Nani aliipa jina la 'Taifa Stars' timu yetu? Linabeba ama kutangaza kitu gani kwa Nchi yetu?

Nani aliipa jina la 'Taifa Stars' timu yetu? Linabeba ama kutangaza kitu gani kwa Nchi yetu?

Wakuu hiki jina Taifa stars nani aliipa timu yetu yaTaifa? Linabeba ama kutangaza kitu gani kwa Nchi yetu?
Ninadhani kunapokuwa na mafanikio kwa timu ya Taifa ni fursa pia ya kutangaza alama maalumu ya Taifa ambayo bila shaka inaweza chochea pia utambulisho wetu na utalii wetu.

Mfano Uganda wanajiita the crane.
Bila shaka wakimaanisha ndege adimu wanaopatikana kwa wingi Uganda.

Wengine wanajiita "mamba weusi"
Wengine "Tai wa Jangwani"
Wengine "simba wa theranga"
Hapo jirani nadhani kwa sabbu ya machimbo ya shaba wanajiita "risasi za moto" chipolopolo.
Ama kule kusini wanajiita "Bafana bafana"

Je kwanini timu yetu ya Taifa isiwe na utambulisho maalumu wenye kuleta maana?

Mfano tukaiita timu yetu "the giraffe"..
"Tukiamini kuwa twiga ni mnyama anayekula majani ya juu ya miti."

Na anaeona Mbali zaidi adui yake kabla hajamkaribia. Pia Twiga ni kimbilio kwa wanyama wengi wasio weza kumuona adui yao kwa mbali..

Napendekeza timu yetu ya Taifa ya mpira wa Miguu iitwa "THE GIRAFFE "!

Timu yenyewe bado iko hoi ngoja iki peak tutaitafutia jina muafaka.
 
Tukijiita Twiga, tutafungwa kila siku, huangalii majina ya wenzetu!?
Simba wa Telanga...
Mamba sijui wa wapi...
Tai wa jangwani.....
Mbwa mwitu...
Mwewe wa Mbugani.....

Sasa wewe ujiite Twiga unamtisha nani? Si bora libaki hilo hilo Taifa stars.....
Coz Players ni Nyota wa Taifa.
 
Mkuu mtoto ukitaka asimame humuimbii nyimbo za hamasa? "Ile simama dede nikupe mkate"...... huimbwa wakati gani?

Huyu mzee sasa tumemuimbia simama dede kwa miaka mingi mpaka sasa ana wajukuu lakini hajasimama
 
Huyu mzee sasa tumemuimbia simama dede kwa miaka mingi mpaka sasa ana wajukuu lakini hajasimama
Tatizo nyota mkuu.! Mrisho Mpoto aliwahi imba

" tubadirishie wimbo huu tafadhari...."
Jina lina maana kubwa katika mafanikio lina maana katika kujenga kujiamini morali na hamasa ya kupambana.!

Unapomwita mchezaji wako "star" anakuwa kivutio "mrembo" "mzuri" kwa kila atakaye kuja kumtazama. "Kumchungulia"
Matokeo yake mwingine akatuita kichwa cha "mwenda wazimu"!
Bila shaka akiwa na maana ile ile mrembo mwenye kuvutia.! "Star"..

Hatuna utiisho, hatuwatishi wapinzani wetu bali sababu sisi ni nyota tunawavutia kufanya watakalo.
Tubadirishe vile tunavyoitwa...
 
TANZANITE MASAII MORANS (Warriors), Hapa tunaua ndege wawili kwa jiwe moja. Kwanza tuta paisha madini yetu pia tutaenzi moja ya kabila letu kubwa. Kwa kua Kenya pia kuna wa masai neno Tanzanite pia litakua likionesha tunaongelea upande wa Tanzania.Tuta ingiza ile hali ya ujasiri wa morani wa kimasai wa kuwinda kwenye mbuga zenye wanyama wakali na kunywa damu za wanyama. Kabla ya game wachezaji watacheza ile ngoma ya kimasai ya kupandisha mori hii itakua na mvuto wa kibiashara, pia italeta hali ya umoja na kupambana kwa wachezaji. Pia ita amsha hamasa kwa mashabiki kipindi mchezo una endelea mashabiki wana eza pia wakawa wanashangilia kwa kupandisha mori. New Zealand wana ngoma yao inaitwa HAKA huwa wanaicheza kabla ya michezo yao hua inahamsha hali na kuleta mvuto kwa timu zao. Jezi zetu pia zinaweza wekwa nakshi za Tanzanite uzuri nayenyewe ni ya blue.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa ktk taifa lolote timu ya taifa husika lazima ndo inakuwa taifa stars, so far jina hlo kwa timu yetu halina maana kwakuwa kila timu ya taifa lolote basi ni taifa stars.
Timu iitwe tu Tanzania kuitambulisha nchi yetu tuache kulalamika kila siku kunyanyaswa na mataifa wakati tunajinyanyasa wenyewe, wazungu hawatajua maana ya taifa stars ispokuwa wataambulia kujua neno stars tu ila ikiwa Tanzania watatuelewa tu.
Asie na uwezo wa kufanya kitu ndo hujiita star bali ajuae siku zote huwa mzalendo kutambulisha jina la uzawa na ataitwa star na wanao mshuhudia.
 
Tukijiita Twiga, tutafungwa kila siku, huangalii majina ya wenzetu!?
Simba wa Telanga...
Mamba sijui wa wapi...
Tai wa jangwani.....
Mbwa mwitu...
Mwewe wa Mbugani.....

Sasa wewe ujiite Twiga unamtisha nani? Si bora libaki hilo hilo Taifa stars.....
Coz Players ni Nyota wa Taifa.
Twiga ni one of the laziest animal, that epitome will transfer to the team as well.
Jina litishe, cheki hata rwanda wanajiita manyigu, yachezee manyigu uone moto wake.
 
Twiga ni one of the laziest animal, that epitome will transfer to the team as well.
Jina litishe, cheki hata rwanda wanajiita manyigu, yachezee manyigu uone moto wake.
Malawi wanajiita "the flames"..!
 
Tatizo nyota mkuu.! Mrisho Mpoto aliwahi imba

" tubadirishie wimbo huu tafadhari...."
Jina lina maana kubwa katika mafanikio lina maana katika kujenga kujiamini morali na hamasa ya kupambana.!

Unapomwita mchezaji wako "star" anakuwa kivutio "mrembo" "mzuri" kwa kila atakaye kuja kumtazama. "Kumchungulia"
Matokeo yake mwingine akatuita kichwa cha "mwenda wazimu"!
Bila shaka akiwa na maana ile ile mrembo mwenye kuvutia.! "Star"..

Hatuna utiisho, hatuwatishi wapinzani wetu bali sababu sisi ni nyota tunawavutia kufanya watakalo.
Tubadirishe vile tunavyoitwa...

We jamaa hatari unafaa kuwa mshenga maana unachonga balaa inabidi nikubali yaishe
 
JAPO NAKILI SIJUI nickname ZAO ILA wenzetu wanatimu zao zinaitwa
ENGLAND
SPAIN
BELGIUM
BRAZIL
CROATIA
KWANINI TUSIJIITE TU TANZANIA? KAMA LINAUKAKASI KULINGANA NA MUUNDO WA MUUNGANO WETU BASI WATAFUTE JINA JINGINE NA SIO MAMBO YA WANYAMA.
England Wanaitwa "The Three Lions" na Brazil wanaitwa "Seleçao"
 
Nadhani tungeipa majina yanayoweza kuitamgaza zaidi nchi yetu....Mfano badala ya Tanzania Bara kutumia jina la "Kilimanjaro Stars" jina hilo litumike kwa Timu ya Taifa badala ya Taifa Stars......
 
Back
Top Bottom