Nani alimtuma Issa Shivji The Professor?

Usijali mkuu kwani hata wafanye nini, hawana njia nyingine zaidi ya kuondoka.Naomba utafute mwenye mjadala wa udasa jana uliokuwa ukirushwa na ITV ili ujue ni kwa jinsi gani hata wasomi werevu walivyoichoka ccm na serikali yake.
 
Achana na kumlaumu Mwalimu , kama mnauwezo wa kuuvunja muungano vunjeni.
Hata kwa sisi Watanganyika tulio wengi Zanzibar ya sasa ni KERO ya muungano.

acha ujuha dogo. muungano uwe mzuri au mbaya ukweli ni kwamba alietekeleza matakwa ya kennedy wa marekani ili tuungane, ni mwl nyerere. mi nazungumzia chanzo cha muungano basi
 
acha ujuha dogo. muungano uwe mzuri au mbaya ukweli ni kwamba alietekeleza matakwa ya kennedy wa marekani ili tuungane, ni mwl nyerere. mi nazungumzia chanzo cha muungano basi
Ukweli na kero za mwaka 1964, najua wewe huwezi kuujua.
Ukweli na kero za leo 2013 ni kwamba Zanzibar ni KERO ya muungano.
 
Pole sana shivji, komaa ivoivo ili tonge yako isipotee but uamini kwamba kwenye maisha mabadiliko ni lazima so Tz kupata mabadiliko ni kitu hakipingiki kupitia rasimu hii
 


Huo usomi wako hapa sijauona...
zaidi ya matusi na kejeli kwa mleta uzi....
hakuna kitu cha hatari dunia kama kujikweza...sote tunatumia majina bandia humu..hatufahamiani ....kama sote tungesema vyuo tulivyosoma na malezi tuliyopitia...labda ungekuwa na mtazamo tofauti.....
tatizo unasahau kuwa Mwalimu Shivji ni binadamu kama wengine....
ajabu eti unaapa kabisa....
kazi kwelikweli...
 
Kwa watu tunaomfahamu Shivji, kusema katumwa ni sawa na kumtukana!. Issue sio usomi bali uelewa!. unaweza kuwa msomi wa Ph.D and yet ukawa na uelewa duni!, na kuna mtu hajasoma hata darasa moja na akawa na uelewa wa kiwango cha kutosha kumwelewa Shivji!. Hapa sizungumzii vidato wala intellects, nazungumzia I.Q!.
 


Wewe mwehu kweli, ubantu gani uliopotezwa?? shida yako ubantu au uarabu?? Watanganyika wetu hili la zanzibar na uwarabu linawauma rohoni mwao sana, kuwa mweledi changia mada wacha upotoshaji.
 
Hii ni nchi yetu na hatma yake ii mikononi mwetu,kama wengi tunasema hatutaki muungano,au tunataka serikali tatu Shivji ni nani hata asimamishe au ashauri au apotoshe lengo letuuu??

Maoni yaliyokusanywa nchi nzima ndiyo yaliyotoa Rasimu sasa anaepingana na maoni yetu yeye ni nani??

Na kama hajatumwa mbona liko kundi linalomifu na kusimamia msimamo wake nani asiyejua wanaopenda serikali mbili ni wale waliotufikisha hapa walioshindwa kutatua kero za muungano kwa miaka hamsini.

Ni DHAMBI kusema uongo na pia ni UHAINI kupotosha umma ,haihitaji elimu kubwa kuona hali halisi na kusoma nyakati zilizopo kila mtu anajua matatizo ya Muungano na Kero zake

Naamini leo tukipiga kura kati ya wanaotaka na wasiotaka muungano SHIVJI angeshangaa zaidi kwani watanzania zaidi ya asilimia 80 hawataki wala kuusikia Muungano.

Changieni kwa busara usijiache uchi hapa kuonyesha ushafu na uozo wa akili zako kwa kutoa maneno ya kifedhuli na ushabiki wa majitaka
 
Mkuu George, George J Minja,
pole sana!. Nimebahatika kuwa mwanafunzi wa Prof. Shivji pale UDSM, alitufundisha somo la constitutional law ambalo nililifumua A na toka wakati huo mpaka kesho, amekuwa role modal wangu!. Kwa waliopita UD enzi hizo, wanaelewa ukipata A+ ya Shivji kulimaanisha nini!. Kulimaanisha ili uweze kumwelewa Shivji vizuri, kunahitaji uwe na level fulani ya uelewa!, vinginevyo utaishia to miss the point na ndicho kilichokukuta Mkuu George!. Pole sana!.

Ushauri wa bure kwako, unapokutana na mawazo ya hawa ma intellectuals waliotukuka, jaribu kuwasoma kwa kituo huku ukitafakari the motive behind hayo mawazo yao, ukijiridhisha umewaelewa vizuri ndipo unaibuka na critique iliyokwenda shule yenye kuweza kupangua hoja kwa hoja na sio kukurupuka kama ulivyokurupuka as if hujaenda shule!.

Kati ya watu ambalo kamwe hawawezi kutumiwa, miongoni mwao ni Prof. Shivji. Mabingwa wa Sherman ya Katiba pale Mlimani wanajulikana!, laiti ungelijua ni kwa nini kwenye Tume ya Warioba, wamewachukua Prof. Palamagamba Kabudi na Dr. Sengodo Mvungi na kumwacha Prof. Shivji, usingelithubutu kuuleta huu utumbo wa eti anatumiwa!.

All and all, kuwa na uelewa duni au hafifu sio kosa!, hata kina Socrates na Plato mwanzoni hawakueleweka na watu wa kawaida, but with time and patience hatimaye watu waliwaelewa!, vivyo hivyo ninaimani, na wewe kwa kuendelea kuwasoma ma gt hata wa humu jf, uelewa wako utaongezeka, utamwelewa Prof. Shivji na wewe kujikuta unashuka na nondo na sio huu utumbo uliotumwagia humu!.
Pole!.
Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…