamwagika. 38 Divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya. 39 Na pia hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai iliyoiva vizuri. Kwa maana husema, ‘Hii divai iliyoiva siku nyingi ni bora zaidi
 
Kwahiyo huo mstari Yesu alikuja ili watu watubu na waendelee na uovu au siyo?

Yaani ndio unasikia leo kwamba haipaswi kuchanganya bongo fleva na Gospel??
Wewe huwa unasali kweli na Biblia huwa unaisoma vizuri??

Hembu usiishie kusema wabongo tunajidai kuijua dini!
To hoja zako kimaandiko ..

Kama hamna cha kucomment mkaage kimya.
Mshana yupo sahihi kabisa mujibu wa Biblia Takatifu ambayo hata mimi naijua.
 
Kupitia hii mada nimegundua wengi ni wakristo jina walio na uelewa wowote na maandiko lakini cha kushangaza zaidi hata wapagani bandia nao wamenizodoa bila hoja bali vioja
 
Kupitia hii mada nimegundua wengi ni wakristo jina walio na uelewa wowote na maandiko lakini cha kushangaza zaidi hata wapagani bandia nao wamenizodoa bila hoja bali vioja
Wakristo jina+wanaocomments kwa chuki zao tu kwako,pia mashabiki mihemko wa huyo wa kujiita Nandy.
 
Eti ooh multi-talented sijui bla bla kiba!
Kwa Mungu hakuna mchanganyiko wa kachumbari namna hiyo..
Gospel na Bongo fleva havikai pamoja..ni sawa lilivyo giza na nuru,Nuru inapoingia giza hutoweka na giza linapoingia nuru hutoweka.
Mliwahi ona wapi giza na nuru vikakaa pamoja nyie binadamu?
Achezi ushabiki wa kijinga hadi kufikia mnataka kubadili ukweli wa Maandiko Sasa kwa hoja zenu za kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…