DAEMUSHIN
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,428
- 120,464
huu mjadala wa zidane na gaucho kiupande fulani unashabihiana zaidi na mjadala unaoendelea kutikisa ulimwengu nyakati hizi unaomuhusu Virgil van Dijk,
je! anastahili kuwekwa katika kundi la walinzi bora kama walivyo legends wengineo tuliopata kuwashuhudia kwa miaka hii 15 iliopita?
hivyo hivyo kwenye huu mjadala wa gaucho na zidane
itategemea na mahitaji husika ya timu, kama nitahitaji mchezaji atakeyeunganisha safu ya ushambuliaji basi sitosita kumchagua ronaldinho gaucho kwa sababu atanipa huduma nyingi sana zaidi ya zidane (atafunga magoli mengi, assist, ataifanya safu ya ulinzi ya timu pinzani muda wote wawe kwenye hali ya presha, dancing, dribbling n.k)
ila kama nitahitaji mwanadamu atakayekuwa kiunganishi between safu ya kiungo pamoja na safu ya ushambuliaji basi nitamchagua zidane haijalishi awe na miaka 40 ya kuzaliwa.
mchango ndani ya timu ya taifa ya wakubwa
kuna mdau fulani alisema alianza kuvutiwa na soka baada ya kushuhudia miujiza ya gaucho mnamo mwaka 2002 na pia namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuifuatilia live michuano ile ya world cup, kiupande wangu najiaminisha ya kwamba gaucho alikuwa ndiye mchezaji wa tano kiubora ndani ya kikosi kile cha Brazil (ronaldo, rivaldo, cafu, carlos, gaucho, lucio, gilberto). Mnamo mwaka 2006 gaucho akiwa kwenye ubora wake alishindwa kuipa mafanikio timu yake ya brazil (nakumbuka walitolewa robo fainali dhidi ya france).
world cup ya 2010 gaucho hakuchaguliwa kwenye kikosi cha brazil jambo lililopelekea baadhi ya mashabiki kumuangushia mzigo wa lawama kocha wa brazil (dunga), waongozaji wakuu wa kampeni ile walikuwa ni washabiki wapenda rangi (show game) na si team work and match fitness...hivi unamchaguaje mchezaji aliyecheza chini ya mechi 70 ndani ya miaka mitatu?
ukija upande wa pili tunajifunza ya kwamba ufaransa ilikuwa ni zidane na zidane ndio ufaransa kuanzia world cup 1998 hadi world cup 2006.
1998 = ufaransa wanabeba ubingwa wa dunia
2002= france wanatolewa hatua ya makundi (kutokuwa fiti kwa zidane pia kulichangia matokeo mabaya)
2000= ufaransa wanabeba kombe la euro
2004= france wanafungwa robo fainali dhidi ya greece michuano ya euro
2006= france wanafungwa fainali dhidi ya Italy
tuwaache hao wanadamu wawili wapumzike
je! anastahili kuwekwa katika kundi la walinzi bora kama walivyo legends wengineo tuliopata kuwashuhudia kwa miaka hii 15 iliopita?
- kama tutaangalia performance yake anayoendelea kuionyesha uwanjani na nidhamu yake basi bila shaka virgil anastahili kuwepo katika kundi la walinzi bora licha ya kuushuhudia ubora wake kwa muda mfupi (wengi wetu tumeanza kumfuatilia akiwa liverpool)....
- ila kama tutatumia kigezo cha muda basi jamaa bado hapaswi kuwekwa katika kundi la walinzi bora kuwahi kutokezea duniani (nilichojifunza wengi wao wanaopingana na van virgil hujificha kwenye hoja hii ya muda, inawezekana vipi van virgil awe sawa au zaidi ya nemanja vidic, john tery, rio ferdinand na wengineo haliyakuwa ubora wake tumeushuhudia zaidi kwa kipindi cha miaka mitatu tu.......
hivyo hivyo kwenye huu mjadala wa gaucho na zidane
- kutoka 2003 hadi 2008 ronaldinho gaucho alikuwa bora zaidi kuliko mchezaji mwengine yeyote duniani, ndani ya muda mfupi alifanikiwa kuleta mapinduzi makubwa sana ya soka hapa ulimwenguni kiasi ambacho wengi wetu tumejikuta tukiwashukuru wazazi wake wawili kwa kufanikiwa kucheza mechi nzuri usiku na hatimaye wakatuletea kijana machachari asiyekasirika, kama hatutoipa nafasi hoja ya muda basi gaucho anapaswa kuwekwa katika kundi moja na legends wengineo waliofanikiwa kuleta mapinduzi makubwa ya soka.
- ila kama tutaipa nafasi hoja ya muda basi tutakuwa tunaleta utani na mzaha wa kutokufunga mipaka ya kifikra kwa tendo la kumpa heshima ronaldinho ya Nabii wa mwisho wa mpira kama walivyoandika na wanavyoendelea kuandika baadhi ya wachangiaji....kiufupi tukitumia hoja ya muda basi gaucho anapaswa awekwe kundi moja na wachezaji aina ya maradona na ricardo kaka
- kwenye huo mjadala wa zidane na gaucho:kama tutaitumia hoja ya kuwa kwenye ubora wa kiwango kwa muda mrefu (consistency), nidhamu ndani ya uwanja, nje ya uwanja bila ya kusahau nidhamu ya mwili na fikra (physical and mental fitness) bila ya shaka tutakuwa tunafanya makosa makubwa sana kumlinganisha ronaldinho gaucho dhidi ya zinedine zidane....
- baada ya kuondoka Spain mnamo mwaka 2008, Ronaldinho alishindwa kurudisha makali yake aliyoyaonyesha Barcelona kwa kipindi cha miaka mitano aliyodumu pale nou camp, kiufupi gaucho alibaki kutembelea umaarufu wake pamoja na skills alizojaaliwa, imagine ndani ya misimu minne pale Milan jamaa alifanikiwa kucheza takribani michezo 96 tu kama nitakuwa nipo sahihi,
- finally tunajifunza ya kwamba kumbe josep guardiola alikuwa sahihi kumuondoa gaucho na hatimaye kutengeneza dynasty mpya iliongozwa na mfalme messi, leo hii dynasty ya lionel messi inaendelea kudumu huu ukiwa ni mwaka wa 12 wakati dynasty ya gaucho ilidumu kwa miaka minne tu pale nou camp...kwa ufupi gaucho alishindwa kujiheshimu ndio maana alipotea kwenye ulimwengu wa soka la ushindani kwa muda mfupi.
- ukija kwa zinedine zidane hali ni tofauti, jamaa alidumu kwenye ubora wake kwa takribani miaka 18 (1997-2006) na ndani ya miaka hiyo alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 3 kama nitakuwa nipo sahihi (ronaldo na messi pekee ndiye wamemzidi)......zizou anaishi kwenye kundi la wachezaji waliojiheshimu kimwili na kifikra kama vile lionel messi, cristiano ronaldo (si delima phenomeno mwenye kilo 300), andrea pirlo, paul scholes, frank lampard, steven gerrard pamoja na babu yao pele ndio maana si ajabu alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora akiwa na miaka 34 (kama sipo sahihi mutanirekebisha) na ndiye anayeshikilia rekodi ya kushinda tuzo akiwa na umri mkubwa
itategemea na mahitaji husika ya timu, kama nitahitaji mchezaji atakeyeunganisha safu ya ushambuliaji basi sitosita kumchagua ronaldinho gaucho kwa sababu atanipa huduma nyingi sana zaidi ya zidane (atafunga magoli mengi, assist, ataifanya safu ya ulinzi ya timu pinzani muda wote wawe kwenye hali ya presha, dancing, dribbling n.k)
copy ya gaucho ni neymar
ila kama nitahitaji mwanadamu atakayekuwa kiunganishi between safu ya kiungo pamoja na safu ya ushambuliaji basi nitamchagua zidane haijalishi awe na miaka 40 ya kuzaliwa.
copy ya zidane ni iniesta