Nani aliagiza na waliohusika kumshambulia Tundu Lisu? Serikali itoe kauli au ifunge jalada

Kuna shahidi yoyote wa hilo tukio mkuu aliyekueleza alichokiona hadi sasa?
Inawezekana ndio maana wanasema muhusika wa ushahidi ni tundu mwenyewe na associates wake. Hii kesi haina hata mpita njia anayefahamu kilichotokea.
Au mimi ndio sijui?
-Lissu amesema muhusika ni Jiwe, ukimya/kigugumizi cha serikali kukanusha wanamlinda nani?
-Footages za CCTV cameras huwa zinabaki kwenye severs hivyo kung'oa cameras si kikwazo cha footages kutokupatikana. Polisi kwa nini wanakalia kimya suala la hizo footages ambazo ndiyo kielelezo kisicho na longolongo?
 
Na kumbuka.mchezo wa kuchezea katiba na chaguzi vimegharimu maisha ya wengi. Akwilina aliuawa akiwa siyo mshiriki wa maandamano.

Aliyesababisha maandamano sasa ndo boss Tume ya Uchaguzi. Je unadhani haya ni bahati mbaya?
Bas hatuna la kusema mkuu
 
Camera za CCTV eneo la tukio ndiyo msema kweli.

Kuna nini hadi zitolewe baada ya tukio?
Hata kama waling'oa zile CCTV cameras lakini footages huwa zinakuwepo kwenye severs, cameras huchukua footages na kuzirekodi.
Kwanini polisi(hasa awamu ya Jiwe) walizificha? Walikuwa wakimlinda nani? Je inawezekana waliziharibu kabisa kuficha/kuharibu ushahidi?
 
Tangu miaka ya 2000 inaanza ninajua uwepo wa softwares za kuretrive deleted data. Hata ukiiformat server mara kumi bado data zote zilizokuwepo zinaweza kuwa reatored.

Nini kinazuria utaalam wa kurudisha data kutumika ili ku unveil ukweli?
 
Lisu na Mbowe ilibidi hii ndiyo iwe agenda ya kwanza kwenye huu upatanishi. Mkuu wa nchi yupo na wahujumiwa (Lisu na Chadema) mpo, this was the first issue to be raised otherwise you are taking us for granted !
 
Tangu miaka ya 2000 inaanza ninajua uwepo wa softwares za kuretrive deleted data. Hata ukiiformat server mara kumi bado data zote zilizokuwepo zinaweza kuwa reatored.

Nini kinazuria utaalam wa kurudisha data kutumika ili ku unveil ukweli

ipo siku itaeleweka
saSA kuna AI it is a far advanced tech
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…