Nani Alikuwa Bora kati ya Zidane na Ronaldinho?

Nani Alikuwa Bora kati ya Zidane na Ronaldinho?

Nani Alikuwa Bora Kati ya Zidane na Ronaldinho?


  • Total voters
    27
  • Poll closed .
huu mjadala wa zidane na gaucho kiupande fulani unashabihiana zaidi na mjadala unaoendelea kutikisa ulimwengu nyakati hizi unaomuhusu Virgil van Dijk,

je! anastahili kuwekwa katika kundi la walinzi bora kama walivyo legends wengineo tuliopata kuwashuhudia kwa miaka hii 15 iliopita?

  • kama tutaangalia performance yake anayoendelea kuionyesha uwanjani na nidhamu yake basi bila shaka virgil anastahili kuwepo katika kundi la walinzi bora licha ya kuushuhudia ubora wake kwa muda mfupi (wengi wetu tumeanza kumfuatilia akiwa liverpool)....
  • ila kama tutatumia kigezo cha muda basi jamaa bado hapaswi kuwekwa katika kundi la walinzi bora kuwahi kutokezea duniani (nilichojifunza wengi wao wanaopingana na van virgil hujificha kwenye hoja hii ya muda, inawezekana vipi van virgil awe sawa au zaidi ya nemanja vidic, john tery, rio ferdinand na wengineo haliyakuwa ubora wake tumeushuhudia zaidi kwa kipindi cha miaka mitatu tu.......
===========================
hivyo hivyo kwenye huu mjadala wa gaucho na zidane
  1. kutoka 2003 hadi 2008 ronaldinho gaucho alikuwa bora zaidi kuliko mchezaji mwengine yeyote duniani, ndani ya muda mfupi alifanikiwa kuleta mapinduzi makubwa sana ya soka hapa ulimwenguni kiasi ambacho wengi wetu tumejikuta tukiwashukuru wazazi wake wawili kwa kufanikiwa kucheza mechi nzuri usiku na hatimaye wakatuletea kijana machachari asiyekasirika, kama hatutoipa nafasi hoja ya muda basi gaucho anapaswa kuwekwa katika kundi moja na legends wengineo waliofanikiwa kuleta mapinduzi makubwa ya soka.
  2. ila kama tutaipa nafasi hoja ya muda basi tutakuwa tunaleta utani na mzaha wa kutokufunga mipaka ya kifikra kwa tendo la kumpa heshima ronaldinho ya Nabii wa mwisho wa mpira kama walivyoandika na wanavyoendelea kuandika baadhi ya wachangiaji....kiufupi tukitumia hoja ya muda basi gaucho anapaswa awekwe kundi moja na wachezaji aina ya maradona na ricardo kaka
  3. kwenye huo mjadala wa zidane na gaucho:kama tutaitumia hoja ya kuwa kwenye ubora wa kiwango kwa muda mrefu (consistency), nidhamu ndani ya uwanja, nje ya uwanja bila ya kusahau nidhamu ya mwili na fikra (physical and mental fitness) bila ya shaka tutakuwa tunafanya makosa makubwa sana kumlinganisha ronaldinho gaucho dhidi ya zinedine zidane....
  4. baada ya kuondoka Spain mnamo mwaka 2008, Ronaldinho alishindwa kurudisha makali yake aliyoyaonyesha Barcelona kwa kipindi cha miaka mitano aliyodumu pale nou camp, kiufupi gaucho alibaki kutembelea umaarufu wake pamoja na skills alizojaaliwa, imagine ndani ya misimu minne pale Milan jamaa alifanikiwa kucheza takribani michezo 96 tu kama nitakuwa nipo sahihi,
  5. finally tunajifunza ya kwamba kumbe josep guardiola alikuwa sahihi kumuondoa gaucho na hatimaye kutengeneza dynasty mpya iliongozwa na mfalme messi, leo hii dynasty ya lionel messi inaendelea kudumu huu ukiwa ni mwaka wa 12 wakati dynasty ya gaucho ilidumu kwa miaka minne tu pale nou camp...kwa ufupi gaucho alishindwa kujiheshimu ndio maana alipotea kwenye ulimwengu wa soka la ushindani kwa muda mfupi.
  6. ukija kwa zinedine zidane hali ni tofauti, jamaa alidumu kwenye ubora wake kwa takribani miaka 18 (1997-2006) na ndani ya miaka hiyo alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 3 kama nitakuwa nipo sahihi (ronaldo na messi pekee ndiye wamemzidi)......zizou anaishi kwenye kundi la wachezaji waliojiheshimu kimwili na kifikra kama vile lionel messi, cristiano ronaldo (si delima phenomeno mwenye kilo 300), andrea pirlo, paul scholes, frank lampard, steven gerrard pamoja na babu yao pele ndio maana si ajabu alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora akiwa na miaka 34 (kama sipo sahihi mutanirekebisha) na ndiye anayeshikilia rekodi ya kushinda tuzo akiwa na umri mkubwa
yupi ni bora zaidi nje ya hoja ya muda?
itategemea na mahitaji husika ya timu, kama nitahitaji mchezaji atakeyeunganisha safu ya ushambuliaji basi sitosita kumchagua ronaldinho gaucho kwa sababu atanipa huduma nyingi sana zaidi ya zidane (atafunga magoli mengi, assist, ataifanya safu ya ulinzi ya timu pinzani muda wote wawe kwenye hali ya presha, dancing, dribbling n.k)
copy ya gaucho ni neymar​

ila kama nitahitaji mwanadamu atakayekuwa kiunganishi between safu ya kiungo pamoja na safu ya ushambuliaji basi nitamchagua zidane haijalishi awe na miaka 40 ya kuzaliwa.
copy ya zidane ni iniesta​

mchango ndani ya timu ya taifa ya wakubwa
kuna mdau fulani alisema alianza kuvutiwa na soka baada ya kushuhudia miujiza ya gaucho mnamo mwaka 2002 na pia namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuifuatilia live michuano ile ya world cup, kiupande wangu najiaminisha ya kwamba gaucho alikuwa ndiye mchezaji wa tano kiubora ndani ya kikosi kile cha Brazil (ronaldo, rivaldo, cafu, carlos, gaucho, lucio, gilberto). Mnamo mwaka 2006 gaucho akiwa kwenye ubora wake alishindwa kuipa mafanikio timu yake ya brazil (nakumbuka walitolewa robo fainali dhidi ya france).
world cup ya 2010 gaucho hakuchaguliwa kwenye kikosi cha brazil jambo lililopelekea baadhi ya mashabiki kumuangushia mzigo wa lawama kocha wa brazil (dunga), waongozaji wakuu wa kampeni ile walikuwa ni washabiki wapenda rangi (show game) na si team work and match fitness...hivi unamchaguaje mchezaji aliyecheza chini ya mechi 70 ndani ya miaka mitatu?

ukija upande wa pili tunajifunza ya kwamba ufaransa ilikuwa ni zidane na zidane ndio ufaransa kuanzia world cup 1998 hadi world cup 2006.
1998 = ufaransa wanabeba ubingwa wa dunia
2002= france wanatolewa hatua ya makundi (kutokuwa fiti kwa zidane pia kulichangia matokeo mabaya)
2000= ufaransa wanabeba kombe la euro
2004= france wanafungwa robo fainali dhidi ya greece michuano ya euro
2006= france wanafungwa fainali dhidi ya Italy

tuwaache hao wanadamu wawili wapumzike
 
Hata kuna kutokea mtu kama Gaucho.

Mara tatu washabiki wa Real madrid walisimama uwanjani kama heshima kwa Rinadinho wakati barcelona na Realmadrid na paka na panya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
let's take ourselves back to 2006 world cup quarter final match,France vs Brazil and just see how zizzou managed to outplay gaucho,Ronaldo de Lima,Kaka,ze Roberto and likewise,....to me zidane is the best than ronaldinho
Rudi Game ya Madrid v Barca pale Santiago Bernabeu, Madrid akiwa na Zidane, Figo, Ronaldo de Lima n.k

Barca ikiwa na Messi, Eto'o na Gaucho.

Bernabeu ilipaswa kumpigia makofi Gaucho.

Nnachojaribu kukwambia ni kuwa usitazame Game moja kutoa matokeo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shabiki yeyote wa gaucho huwa hana hoja za kujitetea...mara nyingi huwa nawauliza maswali wanakimbia...


Wachezaji wangu wa muda wote[emoji116]

Messi
Maradona
[emoji115]Hawa ni level ya kipekee, since dunia iumbwe hapakutokea na hawatatokea viumbe wanaojituma, kuuchezea na kuutendea haki mpira like Messi and Diego(Golden boy)

Level ya Gaucho[emoji116]

Ronaldo
Zidane
Lewandowski
Sadio
Salah
Hazard
De lima
Iniesta
Xavi
Okocha
Requelme
Henry
Suarez
Aguero
Bagio

Pamoja na kuwa at same level but Cr7, Iniesta, Xavi na Suarez wana mafanikio kuzidi hao wote + Gaucho wenu...


Messi na Maradona weka mbali na watoto, tena msiwalinganishe na hao watoto...
Suarez????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
El clasico 2005 rejelea ukamuone dinho

Sent using Jamii Forums mobile app


Nimegundua wewe na hata wenzio mnachoangalia ni show game isiyo na faida yoyote katika timu na ndio maana Barca wakamfukuza baada ya ujio wa King Messi...Zidane mchezaji bora wa 4 ama wa 5 utamcompare vipi na huyu jamaa yako hata 10 bora hayumo!!! Zidane alikuwa mtu wa kazi show game kidogo lakini kazi yake ilikuwa sio ya kitoto, na ndio maana hakosekani 5 bora...ila kwakuwa hayo ni maoni yako hakuna anae kulazimisha!
 
Kama tutaongelea kiburudani sidhani kama kuna mchezaji alikuwa na buridani kama Gaucho.

Lakini ki soccer...nampa Zidane.... Zidane ni moja wachezaji wachache wenye uwezo wa kuibeba timu na mchango wake ukaonekana kwa anavyopambana kuhakikisha ushindi. Just like C. Ronaldo au Messi.

Gaucho ni Neymar mwenye uwezo mkubwa tu.
Diego Maradona na Messi ndio wamenifanya niupende mpira...wana kila kitu cha kunifanya niwakubali zaidi ya mchezaji yeyote duniani, kuuchezea mpira watakavyo they can, kwenye mafanikio ndio usiseme "jeshi la mtu mmoja"


Kama hukuwahi kumuona Yo Soy El diego Armando era yake, hebu mcheki kidogo uone craziest dribbling japo kacheza muda mfupi mno 👇 Gaucho akasome...na ukitaka zaidi zipo youtube....





 
Zidane hamfikii hata INIESTA.

Yani watu kama ninyi mkipewa hata exam ya standard 2 mtapuyanga tu 😀

Zidane ni mchezaji bora wa 4 ama wa 5...Gaucho je? Hata 10 bora hayumo! Humu kumejaa mashabiki na sio wanasoka...but that's your opinion, No one is forcing you...
 
Rudi Game ya Madrid v Barca pale Santiago Bernabeu, Madrid akiwa na Zidane, Figo, Ronaldo de Lima n.k

Barca ikiwa na Messi, Eto'o na Gaucho.

Bernabeu ilipaswa kumpigia makofi Gaucho.

Nnachojaribu kukwambia ni kuwa usitazame Game moja kutoa matokeo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We binti hebu kuwa na heshima hata kidogo. Ronaldo ambaye hata kwa Messi anasumbuana naye ndio umlinganishe na Balozi wa soka la mbinguni duniani?? Unapozungumzia masuala ya soka UCHO mfungie kabatini, then endelea kudiscuss kuhusu hawa wengine. Alaaaaah!!
[emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchezaji bora kwangu wa muda wote ni RONALDO DE LIMA, huyu mwamba alikua anakila kitu ambacho mchezaji anatakiwa awe nacho.
 
Back
Top Bottom