Wakuu,
Poleni na majukumu ya kila siku.
Katika ulimwengu wa sasa ambapo watu wenye taaluma mbalimbali wamejikuta mitaani bila kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato, ningependa kupata maoni yenu na pengine suluhu ya vijana kujiajiri na kuajiri wenzao
Nini hasa kikwazo kinachowafanya vijana wengi washindwe kujiajiri
Ni Sera, malezi, Aibu, Mazingira au Uthubutu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwangu mimi tatizo kubwa ni serikali
Serikali haijaweza kujipanga kuwajenga vijana wajitegemee. (Mtoto umleavo ndivo akuwavo)
1. Serikali haina sera bora kuwajenga vijana
2. Serikali haijawa namikakati bora na kabambe kuwajengea vijana uwezo kujiajili
A. Elimu yetu mtaala wa hovyo.... nadhalia kwa wingi vitendo yaani practicals zero
B. Mazingira
- mitaji sahihi sio hela nyanya kuhadaa vijana Visenti vya kulimia robo heka bila mbolea wala madawa imeisha
- Karakana wezeshi zenye vifaa vyote ilikuboresha ujuzi na maarifa ya vijana
- uhamasishaji sahihi, sio mapambio yakisiasa na ulaghai mitaani katika kulenga kupigiwa kura
- masoko ya bidhaa, serikali inapaswa kuona mbali na kupanga mipango ya makusudi kitaalamu sio kisiasa. Ili vijana iliowaanda kimkakati katika sera bora wajiendeleze kwa miradi yao.
Nk nk nk
Dhana ya vijana wachache kutoka yaani mmoja mmoja kufanikiwa haiwezi kuwa utetezi ama sababu kuwabeza au kuwaona duni waliowengi ambao hawana lakufanya
Ukichimba kwa kina hao mmoja mmoja waliofanikiwa utakuta lazima pembeni kuna aliyesaidia kwa namna moja ama nyingine wakajijenga. (Huwa hawasemi ukweli halisi kwa 100% walivofanikiwa)
Baba
Ndugu
Rafiki
Au mfadhili
Bila ya
1. Mtaji sahihi
2. Mazingira bora
3. Elimu .....sio lazima ya darasani... (uelewa wa jambo alifanyalo kwa undani iwe kilimo, biashara nk.)
Hapa ndipo tunakwama.
unaweza kuwa na vyote bila mtaji, bila mazingira bora (sera na mipango ya serikali sahihi) hatutatoka milele
muwe na mjadala mwema [emoji119][emoji119][emoji119]
1. Aibu...... nikweli nchi nzima vijana wanakwama sababu wanaaibu? Sio kweli
2. Uzembe .... nikweli vijana mikoa yote wazembe? Sio kweli
3. Elimu.... nikweli vijana wakitanzania asilimia kubwa Elimu haiwasaidii .... may be but not certainly
4. Malezi.... nikweli malezi yanawakwamisha maelfu ya vijana! Kwamba wazazi wanamalezi yakufanana nchi nzima? Kigoma, tanga, mtwara .... singida......shinyanga? Sio kweli
5. Mazingira... je mazingira yanaweza kuwa sababu? May be but not certainly kwa taifa zima
6. Uthubutu.... nikweli vijana wengi hawana uthubutu? Kivipi kama taifa tunaongelea asilimia kubwa ya vijana zaidi ya 50%
7. Uoga... kwamba zaidi ya 50% ya vijana wetu waoga? Sio kweli
Unaweza kulaumu sana lkn kama taifa uchumi wetu unatoa ukomo wa jumla kwa mambo mengi.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kipi cha kweli sasa, ama nini mtazamo wako?1. Aibu...... nikweli nchi nzima vijana wanakwama sababu wanaaibu? Sio kweli
2. Uzembe .... nikweli vijana mikoa yote wazembe? Sio kweli
3. Elimu.... nikweli vijana wakitanzania asilimia kubwa Elimu haiwasaidii .... may be but not certainly
4. Malezi.... nikweli malezi yanawakwamisha maelfu ya vijana! Kwamba wazazi wanamalezi yakufanana nchi nzima? Kigoma, tanga, mtwara .... singida......shinyanga? Sio kweli
5. Mazingira... je mazingira yanaweza kuwa sababu? May be but not certainly kwa taifa zima
6. Uthubutu.... nikweli vijana wengi hawana uthubutu? Kivipi kama taifa tunaongelea asilimia kubwa ya vijana zaidi ya 50%
7. Uoga... kwamba zaidi ya 50% ya vijana wetu waoga? Sio kweli
Kuna kitu kinaitwa root cause failure analysis (RCA)
bila ufaham mzuri kila mtu atazuka na visababu vyake kimtazamo ambavyo sio root cause.
lakini jibu sahihi lisilenge mtu mmoja ametokaje Bali asilimia mfano 50% au 70%
tunapotoa majibu tunatakiwa kutazama Wastani wa wahusika sio mafanikio ya mtu mmoja watatu au wanne sababu hawa hawawakilishi sample spaces or representative sample
vijana kwanini asilimia kubwa hawawezi kutoka/kufanikiwa/kupiga hatua/kujiajiri/kujitegemea/kujijenga ...... tatizo ni nini?
Sio kweliMTAJI
Mengine ngonjera tu.
Tatizo sio serikali, mtaji , malezi wala mazingira, Tatizo ni kukosa uhakika wa kuuza. Watu wengi wanapenda kufanya biashara Ila hawana uhakika wa kuuza.
Sent using Jamii Forums mobile app
Root cause ni lack of creativityHaiwezekani tatizo la vijana maelufu kushindwa kuwa ni :-
1. Aibu
2. Uzembe
3. Elimu
4. Malezi
5. Mazingira
6. Uthubutu
7. Uoga
Nk
Haiwezekani mamilioni wanateseka lazima kunatatizo la msingi ambalo ni common yaani Root cause
Tatizo...Wakuu,
Poleni na majukumu ya kila siku.
Katika ulimwengu wa sasa ambapo watu wenye taaluma mbalimbali wamejikuta mitaani bila kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato, ningependa kupata maoni yenu na pengine suluhu ya vijana kujiajiri na kuajiri wenzao
Nini hasa kikwazo kinachowafanya vijana wengi washindwe kujiajiri
Ni Sera, malezi, Aibu, Mazingira au Uthubutu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakuu,
Poleni na majukumu ya kila siku.
Katika ulimwengu wa sasa ambapo watu wenye taaluma mbalimbali wamejikuta mitaani bila kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato, ningependa kupata maoni yenu na pengine suluhu ya vijana kujiajiri na kuajiri wenzao
Nini hasa kikwazo kinachowafanya vijana wengi washindwe kujiajiri
Ni Sera, malezi, Aibu, Mazingira au Uthubutu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa. Ila uhakika wa kuuza unakuja pale mtu anapoanzisha biashara bila kujua kama watu wanauhitaji wa bidhaa zake au huduma yake. Ila kama mtu akiuza bidhaa au huduma ambazo watu wako tayari kununua hawezi kosa wateja.Tatizo sio serikali, mtaji , malezi wala mazingira, Tatizo ni kukosa uhakika wa kuuza. Watu wengi wanapenda kufanya biashara Ila hawana uhakika wa kuuza.
Sent using Jamii Forums mobile app
SABABU KUBWA NI MINDSET
Asilimia kubwa ya vijana mfano hapa Tanzania tunaishi chini ya utamaduni na mfumo wa maisha unaofanana kwa wengi. Kutokana na hali hii, wazazi/walezi wanaandaa vijana kusoma ili wapate kazi nzuri kwa kuajiriwa. Hvyo kijana anaanza kusoma akilenga kuajiriwa sehemu fulani na sio kujiajiri sehemu fulani. Kutokana na % kubwa kuwa na Mindset inayofanana, ndiyo maana tatizo la ukosefu wa ajira linazidi kuwa kubwa kwa vijana wengi.
SABABU BAADHI NDOGO NDOGO ZINAZOUNDA SABABU KUBWA TAJWA HAPO JUU NI-:
1. Kijana Kutotambua wapi aanzie ili kujiajili.
2. Vijana wengi wanahisi hawana uwezo wa kufanya kazi fulani wakisema kazi hzo ni za watu fulani au ni za mataifa fulani na mwisho wa siku hukaa bila kuwa na kitu cha kufanya maana kila wanachofikiri wanaona kwao hakiwezekani.
3. Uzembe wa kuchukua hatua, yaani kijana anasema kesho nitafanya na kesho huzaa kesho bila kuanza anachokifikiri.
4. Kukosa plan B na hvyo Kupoteza muda mwingi kulaumu Serikali, ndugu na marafiki badala ya kuangalia nini cha kufanya.
5. Vijana wengi wanahisi kujiajiri ni kuuza bidhaa tu na kama hana fedha za kuanzisha biashara fulani basi anakaa wakati anaweza kuanzisha biashara inayouza huduma na akaingiza fedha nyingi bila hata mtaji wa fedha.
6. Baadhi walijaribu kujiajiri lakini walichagua mawazo ya biashara yasiyosahihi (WRONG BUSINESS MODELS) ambapo biashara zao zilikufa mapema na wakakata tamaa.
NINI KIFANYIKE KAMA SULUHU
Suluhu kubwa ya tatizo la ajira ni jamii kwa ujumla kubadili MINDSET zao ili mtu awe na mawazo ya kujiajiri tokea akiwa mdogo.
MAMBO MENGINE YA KUZINGATIA KAMA SULUHU NI KAMA
1. Jambo la kwanza ni kuepuka vikwazo kama hivyo nilivyovitaja hapo juu.
2. Vijana watambue mtaji mkubwa ni akili na uwezo waliopewa na mwenyezi Mungu wala sio pesa.
3. Vijana wasiwe wabinafsi. Mfano, mtu anawazo zuri la biashara na hana pesa na anashindwa kumshirikisha mwenzake mwenye pesa ili waanzishe biashara na hivyo anakaa na wazo lake hadi linakufa bila mafanikio.
4. Vijana wasikimbilie kuuliza biashara gani inalipa wataangukia shimoni maana mahesabu ya kwenye karatasi ni tofauti na mahesabau halisia. Hivyo vijana wajikite katika kutatua matatizo ya watu hapo ndipo kuna biashara inayolipa maana mtu akitatuliwa tatizo lake yuko tayari kulipa kiasi chochote.
5. Kila kijana aamini kuwa anauwezo wa kufanya jambo fulani hata kama anahisi hana uwezo wa kufanya. Imani inaweza kufanya mambo makubwa.
Hapana mimi si mhanga wa ajira. Nimeajiriwa na Serikali lakini pia nimejiajiri mwenyewe hvyo nina uzoefu mkubwa wa kuweza kushahuri vijana maana mimi ni Business Coach