Nani alimpa u-'SIR' George Kahama?, Tanzania wenye cheo hiki wapo wangapi?

Sir George Kahama u-Sir wake alipewa na Mzee Nyerere kwa utani tu alikuwa anamwita Sir, basi ikang`ang`ania.
 

mambo ya kunukuu, weka kwa kiswahili
 
Elton John nae alipataje U-Sir?
umagharibi si wa kuiga hata kidogo

Kupata knighthood kuna vigezo kadhaa. Huyu jamaa alipata kutokana nammchango wake mkubwa katika muziki. Andy Chande alipewa KBE kwa kilichoitwa "protecting British interests in Tanzania". George Kahama alikuwa mtani tu wa Nyerere.
 
Ha ha ha kumbe sir Kahama ni wa kuzuga nishagoogle sana sijapata jibu leo nimecheka sana
 
Huitaji kuwa knighted kuitwa "sir". Ukipanda kwenye ndege kuelekea ulaya au usa utaitwa "sir" na mhudumu kwenye ndege. Ukishuka airport utaitwa "sir". Hotelini na mitaani vivyo hivyo.
 
Napenda kujua mtu mpaka anaitwa SIR awe na vigezo gan?. Halaf mbona sijawah sikia mwanamke akiitwa SIR!??. Karibun tujadili.

Kwa humu JF ni mpaka uwe mpigwa ban wa kufa mtu na wa mara kwa mara kama member mwenzetu GENTAMYCINE ndipo unaweza kuitwa " Sir ". Sijui huko kwingineko.
 
Naukumbuka huu wimbo ".............Nilishituka nikazimia kusikia msemo huo,nikiwa bado sijiwezi wote walinizunguka
Chorus/"Put water on the sir you find the sir is dry...........sikieni kioja hiki.....ooh yes sir are you very dry!
 
Hivi yule aliyesafiri safari nyingi za nje kuliko alivyosafiri kwenda kumtembelea mzazi wake hastahili huo u sir?
 
Kwa hiyo ni malkia pekee ndo anatoa hik cheo dunia nzima? why?
 
Napenda kujua mtu mpaka anaitwa SIR awe na vigezo gan?. Halaf mbona sijawah sikia mwanamke akiitwa SIR!??. Karibun tujadili.
Mkuu nafikiri hapa kwetu Sir George Kahama na yule Chairman wa Freemansons Sir Chande hao ndio wanaweza kukupa jibu la uhakika na sio ya kusoma kwenye Wikipedia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…