mbinguni
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 2,759
- 1,061
Usijali mkuu kwani hata wafanye nini, hawana njia nyingine zaidi ya kuondoka.Naomba utafute mwenye mjadala wa udasa jana uliokuwa ukirushwa na ITV ili ujue ni kwa jinsi gani hata wasomi werevu walivyoichoka ccm na serikali yake.
Nilimsikiliza kwenye mdahalo wake wakuaga uongozi wa kigoda cha Mwalimu Nyerere,imesoma ile hotuba yake mara kadhaa na kugundua kuwa sio bure Mwanataaluma huyu alitumwa na akatumika.
Kwa msomi kuwa mnafki haipendezi;Profesa huyu anaujua ukweli wa hali halisi na mazingira ya Muungano wetu kwa sasa anajua ni jinsi gani watanganyika wamedhulumiwa serikali yao kwa miaka mingi,anajua maoni yaliyokusanywa na Tume ya Warioba ni maoni ya wananchi na sio maneno ya Warioba na tume yake ,anajua ni jinsi gani Matatizo ya Muungano yasivyoisha na hayawezi kuisha kweli leo anasema Serikali mbili ndio suluhisho??Baada ya kushindwa kutatua matatizo haya kwa miaka zaidi ya 40 msomi alietukuka anasema serikali mbili ndio mwarobaini??
Inanishangaza sana na leo nimeanza na hili la serikali tatu kwsho nitakuja na jambo lingine la ajabu kabisa ambalo waliomtuma Shivji wamemuambia awadanganye watanzania pia
Acheni kuitumikia CCM imeelemewa na inazama sasa
"Problems canot be solved with the same level of thinking that created them""hii ni principle sio Siasa we need someone else to solve our problems and in this case and time we have CHADEMA ndio mwarobaini sio Shivji na siasa za uvungungi dont fight from dark tangaza wewe ni mwanachama wa CCM na unafanya kazi zao kwa wasomi.