Mathayo 9:16
[16]Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
: mafundisho yake na ya sheria zao
Kwa kifupi hapa anaongelea mafundisho yake na yale ambayo yalikwisha kutangulia. Ambapo alikuwa anasisitiza juu ya kukubali kuanza upya na kufuata haya anayowaelekeza maadam yale ya mwanzo kama alivyo sema hakujakutangua isipokuwa kutimiliza. ( kuna mahala aliwahi kuwaambia mambo haya yametimia masikioni mwenu..Lk 4:20)
: kwa nini mfano wa nguo mpya na kiraka?
Zamani walikuwa wanatengeneza nguo na material kama vile ngozi nk. zile za kwanza zinakuwa tayari zimekwisha kukauka.. unapokuja kuweka hii mpya, inakulazimu kutoboa ile ya zamani na kuweka kiraka.
Kitendo cha kutoboa kwa zamani ilileta shida kidogo, kwa sabab hii nyingine ikishawekwa itaanza kusinyaa(kucontract), kumbe inaleta changamoto. N.k
Kumbe basi Yesu, anawaeleza, kuvua utu wa kale na kuvaa upya uti mpya. Kwa kutolea mfano huo Waone wenyewe jinsi ilivyo ngumu kusikiliza na kufuata mfano wa mafundisho ya Yesu na zile sheria walizokuwa nao.
: katika maisha yetu pia inakuwa na maana kubwa zaidi.kwa mfano, hauwezi kuweka maji masafi kwenye chombo kichafu. Maana yatachafuka, Kumbe, nasi pia, ili tuweze kuenenda na mafundisho ya Kristo lazima tukubali kujikana wenyewe, ni wazi kabisa tutapata mapingamizi mengi, kutoka kwa jamii ya watu wa kizazi chetu cha leo. Lakini lazima tushone nguo mpya na sio kuweka kiraka katika nguo ya zamani.