Nani adui wa vijana katika Kujiajiri. Ni Uthubutu, Serikali, au Malezi na Mazingira?

Nani adui wa vijana katika Kujiajiri. Ni Uthubutu, Serikali, au Malezi na Mazingira?

Zillion

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2017
Posts
1,378
Reaction score
1,866
Wakuu,
Poleni na majukumu ya kila siku.

Katika ulimwengu wa sasa ambapo watu wenye taaluma mbalimbali wamejikuta mitaani bila kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato, ningependa kupata maoni yenu na pengine suluhu ya vijana kujiajiri na kuajiri wenzao

Nini hasa kikwazo kinachowafanya vijana wengi washindwe kujiajiri
Ni Sera, malezi, Aibu, Mazingira au Uthubutu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo hayo naweza nkasema yanategemeana kwa namna fulani..

Mfano, malezi na mazingira yanaweza kumpelekea kijana akakosa uthubutu wa kujiajiri... Yaan unakuta mzazi akawa anafanya shughuli zake mbalimbali za kumuingizia kipato (amejiajiri) lakini hamshirikishi mwanae katika biashara hizo ili kumfanya ajijenge kiakili kuhusu namna biashara hizo zinavyokwenda... Hvyo mtoto hadi anakua mtu mzima hafahamu chochote kuhusu kuendesha biashara mbalimbali..!
 
Mkuu
Mimi nimejiajiri tangu 2014
Ni mjasiriamali mdogo
Nilikataa kuajiriwa na Polisi
Sijawahi kujutia maamuzi yangu

Bado sijafikia malengo kwa 100% lakini naona milango ikifunguka siku hadi siku

Nimejifunza uthubutu, kupambana, uvumilivu na kusimamia ninachokiamini bila kuyumba ( Consistence) na vimenisaidia Sana.

Mwanzo ndugu zangu hawakunielewa, walitaka niajiriwe lakini niliweka msimamo sihitaji kuajiriwa lakini sasa wameelewa nilichokuwa namaanisha.



Tuanze na wewe kwanza, elezea uliko

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye kujiajiri ni kutokufikiria zaidi na kufanya uchunguzi wa nini ambacho anaweza kukipeleka sokoni kikakubalika kirahisi.

Ila Mkuu tuache siasa nyingi pia

UVIVU TUU! na TAMAA za kijinga..

tukirudi kwenye kuajiriwa utakubaliana na mimi kuwa kila eneo linahitaji watu wakugrow value ya shirika/kampuni sasa miongoni mwa vijana wengi wamejawa na uvivu + tamaa za haraka haraka anataka akipata hela tayari break yake ya kwanza kwenye gari kali na mademu! + MALEZI MABOVU.

nikimaanisha “ incorporates the practical knowledge of how to perform tasks” + “personal and intimate to the user, often learned without instruction or guidance”


Na siku zote ukitaka kupima Inteligence test ya kijana mpe kazi bila pesa,hata ya kujitolea utaona vituko.


So as vijana we must figure out what an audience wanted and give it to them!

Kila la kheri
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kinaitwa root cause failure analysis (RCA)

bila ufaham mzuri kila mtu atazuka na visababu vyake kimtazamo ambavyo sio root cause.

lakini jibu sahihi lisilenge mtu mmoja ametokaje Bali asilimia mfano 50% au 70%

tunapotoa majibu tunatakiwa kutazama Wastani wa wahusika sio mafanikio ya mtu mmoja watatu au wanne sababu hawa hawawakilishi sample spaces or representative sample

vijana kwanini asilimia kubwa hawawezi kutoka/kufanikiwa/kupiga hatua/kujiajiri/kujitegemea/kujijenga ...... tatizo ni nini?
 
Haiwezekani tatizo la vijana maelufu kushindwa kuwa ni :-

1. Aibu

2. Uzembe

3. Elimu

4. Malezi

5. Mazingira

6. Uthubutu

7. Uoga

Nk
Haiwezekani mamilioni wanateseka lazima kunatatizo la msingi ambalo ni common yaani Root cause
 
1. Aibu...... nikweli nchi nzima vijana wanakwama sababu wanaaibu? Sio kweli

2. Uzembe .... nikweli vijana mikoa yote wazembe? Sio kweli

3. Elimu.... nikweli vijana wakitanzania asilimia kubwa Elimu haiwasaidii .... may be but not certainly

4. Malezi.... nikweli malezi yanawakwamisha maelfu ya vijana! Kwamba wazazi wanamalezi yakufanana nchi nzima? Kigoma, tanga, mtwara .... singida......shinyanga? Sio kweli

5. Mazingira... je mazingira yanaweza kuwa sababu? May be but not certainly kwa taifa zima

6. Uthubutu.... nikweli vijana wengi hawana uthubutu? Kivipi kama taifa tunaongelea asilimia kubwa ya vijana zaidi ya 50%

7. Uoga... kwamba zaidi ya 50% ya vijana wetu waoga? Sio kweli
 
Back
Top Bottom