Nani aliipa jina la 'Taifa Stars' timu yetu? Linabeba ama kutangaza kitu gani kwa Nchi yetu?

Unadhani lipi laweza kuwa jina linalobeba hamasa kwa timu yetu ya Taifa? Likia akisi baraka na utajiri Mungu alio tukirimia kama Taifa..?
 
Jina la Taifa stars tu ndugu zangu wasukuma na wamakonde hawawezi kulitamka vizuri je tukiongeza likawa giraffe si ndio ajari za kujing'ata ulimi zitazidi usukumani..

Kama vipo waitwe "FARU JOHN"
Mkuu unajisikiaje ukirudia kusoma mchango wako.
 
Iitwe Kilimanjaro, hayo mengine hata ladha hayana.

kiĺïmanjaro zuri ila jiwe hapendi mkoa wa Kili na watu wake najua hatokubali
 
Samahani kwa kunakili habari yote. Mimi sijui na naomba unifahamishe stars maana yake nini?
Huenda lina maana ya "nyota" je ni nyota ipi hapo ndio kwenye tatizo..! Na je hiyo nyota inabeba ujumbe gani kwa Timu ya Taifa huko sitaki kuendelea ila naona kama neno "Nyota" halina morali yoyote kimichezo.
 
Je watumie utambulisho upi? Nimeona Giraffe kwenye ndege zetu. "Air Tanzania" na nikajaribu kuwaza sifa za kipekee za Twiga.
Kama ilivyoshauriwa hapo juu :Ningefurahi kama ingeitwa The Tanzanites au Cheetahs!
 
JAPO NAKILI SIJUI nickname ZAO ILA wenzetu wanatimu zao zinaitwa
ENGLAND
SPAIN
BELGIUM
BRAZIL
CROATIA
KWANINI TUSIJIITE TU TANZANIA? KAMA LINAUKAKASI KULINGANA NA MUUNDO WA MUUNGANO WETU BASI WATAFUTE JINA JINGINE NA SIO MAMBO YA WANYAMA.

England- Three lions
Spain - La Furia Roja ( The Red fury)
Belgium- Red Devils
Brazil - Seleção
Croatia- Vatreni ( The Blazers)
 
Mkuu tunafanyaje ili hoja ipate nguvu na kuwafikia wahusika?
Tuendeleze malalamiko na kulilaani jina Taifa stars na kuwaaminisha wengine kuwa hilo jina limelogwa,halifai,halina mvuto na ndiyo hasa kisa cha kushindwa kwetu kufikia mafanikio ya juu. Nimeandika kwa utani ila ndiyo hivyo.
 
Iitwe Kilimanjaro, hayo mengine hata ladha hayana.

kiĺïmanjaro zuri ila jiwe hapendi mkoa wa Kili na watu wake najua hatokubali
Natumai tunayo timu ya bara inayoitwa Kilimanjaro kisha nayo wameweka stars mbele..[emoji17]
 
Tuendeleze malalamiko na kulilaani jina Taifa stars na kuwaaminisha wengine kuwa hilo jina limelogwa,halifai,halina mvuto na ndiyo hasa kisa cha kushindwa kwetu kufikia mafanikio ya juu. Nimeandika kwa utani ila ndiyo hivyo.
Hapana labda tunaweza tengeneza hoja kuwa jina "Stars" halina morali ya kimichezo halitengenezi hamasa yaani "mzuka" wa watu kupambana.!
Mfano wanao penda kuangalia mieleka kuna baadhi ya wachezaji huwa wanavaa vinyago vya kutisha ama kujichora michoro hiyo natumai lengo huwa ni kiwatisha ama kuwatengenezea hofu wapinzani wao..
Jina la timu yetu ya Taifa linawafanya wapinzani wawaone wachezaji wetu kuwa warembo wenye kuvutia. "Stars"

Na hivyo kuwafanya watakavyo. Kichwa cha "mwendawazimu"!!

Hivi mfano wangeitwa "simba dume wa mikumi"

Nani anaweza kusogea kumnyoa ndevu simba..?
 
Bichwa la Mwendawazimu!! Hili jina nahisi linatutia gundu.
 
Ikiitwa Tanzania means na Zanzibar wapo ndani, ilhali kule nako wana timu yao Zanzibar Heroes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…