Mkuu hapo kwenye red ndipo ninapotegemea msomi wa ukweli apasimamie. Huo ndio utakuwa muungano wa kweli nje na hapo utabaki kuwa ni muungano wa "kichina". Msomi wa kweli hawezi tu kuishia kusema huu huwezekani kwa sababu ya ubinafsi wa watawala. ashauri roadmap ya kuua au kuudhibiti huo ubinafsi ili tuweze kuwa na muungano halisi. Hatuhitaji kubembelezana kuunda muungano. Mimi nadhani serikali tatu itatusaidia kujitambua na inaweza kutufundisha practically kwa nini tuwe na serikali moja tu ya muungano. Zanzbar wakipata machungu ya kuwa na serikali yao katika tuvisiwa twao watapata akili na kujua kwa nini wakenya wanatutamani sana tuungane nao, nao watakuwa wa kwanza kututafuta na kutubembeleza watanganyika turudiane.Wakati mwingine unaweza ukaanza kurusha mateke hewani ukifikiri utampata unayetaka kumtandika kumbe mtu mwenyewe hata hayupo. You're missing a point.
Kasome kwanza alichokisema Prof. Shivji ili ukielewe na pia naomba utambue kuwa kila Mtanganyika na Mzanzibari ana maoni kama yalivyo maoni yako.
Kama yeye anatumika na CCM, na wewe utakuwa unatumika na nani kwa sababu hawezi yeye kutumika na wewe usitumike.
Huoni kama mawazo yako ndiyo yanaonekana zaidi kama unatumika.
Kwangu mimi ninatakata wananchi wapewe fursa ya kupiga kura ya maoni kuchagua kama wanataka muungano au waachane nao.
Serikali mbili zimeshindwa kuondoa matatizo kwa sababu hazikuingia kwenye muungano zikiwa na nguzo imara za kisiasa ambazo ni kukubalika kwa wingi na wananachi. Muungano ulikuwa ni makubaliano ya viongozi wakuu wawili.
Serikali tatu ni barabara ya kuua muungano lakini kwa gharama kubwa.
Serikali moja ni dawa ya muungano lakini hakuwezekani kwa siasa na wanasiasa wa Tanzania kwa sababu ya ubinafsi wao.