Nani alimtuma Issa Shivji The Professor?

Nani alimtuma Issa Shivji The Professor?

George J Minja

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
289
Reaction score
203
Nilimsikiliza kwenye mdahalo wake wakuaga uongozi wa kigoda cha Mwalimu Nyerere,imesoma ile hotuba yake mara kadhaa na kugundua kuwa sio bure Mwanataaluma huyu alitumwa na akatumika.

Kwa msomi kuwa mnafki haipendezi;Profesa huyu anaujua ukweli wa hali halisi na mazingira ya Muungano wetu kwa sasa anajua ni jinsi gani watanganyika wamedhulumiwa serikali yao kwa miaka mingi,anajua maoni yaliyokusanywa na Tume ya Warioba ni maoni ya wananchi na sio maneno ya Warioba na tume yake ,anajua ni jinsi gani Matatizo ya Muungano yasivyoisha na hayawezi kuisha kweli leo anasema Serikali mbili ndio suluhisho??Baada ya kushindwa kutatua matatizo haya kwa miaka zaidi ya 40 msomi alietukuka anasema serikali mbili ndio mwarobaini??

Inanishangaza sana na leo nimeanza na hili la serikali tatu kwsho nitakuja na jambo lingine la ajabu kabisa ambalo waliomtuma Shivji wamemuambia awadanganye watanzania pia


Acheni kuitumikia CCM imeelemewa na inazama sasa

"Problems canot be solved with the same level of thinking that created them""hii ni principle sio Siasa we need someone else to solve our problems and in this case and time we have CHADEMA ndio mwarobaini sio Shivji na siasa za uvungungi dont fight from dark tangaza wewe ni mwanachama wa CCM na unafanya kazi zao kwa wasomi.
 
Alitumwa na Nape,watu njaaa sana mkuu wewe wasikilize leo wako Nkrumah uone wanavyojipendekeza sijui kazi na faida za Usomi wao ni nini kwa taifa hili.
 
hapo kwenye weusi kunaonesha kuwa kinachokusumbua ni jina Tanganyika. shivji ni muumini wa muungano. watawala kushindwa kutatua kero za muungano siyo kosa la shivji. anaona serikali 3 zitasababisha muungano kuvunjika. kosa lake ni lipi kuamini hivyo? TAFADHALI USIMDHALILISHE SHIVJI KWA KUSEMA AMETUMWA! KUWA NA ADABU. wakumlaumu ni nyerere alieitwa na kennedy na kuombwa aungane na znz kwa kuhofia kusambaa kwa ukomunisti afrika mashariki. znz ilikua na itikadi za kikomunisti. ALIETUMIKA KUIFUNIKA TANGANYIKA NI NYERERE SIYO SHIVJI. acha ujuha!
 
Naona ulikuwa mpango Mkakati wa muda mrefu tangu Enzi za TANU hadi CCM kwamba watanzania wanyimwe elimu ili iwe rahisi kuwatawala, na wale waliojitambua SERIKALI za TANU/ASP na baadaye CCM ziliwanyamazisha kwa kashfa mbali mbali za kutungwa na mpaka leo wako kimya!! Chief Fundikira, Kasanga Tumbo, James Mapalala, Abdulrahman Mohamed Babu, Oscar Kambona nk nk!! Na wale waliokubaliana na SYSTEM wengi ambao ni GENIUS waliingizwa UWT/TISS nina wasi wasi Prof Shivji (Japo ninamheshimu sana) naye yumo ndani ya kundi hilo kama Prof Paramagamba Kabudi!! Hawa wote ni wapinzani MAHIRI wa demokrasia na wanatumia mbinu za hali ya juu sana ili wasigundulike!! Sasa Prof Shivji nadhani na umri umeenda (You can not teach an old dog new techniques/skills)that's why anachanganya MADESA kiulaini!! Anasahau kwamba serikali TATU ni maoni ya watanzania (siyo ya Warioba et al) na serikali mbili ni CCM and her allies (Shivji et al inclusive???) SHAME ON HIM!!!
 
Wewe hujawahi kumuelewa Shivji
tatizo ni uwezo wako wa kuelewa..
Shivji kasema mbona hakuna hansard za majadiliano kati ya wajumbe wa tume?
je hili la serikali tatu lilikuwa ni makubaliano ya maafikiano au makubaliano ya kushindwa maafikiano?
was it a compromise?

wewe hujaelewa hayo yoote.....
 
Wakati mwingine unaweza ukaanza kurusha mateke hewani ukifikiri utampata unayetaka kumtandika kumbe mtu mwenyewe hata hayupo. You're missing a point.

Kasome kwanza alichokisema Prof. Shivji ili ukielewe na pia naomba utambue kuwa kila Mtanganyika na Mzanzibari ana maoni kama yalivyo maoni yako.

Kama yeye anatumika na CCM, na wewe utakuwa unatumika na nani kwa sababu hawezi yeye kutumika na wewe usitumike.

Huoni kama mawazo yako ndiyo yanaonekana zaidi kama unatumika.

Kwangu mimi ninatakata wananchi wapewe fursa ya kupiga kura ya maoni kuchagua kama wanataka muungano au waachane nao.

Serikali mbili zimeshindwa kuondoa matatizo kwa sababu hazikuingia kwenye muungano zikiwa na nguzo imara za kisiasa ambazo ni kukubalika kwa wingi na wananachi. Muungano ulikuwa ni makubaliano ya viongozi wakuu wawili.

Serikali tatu ni barabara ya kuua muungano lakini kwa gharama kubwa.

Serikali moja ni dawa ya muungano lakini hakuwezekani kwa siasa na wanasiasa wa Tanzania kwa sababu ya ubinafsi wao.
 
Yan hoja ulizoraise hapa ukilinganisha na alicho analyse shivji kuhusu rasimu nadiriki kusema wewe ni 0 kabisa,kutokana na analysis aliyo fanya tume wameamua kumuita yeye kama mtu binafsi pekee ukiachilia kundi la viongozi wa kisiasa kutoa maoni yake....tuliwahi kuambiwa na prof mmoja kwamba ni vigumu sana kwa watu wenye upeo mdogo kumuelewa prof sasa nimeanza kuamin kauli ile
 
Prof. Shivji katoa maoni yake kama SHIVJI, yaweza kuwa sahihi au kutokuwa sahihi. Nadhani maandishi yake ya nyuma na mtizamo wake wa sasa vinaweza kuwa vinakanganya tukifikiri kwa upeo mdogo. Hapo nyuma ni maoni yangu kuwa àliutazama uhalali wa kisheria wa muungano kama ulivyo kwenye mkataba na sheria za muungano (1964), ni wazi kuwa muungano katika ujenzi ulikiuka mambo flani kisheria, lakini sasa àmetoa nadharia anayoifikiria yaweza kufit political legimacy ya muungano na kujenga consititutional basis.
 
Wewe hujawahi kumuelewa Shivji
tatizo ni uwezo wako wa kuelewa..
Shivji kasema mbona hakuna hansard za majadiliano kati ya wajumbe wa tume?
je hili la serikali tatu lilikuwa ni makubaliano ya maafikiano au makubaliano ya kushindwa maafikiano?
was it a compromise?


wewe hujaelewa hayo yoote.....
Correct. Amemtuhumu Prof. jumla jumla tu.
 
Naona ulikuwa mpango Mkakati wa muda mrefu tangu Enzi za TANU hadi CCM kwamba watanzania wanyimwe elimu ili iwe rahisi kuwatawala, na wale waliojitambua SERIKALI za TANU/ASP na baadaye CCM ziliwanyamazisha kwa kashfa mbali mbali za kutungwa na mpaka leo wako kimya!! Chief Fundikira, Kasanga Tumbo, James Mapalala, Abdulrahman Mohamed Babu, Oscar Kambona nk nk!! Na wale waliokubaliana na SYSTEM wengi ambao ni GENIUS waliingizwa UWT/TISS nina wasi wasi Prof Shivji (Japo ninamheshimu sana) naye yumo ndani ya kundi hilo kama Prof Paramagamba Kabudi!! Hawa wote ni wapinzani MAHIRI wa demokrasia na wanatumia mbinu za hali ya juu sana ili wasigundulike!! Sasa Prof Shivji nadhani na umri umeenda (You can not teach an old dog new techniques/skills)that's why anachanganya MADESA kiulaini!! Anasahau kwamba serikali TATU ni maoni ya watanzania (siyo ya Warioba et al) na serikali mbili ni CCM and her allies (Shivji et al inclusive???) SHAME ON HIM!!!
Hakuna msomi aliye na maarifa mengi kuliko UZOEFU.PROF SHIVJVI, pamoja na kuwa msomi wa kiwango hicho lakini pia ana uzoefu wa siasa za TANZANIA kuliko wachangiaji wa mada hii. Amini usiamini serikali tatu siyo suluhu ya matatizo ya MUUNGANO.Kwa hakika kila muungano huwa na matatizo yake,mengine huwa ni ya kupita tu na mengine huwa ni ya kudumu kama ilivyo jamii yenyewe. hakuna jamii isiyo na changamoto zake.wanao dhani serikali tatu ndio muarobaini wa changomoto za muungani wamepata wapi uzoefu huo? hakuna equation ambayo tumekokotoa ikatupa uhakika huo! kwangu mimi kama isingekuwa tamaa uchwara za wanasiasa njia bora ni kuwa na MUUNGANO WA SERIKALI MOJA.NO LESS NO MORE. Wanasiasa wanasema wanaona zanzibar watapoteza IDENTITY YA TAIFA LAO! Kweli? mbona wamepoteza identity za jamii zao na kurithi majina ya kiarabu ilihali wao ni wabantu!
 
Unajua usomi wa kutukuka usiokosolewa ni DHAMBI,ni lazima sisi tunaosema MSOMI ALIYETUKUKA tuwe na uwezo wa kufikiria nje ya BOX je ni kweli kuwa Watanganyika wanataka serikali mbili??na kama ni hivyo je ni sahihi kuendelea na serikali mbili ilhali zimetufikisha hapa tulipo??

Nilikuwa naangalia taarifa ya habari ITV muda sio mrefu mabaraza ya katiba Zanzibar wanasema kwa ukakamavu na msisitizo wanataka Zanzibar itambulike nje ya nchi kama nchi tena kuna mwana mama ameongea kwa uchungu na akimaanisha tafsiri yake ni kuwa Wazanzibari wanataka nchi kamili sio utani uliopo sasa

Ukiwauliza watanzania mmoja mmoja ambaye hana maslahi na faida kutoka CCM awe mpinzani au sio atakuambia tunahitaji serikali ya Tanganyika sasa Shivji ametumwa na nani kuwaambia watanganyika kuwa hawana haki ya kuwa na serikali yao??
 
Yani huu muundo wa muungano umeharibu akili/fikra za watu wa "Tanzania bara" kama inavyoitwa siku hizi. Watu pamoja na viongozi wa Zanzibar wanawaza kama Wazanzibari kwanza, ndiyo maana hata ardhi yao wanaidhibiti kwenda kwa mtu yeyote wa nje hata kama ni wa upande mwingine wa muungano. Wakati huohuo sisi wa Tanzania bara pamoja na viongozi wetu wote tunawaza kama "Watanzania" ndiyo maana tunaona kila tulicho nacho ni cha kwetu pamoja na wenzetu wa Zanzibar. Ni vema serikali ya TANGANYIKA irudi, wanachi na viongozi sote tutaanza kuwaza kama watanganyika, itatusaidia kupiga hatua sana kimaendeleo.
 
Ukiwauliza watanzania mmoja mmoja ambaye hana maslahi na faida kutoka CCM awe mpinzani au sio atakuambia tunahitaji serikali ya Tanganyika sasa Shivji ametumwa na nani kuwaambia watanganyika kuwa hawana haki ya kuwa na serikali yao??
Kwanini wewe una amini yeyote asiecheza na tune ya Tanganyika ni mwana CCM. Pili tatizo la muungano kwa upande wa bara liko wapi hasa? maana hizi tosh Tanesco bills sidhani kama ni sababu halali in the national context za kuvunja muungano au upuuzi aliouzungumza mh. Mbowe, eti wanaingia kwenye bunge letu na tunalipwa sawa wakati wao wana represent watu wachache pumba za ajabu from a national leader.

Kwani representative has to be measured by number, yeye mwenyewe embu hatoke mbele ya kadamnasi aseme in the last two decades of his representative how many of the government bad policies has he ever critised not only national ones, but those that have huge implications on his constituency and the Kilimanjaro region in general. Kwanza akiwa kama kamanda wa fujo he has done more damage to the local income in those parts than CCM poor policies.

Kikubwa hapa kwa wasio utaka huu muungano ni watu wasiopendana kutoka pande za bara na ZnZ, sie ambao tunathamini ubantu kwanza think this course is worth fighting for and there are more benefits in the long run kuliko kuuvunja muungano, kwanza asilimia kubwa ya wapemba in the mainland add to the local economy in one way or another..
 
"Wako watu wengi tu waliotaka muungano wa serikali moja na kwa kweli walitoa sababu nzito sana, lakini sisi tume tumeona mfumo huu haifai kuwepo kwa sasa maana upande mmoja utahisi kumezwa" Jaji Warioba

Haya ndiyo maoni ya watananchi, tume haijali wingi wa watoa hoja "Tume imewasilisha maridhiano ya wajumbe wake baada ya kuwa na mvutano mkali" Prof Shivji
 
Nataka niwaulize tena hao wanaopigia chapuo serikali mbili Shivji inclusive, serikali ya Tanganyika ilienda wapi baada ya mwuungano? Mbona ya Zanzibar ilibaki? Hivi Tanzana Bara ni nchi gani na ilipata uhuru lini? Kama ndiyo Tanganyika ni lini ilibadili jina na kwa sheria au katiba ipi? Mawazo ya Shivji siho lazima yawe sahihi. Halafu hii dhana ya kuwaenzi waasisi wa muungano hata pale panapoonekana dhahiri kuna utata kwenye muungano haina mashiko. It is high time we agreed on the type of union that is fruitfull. Hatuwezi kuendelea na makosa yaleyale. Waasisi wa muungano hawakuwa Mungu na hii kitu siyo panacea. Mtazamo wangu ni kwamba hapa tulipo serikalli 2 haiwezekani tena. Either ziwe 3 au moja. Tuzisome articles za muungano vizuri ili tusahihishe makosa. Karume alishasema koti likikubana unalivua. Hata SeneGambia ilishindikana. Hakuna cha ajabu hapa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom