Nani afumbue fumbo hili?

Nani afumbue fumbo hili?

Mtu mmoja alikuwa ndani ya nyumba yake. Ghafla wakaja wageni kadhaa. Katika wageni hao kulikuwa na wababa wawili, watoto wawili, babu mmoja na mjukuu mmoja. Ikiwa jamaa (mwenyeji) anataka kukaa nje na wageni wake wote, Je atatoka na viti vingapi?

Welcome guys!!!

Tusiweke doubts ambazo kwenye swali la kwanza zimejibiwa HAPA TUNAONA INASEMWA IKWA ATATAKA KUKAA NJE NA WAGENI WAKE WOTE. MIMI NAONA NI VITI SABA.
 
Tusiweke doubts ambazo kwenye swali la kwanza zimejibiwa HAPA TUNAONA INASEMWA IKWA ATATAKA KUKAA NJE NA WAGENI WAKE WOTE. MIMI NAONA NI VITI SABA.

we elewa swali.. umeambiwa katika wageni hao kulikuwa na.... na si wageni ni...
 
Viti Vinne
1. Cha menyeji.
2. Babu ambaye ni baba pia.
3. Baba amabaye ni mtoto pia.
4. Mtoto.
 
kuna hujuma hapa nimejibu viti 4 post yangu imepotea, au hamkuta nijiunge leo na niwe mshindi?

TAFAKARI
HAKI ELIMU
 
Viti vinne.
Kimoja cha Babu (Baba #1)
Kimoja cha Mtoto wa babu (Baba # 2)
Kimoja cha mjukuu wa babu (Mtoto wa baba # 2)
Kimoja cha yeye mwenyewe mwenyeji wao.
 
Mtu mmoja alikuwa ndani ya nyumba yake. Ghafla wakaja wageni kadhaa. Katika wageni hao kulikuwa na wababa wawili, watoto wawili, babu mmoja na mjukuu mmoja. Ikiwa jamaa (mwenyeji) anataka kukaa nje na wageni wake wote, Je atatoka na viti vingapi?

Kiswahili saafi ni akina baba wawili na siyo wababa wawili
 
Attachments

  • brucelee.gif
    brucelee.gif
    16.9 KB · Views: 44
Mtu mmoja alikuwa ndani ya nyumba yake. Ghafla wakaja wageni kadhaa. Katika wageni hao kulikuwa na wababa wawili, watoto wawili, babu mmoja na mjukuu mmoja. Ikiwa jamaa (mwenyeji) anataka kukaa nje na wageni wake wote, Je atatoka na viti vingapi?

Welcome guys!!!

Viti 4 mkuu. Viti 3 kwa wageni na kiti 1 kwa mweyeji.
1 = Baba (babu)
2 = Baba (mtoto)
3 = mtoto (mjukuu)
4 = mwenyeji
Mkuu labda nibanie tuu ila nina uhakika na hili jibu
 
Mtu mmoja alikuwa ndani ya nyumba yake. Ghafla wakaja wageni kadhaa. Katika wageni hao kulikuwa na wababa wawili, watoto wawili, babu mmoja na mjukuu mmoja. Ikiwa jamaa (mwenyeji) anataka kukaa nje na wageni wake wote, Je atatoka na viti vingapi?

Welcome guys!!!

Hayo maneno ya rangi nyekundu yanatosha kutoa jibu. Wageni walikuwa kadhaa (hawana hesabu), waliotajwa ni miongoni mwa wageni wasiohesabika. Hivyo hatuwezi kujuwa idadi maalumu ya viti wakati hatujui idadi maalumu ya wageni. Fuata kanuni za lugha sio akili inavyotafsiri lugha.
 
Chemsha Bongo Nyingine hii..........Nitatoa Jibu baadae...
A man was looking at a potrait. Someone asked him, "Whose Picture are you looking at?" He replied: "Brothers and Sisters have I none, but this man's father is my father's son." ("This man's father" means, of course, the father of the man in the picture.) Whose picture was the man looking at?
 
Ataleta viti vitatu
kwani kuna babu,mwanae na mjukuu
(watoto wawili-baba(mtoto wa babu) na mwanae(mtoto wa baba)
wababa wawili-(babu na mwanae)
 
Back
Top Bottom