Nani alimwelewa Yesu kwenye hili fumbo?

Nani alimwelewa Yesu kwenye hili fumbo?

Koran 5;51. Enyi mlio amini! (Waislamu) Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki.

USHETTTANI KAMA HUU UNAUZUNGUMZIAJE...???
quran ilivyofutwafutwa hapo utakutana na Toleo lengine halijaandika hivo
FaizaFoxy
 
Mathayo 9:16 inasema, "Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi la zamani; kwa kuwa kiraka hukiondoa kwa vazi na ufa huwa mkubwa zaidi."

Aya hii ni sehemu ya mafundisho ya Yesu katika Injili ya Mathayo. Inaelezea kanuni ya kiroho kwa kutumia mfano wa kiraka cha nguo mpya na vazi la zamani.

Kwa kuzingatia muktadha wa aya hiyo, Yesu alikuwa akizungumza juu ya tofauti kati ya mafundisho yake mapya na mafundisho ya kidini ya Kiyahudi yaliyokuwepo wakati huo. Alikuwa akileta mafundisho mapya ambayo yalikuwa na msukumo mpya na kuleta mabadiliko katika maisha ya watu.

Mfano wa kiraka cha nguo mpya na vazi la zamani unamaanisha kuwa mafundisho ya Yesu hayawezi kufungwa kwa mafundisho ya kidini ya zamani. Kama vile kiraka cha nguo mpya kinavyoondoa sehemu ya vazi la zamani na kusababisha ufa mkubwa, mafundisho mapya ya Yesu yanahitaji mabadiliko kamili na kuacha mafundisho ya zamani ya kidini.

Hivyo, Mathayo 9:16 inaonyesha kuwa mafundisho ya Yesu ni mapya na yanahitaji njia mpya ya kufikiria na kuishi. Inahimiza watu kubadilika na kuelekea mafundisho mapya ambayo Yesu alikuwa akiwaletea.
hiyo mithali inatakiwa iwe na mahusiano na swali ambalo walimuuliza Yesu.

Aliulizwa mbona wanafunzi wako hawafungi ?

Yesu ni Vazi jipya.
Wafunzi ni vazi kuukuu

kama ulikua na matendo maovu inamaana vazi lako linakua limechakaa.

Yesu haji kuziba mapungufu ya wanafunzi wake kwa kutumia tabia yake ya kivazi jipya.

Divai mpya .... kiriba kikuukuu kitapasuka.
mtu kaokoka jana, leo unamwambia afunge kula siku nne kavu.
aloo utampoteza.

Kuna neno ukimwambia mtu aliyekomaa kwenye wokovu atakuelewa, lakini ukimwambia mtu aliyeokoka jana hawezi kustahimili.
 
Mathayo 9:16
[16]Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
: mafundisho yake na ya sheria zao
Kwa kifupi hapa anaongelea mafundisho yake na yale ambayo yalikwisha kutangulia. Ambapo alikuwa anasisitiza juu ya kukubali kuanza upya na kufuata haya anayowaelekeza maadam yale ya mwanzo kama alivyo sema hakujakutangua isipokuwa kutimiliza. ( kuna mahala aliwahi kuwaambia mambo haya yametimia masikioni mwenu..Lk 4:20)

: kwa nini mfano wa nguo mpya na kiraka?
Zamani walikuwa wanatengeneza nguo na material kama vile ngozi nk. zile za kwanza zinakuwa tayari zimekwisha kukauka.. unapokuja kuweka hii mpya, inakulazimu kutoboa ile ya zamani na kuweka kiraka.
Kitendo cha kutoboa kwa zamani ilileta shida kidogo, kwa sabab hii nyingine ikishawekwa itaanza kusinyaa(kucontract), kumbe inaleta changamoto. N.k

Kumbe basi Yesu, anawaeleza, kuvua utu wa kale na kuvaa upya uti mpya. Kwa kutolea mfano huo Waone wenyewe jinsi ilivyo ngumu kusikiliza na kufuata mfano wa mafundisho ya Yesu na zile sheria walizokuwa nao.

: katika maisha yetu pia inakuwa na maana kubwa zaidi.kwa mfano, hauwezi kuweka maji masafi kwenye chombo kichafu. Maana yatachafuka, Kumbe, nasi pia, ili tuweze kuenenda na mafundisho ya Kristo lazima tukubali kujikana wenyewe, ni wazi kabisa tutapata mapingamizi mengi, kutoka kwa jamii ya watu wa kizazi chetu cha leo. Lakini lazima tushone nguo mpya na sio kuweka kiraka katika nguo ya zamani.
 
Ukitafakari mintarafu Hekima ya Mungu basi utaona kwamba Kiraka kipya kwenye Nguo Kuukuu ni Ile hali ya kuleta mafunzo mapya,hekima mpya,maarifa mapya na kuyalazimisha yalandane na Mafunzo au hekima ya Zamani.Kwa mfano Somo hili lilizungumzia swali aliloulizwa Yesu Kuhusu Wanafunzi wake mbona hawafungi?Naya akawajibu hivyo akimaanisha kwamba Kwa wakati ule alikuwa analeta habari njema mpya kabisa ambayo msingi wake haukuwa desturi na mafunzo ya zamani kwani hayo yalikuwa hayaendani na Mafunzo yake Mapya.Na angewachanganyia Mafunzo na desturi za Zamni basi kwa hakika wangevurgika.
 
Back
Top Bottom