Nani alimwelewa Yesu kwenye hili fumbo?

Nani alimwelewa Yesu kwenye hili fumbo?

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Mathayo 9:16
[16]Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
 
Ukisoma Math:9,16,17,Hyo Kiraka Cha nguo,viriba vikuukuu ni mifano ihusuyo udhaifu katika mambo ya dini ya kiyahudi mintarafu azimio la wokovu.

Na Nguo mpya na divai mpya ni mifano wa Hali mpya ya ufalme wa Mungu. Hali mpya ya ufalme wa Mungu haiwezi kutegemea mambo hafifu ya mpango wa Kale Kwa kuwa ujio wa Yesu amefanya yote upya katika ukamilifu (Math 5:17).

Ikiwa nimekosea turekebishane ili tupate kujifunza sote🙏🏿
 
Ukimapata Yesu unafanywa kuwa mpya as whole.yaani. lazima ubadilishwe kwa sababu Yesu ni mambo yote kati ya yote.

Divai mpya haiwezi kukaa kwenye kiriba cha zamani.Ukimpata Yesu na Roho mtakatifu kweli, Utake usitake lazima ugeuzwe tuuu.Yaani automatically unakuwa wa tofauti

Chukulia Mwanamke, akipata mimba mara nyingi hali yake inabadilika.Yaani kuna vitu alikuwa napendelea kula,utashangaa sasa vitu hivyo hivyo hataki hata kisikia harufu yake.Ndiyo hivyo hivyo ukimpata Yesu kuna vitu utaviacha kabisa tena utavichukia.utakuwa mwingine kabisa.

Nadhani unamkumba Sauli,baadaye Paulo.

Ukimkuta mlevi anakwambia ameokoka halafu bado analewa ujue hapo kuna uwalakini
 
umejaribu lakini bado hujakamata vizuri alilenga kufundisha nn
 
bado sijapata mtu wa kuelezea vizuri mithali hiyo.
 
Mathayo 9:16
[16]Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
Torati ni kiraka neema ni vazi mpya ukichanganya torati na neema hutoboi torati ni kivuli na neema ni halisi amua leo kuwa baridi au moto usiwe vuguvugu
 
hapana hakufundisha hicho.

Kumbuka kabla ya kutoa huo msemo, hapo juu walimuuliza kwanini wanafunzi wako hawafungi ?
 
Nitakufafanulia Mkuu natumaini utanielewa sana KUPITIA Roho mtakatifu.

Karibu sana
 
Mathayo 9:16 inasema, "Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi la zamani; kwa kuwa kiraka hukiondoa kwa vazi na ufa huwa mkubwa zaidi."

Aya hii ni sehemu ya mafundisho ya Yesu katika Injili ya Mathayo. Inaelezea kanuni ya kiroho kwa kutumia mfano wa kiraka cha nguo mpya na vazi la zamani.

Kwa kuzingatia muktadha wa aya hiyo, Yesu alikuwa akizungumza juu ya tofauti kati ya mafundisho yake mapya na mafundisho ya kidini ya Kiyahudi yaliyokuwepo wakati huo. Alikuwa akileta mafundisho mapya ambayo yalikuwa na msukumo mpya na kuleta mabadiliko katika maisha ya watu.

Mfano wa kiraka cha nguo mpya na vazi la zamani unamaanisha kuwa mafundisho ya Yesu hayawezi kufungwa kwa mafundisho ya kidini ya zamani. Kama vile kiraka cha nguo mpya kinavyoondoa sehemu ya vazi la zamani na kusababisha ufa mkubwa, mafundisho mapya ya Yesu yanahitaji mabadiliko kamili na kuacha mafundisho ya zamani ya kidini.

Hivyo, Mathayo 9:16 inaonyesha kuwa mafundisho ya Yesu ni mapya na yanahitaji njia mpya ya kufikiria na kuishi. Inahimiza watu kubadilika na kuelekea mafundisho mapya ambayo Yesu alikuwa akiwaletea.
 
Mathayo 9:16
[16]Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
alinena kwa habari ya agano la kale na agano jipya.. aliongeaa kwa old covenant na new covenant ( agano la damu yake )
 
Mathayo 9:16
[16]Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
maana ake huwez kutoa ktu chenye thamani kubwa kwenda kukamilisha sehem ndogo ya ktu kscho na thaman hata kdg, sbb mkamilisho huo utakifanya kitu kisicho thaman kupotea kabisa au mazma ndo mana anasema kpande cha nguo mpya ukikifanya kilaka kwnye nguo kuukuu nguo hyo itatatuka zaidi, yan kilaka kitaikimbiza nguo
 
Una nguo mpya na ya zamani. Ya zamani ikapata tundu. Je utaliziba kwa kukata kipande cha nguo mpya si utakuwa unaiharibu, tundu lile litazidi kuwa kubwa kadiri unavyoitumia.
Unapoongelea nguo inaleta mantiki, ila ufananisho wa uwepo wake kati ya wafuasi wake, ni ngumu kuleta mantiki.
 
bado

Ufunuo wa Yohana 16:16
[16]Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.
 
Back
Top Bottom