Nani alikuja na huu Utaratibu wa Kimasikini na wa Kishamba ndani ya Vichwa vya baadhi ya Watanzania?

Nani alikuja na huu Utaratibu wa Kimasikini na wa Kishamba ndani ya Vichwa vya baadhi ya Watanzania?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Sijui ni lini hii Poverty Mentality itaondoka ndani ya Vichwa vya Watanzania. Yaani unakutana na Mtu ana Simu ya Thamani Kubwa sana na ya Kisasa ( tena Boss mahala fulani ) halafu tena unamkuta ana Kasimu ka Shilingi Efu Aobaini au Elfu Thelathini na ukimuuliza kwanini ana hiyo Simu atakujibu kuwa Simu yake Kubwa huwa haikai na Chaji hivyo hiyo Simu ndogo ni Substitute ya Simu Kubwa pale ikiisha na Chaji.

Kama ilivyo kawaida yangu kwa Kupenda Kuchunguza na Kudadisi Mambo / Masuala / Vitu nikalazimika Kuulizia kwa Watanzania walioko Majuu ( Mamtoni Ulaya na Marekani ) na hata kwa Kuwaangalia Wazungu wengi ninaokutana nao hapa nchi ya Ugenini nilipo je, na Wao wana huu Upuuzi nilichokigndua ni kwamba wala hawana na Wao Wanatumia Simu zao kama Chaji zao zinavyosema na kwamba Chaji ikiisha tu wanachofanya ni Kuzima Simu kisha Kuichaji na kuendelea na Mawasiliano yao baadae au wananunua Power Banks ili kuhakikisha Chaji za Simu zao hazipungui lakini siyo kuwa na Simu ya Milioni Tatu halafu unakuwa na Kasimu ka Philips au Nokia ka Shliingi Elfu Arobaini au Elfu Thelathini Tandika au Ilala Boma.

Haya upesi sana Wewe Afisa Ubalozi nchi niliyoko sasa Kesho nisikukute na hako Kasimu Kako Kadogo kwani unaiabisha Tanzania sawa? Afisa Balozi gani unashindwa kununua Power Bank kwa ajili ya hiyo Simu yako ya Thamani na baalala yake unatembea na Simu zote Mbili huku hiyo Simu yako Ndogo Batani yake moja ikiwa imefutika Herufi kiasi kwamba ukiwa una Type inabidi uibahatishe hiyo Herufi?

By the way hata Mimi GENTAMYCINE ninayendika huu Uzi ni Masikini vile vile ila huu Upuuzi kamwe sitokuja Kuufanya. Ok?
 
Huwa ni tabia inayoashiria Umaskini au ubahiri. Kiumbe hana kazi hata ya kuuza kahawa lkn ana Laini 6 za simu maana ana simu 2 ambazo kila moja inakaa na laini 3 unabaki kujiuliza huyu mtu anachosumbukia ni kipi?

Mwanaume wa kweli simu moja inatosha huna haja kutembea na Makalokocho mkononi kisa Wa tigo umpigie kwa tigo Voda vile vile. Huu ni ukichaaa
 
Mkuu ulichosema "Ni ukweli wa maisha ya bongo

Unakuta mbongo kajenga mselfu Kisha hapo mlango sasa

Kuna mlango wa grili wenye viio na wa mbao tena na zote zina komeo

Mpaka una shindwa assume moto ikiwaka itakuwa aje?
 
Kua na simu kubwa na kiswaswadu kibongo bongo ni sawa kabisa maana umeme ni shida sana viswaswadu vinakaa sana na chaji .Pia kwa usalama kuna sehem unaweza kwenda si afya ukiwa na simu kubwa lakini ukiwa na kiswaswadu unapita kwa amani wakati simu kubwa umeificha na viswaswadu ni vyepesi kwa kuongea na mtu mda mrefu kuliko kushika simu kubwa masikioni mda mrefu...
 
Asee kitochi kitamu sana kutongozea unashusha mistari bila hta kuangalia button, mie watu wa sms za kawaida na kupiga na kupigiwa line yake nimeweka kwenye kitochi,, smartphone kama kuwasiliana ni watsap tu na telegram ukitoa hapo ni mwendo wa mavitabu, youtube na ku browse hasa huku jf
 
Poverty Mentality na Ushamba vinatutesa mno baadhi ya Watanzania.
Kuna baadhi yetu tunaendeshwa na mihemko tunafanya mambo Ili kutizamwa na wengine,
Au kuonekana wakuu sana
Kumbe wale wanaofanya hufanya Kwa sababu zao,
Ile wengi tunaisha kufanya kama kina flani wanavyofanya Ili tuonekane kama wao,bila kujua tuna Poteza yakwetu kwakuishi Kama wao
Mwisho wasiku watu wanatambua kumbe hatushi life letu
. tusi fake life ...
 
Poverty Mentality na Ushamba vinatutesa mno baadhi ya Watanzania.
Tanzania kuna vitu vingi sana watu wanaigana bila kutafakari ni kwa nini wanafanya hivyo. Ni vingi sana na hata ukihesabu humalizi. Kwenye simu pengine umeme ni hauaminiki? Ukizingatia mtanzania kwenye simu yake ana ma-group ya whatsup kama kumi na kila group msg za ku-share zinaingia karibu kila dakika.
 
Sijui ni lini hii Poverty Mentality itaondoka ndani ya Vichwa vya Watanzania. Yaani unakutana na Mtu ana Simu ya Thamani Kubwa sana na ya Kisasa ( tena Boss mahala fulani ) halafu tena unamkuta ana Kasimu ka Shilingi Efu Aobaini au Elfu Thelathini na ukimuuliza kwanini ana hiyo Simu atakujibu kuwa Simu yake Kubwa huwa haikai na Chaji hivyo hiyo Simu ndogo ni Substitute ya Simu Kubwa pale ikiisha na Chaji.

Kama ilivyo kawaida yangu kwa Kupenda Kuchunguza na Kudadisi Mambo / Masuala / Vitu nikalazimika Kuulizia kwa Watanzania walioko Majuu ( Mamtoni Ulaya na Marekani ) na hata kwa Kuwaangalia Wazungu wengi ninaokutana nao hapa nchi ya Ugenini nilipo je, na Wao wana huu Upuuzi nilichokigndua ni kwamba wala hawana na Wao Wanatumia Simu zao kama Chaji zao zinavyosema na kwamba Chaji ikiisha tu wanachofanya ni Kuzima Simu kisha Kuichaji na kuendelea na Mawasiliano yao baadae au wananunua Power Banks ili kuhakikisha Chaji za Simu zao hazipungui lakini siyo kuwa na Simu ya Milioni Tatu halafu unakuwa na Kasimu ka Philips au Nokia ka Shliingi Elfu Arobaini au Elfu Thelathini Tandika au Ilala Boma.

Haya upesi sana Wewe Afisa Ubalozi nchi niliyoko sasa Kesho nisikukute na hako Kasimu Kako Kadogo kwani unaiabisha Tanzania sawa? Afisa Balozi gani unashindwa kununua Power Bank kwa ajili ya hiyo Simu yako ya Thamani na baalala yake unatembea na Simu zote Mbili huku hiyo Simu yako Ndogo Batani yake moja ikiwa imefutika Herufi kiasi kwamba ukiwa una Type inabidi uibahatishe hiyo Herufi?

By the way hata Mimi GENTAMYCINE ninayendika huu Uzi ni Masikini vile vile ila huu Upuuzi kamwe sitokuja Kuufanya. Ok?
 
Mimi kwa maoni yangu kusema ukweli mimi naona ukweli usemwe tu maana naona naweza nikaongea na katika hatua hii ndugu zangu nafikiri na naona kabisa kuwa kwa muda huu naona na natamani niongee kuhusu haya na nina mengi ya kusema moyoni lakini kuhusu hili acha nichangie hoja kwa kusema ni kweli mnayosema na mimi sina la kusema
 
Nima walakini na jinsia yako

Yaani kidume mzima unatembea na power bank ili nini?

Mwanaume lijali ana simu 1 wala hana mikoba ya kubeba power bank

Popoma nitakufundisha miikonya kiume hadi lini

Anyway kesho ntakunulia mkoba na kipochi cha rangi ya pink ubebe power bank yako
 
Back
Top Bottom