NANE NANE ITIMIZE MALENGO YAKE, ISIISHIE KUWA GULIO — USHAURI KWA WIZARA YA KILIMO

NANE NANE ITIMIZE MALENGO YAKE, ISIISHIE KUWA GULIO — USHAURI KWA WIZARA YA KILIMO

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Wakuu,

Nadhani umefika wakati Wizara ya Kilimo iangalie upya namna tunavyoendesha Maonesho ya Nane Nane nchini ili yawe na matokeo makubwa zaidi kwa mkulima na sekta ya kilimo kwa ujumla.

Kwanza, Nane Nane isiishie kuwa gulio kubwa la kila aina ya bidhaa, vyakula na burudani.

Hayo yana nafasi yake, lakini yasije yakafunika kusudi kuu la maonesho haya ambalo ni kilimo, mkulima, teknolojia, masoko na kuongeza tija.

Pili, nafikiri tunapaswa kujiuliza:

Je, uzito wa Nane Nane haupaswi kwenda zaidi kwenye maeneo ambayo ndiyo kitovu cha uzalishaji wa chakula nchini?

Kwa mfano, ningetarajia kuona uwekezaji na uzito mkubwa zaidi wa maonesho ukiwekwa Mbeya kwa Nyanda za Juu Kusini, Morogoro kwa maeneo ya Kati/Mashariki, Arusha kwa Kanda ya Kaskazini na Kagera kwa ukanda wa Ziwa.

Hapa ndipo Nane Nane inaweza kugeuzwa kutoka kuwa event ya siku chache na kuwa agricultural innovation hub inayofanya kazi mwaka mzima.

Maeneo haya yawe na mashamba darasa ya kudumu, vituo vya teknolojia za kilimo, mifumo ya kisasa ya umwagiliaji, mechanisation, mbegu bora, teknolojia za uhifadhi wa mazao, kuongeza thamani, taarifa za masoko na hata maeneo ya kuwaunganisha moja kwa moja wakulima na wanunuzi wakubwa.

Mkulima anayefika Nane Nane asiishie kuzunguka mabanda na kupewa brochure.

Akiingia akiwa na tatizo la mbegu, atoke na suluhisho.

Akiwa na tatizo la soko, akutanishwe na wanunuzi.

Akiwa anataka umwagiliaji, aoneshwe teknolojia inayolingana na uwezo wake.

Akiwa anataka trekta au mashine ndogo za kilimo, akute suppliers na financing arrangements hapo hapo.

Akiwa anataka kuongeza thamani ya mazao yake, aoneshwe teknolojia na namna ya kufikia masoko.

Na muhimu zaidi, mafanikio ya Nane Nane yapimwe kwa matokeo, sio ukubwa wa gulio.

Baada ya maonesho Wizara ituambie:

wakulima wangapi wameunganishwa na masoko?

Wangapi wamepata teknolojia mpya?

Wangapi wameunganishwa na taasisi za fedha?

Ni teknolojia zipi zimeanza kutumika mashambani kutokana na Nane Nane?

Na uzalishaji umeongezeka kwa kiwango gani?

Hapo ndipo Nane Nane itakuwa na maana kubwa zaidi.

Kanda nyingine ziendelee kuwa na maonesho kulingana na shughuli na mazao yanayotawala katika maeneo yao, lakini uzito mkubwa wa uwekezaji katika Nane Nane ufuate ramani halisi ya uzalishaji wa kilimo nchini.

Haiingii sana akilini kuwa na maonesho makubwa ya kilimo lakini mkulima anayezalisha mahindi, mpunga, viazi, ngano, maharage, ndizi na mazao mengine kwa kiwango kikubwa huko aliko, teknolojia na wataalamu wanaomsaidia bado wanapatikana zaidi kwenye mabanda kwa siku nane tu za maonesho au wanapatikana mkoa wa mbali sana!

Nane Nane isiwe mahali pa kwenda kuona kilimo kula nyama choma na bia.

Iwe mahali pa kwenda kubadilisha kilimo.

Na ikiwezekana, maeneo makubwa ya Nane Nane katika kanda muhimu za uzalishaji yawe vituo hai vya kilimo, teknolojia na masoko vinavyofanya kazi siku 365 kwa mwaka, badala ya kusubiri Agosti kila mwaka.

Hapo tutakuwa tumeifanya Nane Nane iwe sehemu ya mkakati wa kuongeza uzalishaji na usalama wa chakula nchini, badala ya kuwa tamasha kubwa linalokuja na kuondoka kila mwaka.

Wizara ya Kilimo, hili nalo linafaa kufikiriwa.

Wadau mnalionaje?
 
Mambo mengi uliyotaja yanafanyika. Nimelala saa nane za usiku sababu ya kusoma na kufuatilia teknolojia nilizoziona kwenye maonyesho ya Nane Nane.
Nimetoka na samples, picha, contacts, brochures, vitabu.

Pia kuna vipando vilikuwepo ambavyo kukomaa kwake ni miezi sita, kwahiyo sio kweli kwamba maonyesho yamefanyika siku nane. Nane Nane inaanza maandalizi miezi kadhaa, haitokuwa na maana tena kuanzisha festivals alafu zinafanyika siku zote za mwaka. Hayo sio maonyesho sasa bali daily life.

Kitu kingine ambacho labda hujui ni kwamba kuna taasisi za serikali na mashirika binafsi na NGOs ambazo hayo yalioonyeshwa kwenye Nane Nane ndio maisha yao ya kila siku. Ni uvivu wa wakulima au kutojua au kutokuwa na taarifa kunakofanya wawe mbali na hizo huduma.

Hakuna taasisi ilianzishwa kwenye maonyesho ya Nane Nane. TARI, Bayer, vyuo vikuu, Yara, Interchick, SIDO, halmashauri, bodi za mazao, etc zote zipo zinafanya kazi kila siku. Watu waache uvivu watumie fursa hizo.

Nimejifunza nami kuacha uvivu kufuata hizo taasisi. Kwenye Nane Nane iwe ni siku ya kuonyesha matokeo na kujifunza kwa wengine au kuona teknolojia mpya ambayo lazima iwepo na huwezi jua kila kitu. Sio unalala uko unasubiri hata mbegu basic uzionee Nane Nane.

Pia, Nane Nane kwa hizo siku nane haiwezekani iwe kuonyeshana kilimo tu. Lazima kuwepo na biashara za kusaidia kilimo mfano mitandao inauza WiFi routers, banks na biashara unrelated. Si jambo baya naona. Wanaotaka kilimo wanaenda direct kwa wanachotaka. Ambaye si mkulima atakuja kuona vitu vingine, then awe inspired kufanya kilimo by chance.
 
Uzi ufungwe
 
Hiyo mifumo ya siku 365 mtailipia ninyi? Wizara yenyewe bajeti ya kuendesha maonesho kwa siku 8 tu inasua-sua. Hiyo working capital ya kuendesha vituo mwaka mzima nchi nzima itoke wapi?
 
Maonyesho ya Tanzania yameanza waganga wa kienyeji wakiuza dawa feki walizofunga vizuri kwenye vichupa usilogwe uwaangalie tuu watalukimbilia na vipeperushi vyao. Wanaibia Sana watanzania kwa sababu Wana promote hadharani kuwa wanatibu yake magonjwa makubwa yaliyoshindikana Hospitalini. Hawana tofauti na akina mwamposo na matapeli wengine wali hasi kanisa kwa kuanzishwa Imani zao lakini wakijiitanwakristu. Wanadanganya watu kutoa ushuhuda kuwa wamepona wakati wanapo fariki Wala hawapo ndungu ndio wanahangaika. Wengi wamedanganywa kuacha ARV zao eti wamepona mwisho wa siku Kinga zinashika gafla wanakufa
 
Back
Top Bottom