Nani aliiba idea ya mwenzake, Mwana FA au Jay Mo?

Hakuna aliyeiga idea ya mwenzake, kikubwa nilichokiona mimi ni kwamba kwenye ujana unaweza kuta watu wawili au wengi wenye mfanano wa kimawazo lakini tofauti inakuja kwenye uwasilishaji wa hayo mawazo yao. Mfano Jay moe yeye ameelezea jinsi mwanamke anaemtaka anavyotaka awe (Kama unataka dem sema unataka aweje aweje) lakini mwana fa yeye ameelezea namna ya wanawake anaowapenda na jinsi wanavyompenda (Mi na mabinti dam dam kaeli).
[emoji106][emoji106]

"رمضان كريم وصوم مقبول"
 
Amani iwe nanyi....!
Hilo wazo, na hiyo nyimbo kiasili ni ni ya Mo Techics. Nakumbuka Mo akiwa anahojiwa katika kituo cha Redio One Stereo, mtangaji akiwa ni Aboubakar Sadiki mwaka kama sikosei sana ni 2005; alipoulizwa swali kama hili alijibu....
"nyimbo ya Mimi na mabinti damudamu ilikuwa ni yangu, nikapanga nimshirikishe Mwana FA, ila huku na kule nikaisikia inapigwa redioni, ikiimbwa na Mwana FA."

Hivyo ikabidi yeye atumie "technics" zake aandike maneno mengine katika wazo karibiano. Na hapo ndipo akatoa ngoma ya "Kama unataka Demu." na mambo yakaisha hivyo.

Na nakumbuka akaendelea kusema, ni kama wananionea maana hata " beat" ya nyimbo ya Mzee wa Mitulinga/Niga Jay/Prof Jay ya "Promota", ni ya kwake(Jay Mo) na aliitumia kurekodi nyimbo yake ya "Cheza kwa step" ft Genious Ngwair(PKA). Lakini baada ya kupishana kidogo na Majani, mdundo akauziwa Prof Jay.

Lakini, baadaye waliyaweka sawa, na Mo akapewa mdundo mwingine, akaingiza tena mistari ya Cheza Kwa Step akiwa na jirani yake wa Chamber Squad(Ngwair) Mambo yakaisha kihivyo.

Hivyo basi, kati ya Jay Mo, na Mwana FA mwizi alikuwa Mwana FA.
 
Wote wamemtaja Radhia na Kithethe,Wote wamemtaja Seven....Nina imani 100% kuna mtu alidukua idea ya mwenzake ila NGOMA ZOTE ZILIKUWA KALI.

Ingekuwa vipi hiyo ngoma nakumbuka ilikuwa kama sio 2001 au 2002 hiyo..
 
Yes uwezekano wakufanana mawazo upo, lakini Kuna uwezekano mkubwa waliibiana idea ukizingatia hawa watu miezi michache kabla hawajatoa hizi ngoma walikuwa wameshirikiana kwenye kazi nyingine na walikuwa na ukaribu, na baada ya hizo ngoma kutoka ni kama walikuwa na kabifu ka chinichini
 
Ila sikatai kwa mtazamo wako kwani hata Dj carter alishaingia kwenye bifu na Q chillah kwa ajili ya Wiper, then Jaffarai pia alishaingia kwenye bifu na Q chillah kwa ajili ya my boo, Ngwea na Mchizi mox kwa ajili ya mikasi, na hiyo yote ni kutokana na kuwa aidha walikuwa wanafanyakazi pamoja au kuna mmoja alimshirikisha mwenzake kwenye uandishi wa nyimbo. Ila pia kama kuna mmoja alimuibia mwenzake basi Jay moe ndio mwenye idea ya wimbo, na snitch mwanakhamisi [emoji38][emoji38][emoji38] (aka Mwana fa) ndio ameiga mawazo ya Jay moe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
Kwa maana nyimbo ya Jay moe (Kama unataka dem) imepangika vizuri sana, beat nzuri na hata featuring nzuri (Solo thang) nyimbo imetulia tena haichuji. [emoji106][emoji106]

"رمضان كريم وصوم مقبول"
 
Pia tukumbuke hawa jamaa walikuwa wakifanya kazi kwa ukaribu kuanzia kwenye Ingekuwa vipi. [emoji106][emoji106][emoji106]

"رمضان كريم وصوم مقبول"
 
Kipindi hicho husikii kibakuli sijui domo wanaume watupu me hata dar sijaijua wajameni
 
Ile chorus ya Chillah ni faya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran mkuu

Its not over until its over...[emoji769]
 
Kama unataka dem ya Jay mo ni kali kushinda Mabinti ya Mwana FA. (Fikra zangu)

Ni ngoma mbili tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…