Nani aliwalipia Wasanii gharama za ziara ya Korea?

Hivi ndivyo kodi zetu na mikopo tunayokopa kila kona kila uchao inavyotumika kama tumepagawa vile.

Hatukatai serikali kuwapeleka wasanii kutoa tongo tongo na kuwapiga brush huko Korea lakini je nani anaweza kutuambia why walipiwe Business Class ambayo hata wafadhili wetu hawatumii.

Tena kipindi hiki ni peak season ya utalii hivyo tiketi za ndege ni aghali zaidi duniani kote hivyo kutumia tiket za dola 5,800 hadi dola 8,000 badala ya tiketi za dola 1,700 I ubadhirifu wa kiwango cha mauaji ya wajawazito kukosa pesa za kujifungulia na kulipia mtu mmoja tiketi ya 20m na kuacha tiketi ya 4.7m ni Insane.

Nadhani hela za mikopo na za uza uza zimetulevya tumeamua kuzitapanya huku tukibana wazee kwenye tozo na matibabu.

NI LAANA...Kuua si lazima kupiga watu shoka! Kuna mauaji ya indirect!!
 
Unasema wasanii hata viongozi wa serikali wanaenda nje kama kutalii ,kama ni project wanayoifuata unakuta washaandaa ripot ndio wanaenda .

wakimaliza kikao kuna kuzunguka na kupiga picha ili mradi wakae mda mrefu kidogo .
 
Wabongo sisi ni kulalamika tu always nafikiri mmoja kati yetu angekuwa ni sehemu ya hiyo ziara bila shaka angekula buyu
Siku zote ukiwa sehemu ya wanufaika huwezi kulalamika, walalamikaji wengi ni sisi ambao kweli keki ya taifa inatupitiq pembeni, lakini pia ni aibu sana kwa sababu sisi kama taifa tuna changamoto nyingi sana, matatizo mengi sana. Tukiona hivi hata nguvu ya kulipa kodi inakuwa ndogo.
 
Binafsi sijaona shida iko wapi hapo maana hta walioenda ni sehemu ya walipa kodi pia na lengo ni zuri ila linapoteza maana sababu ya wakati na aina ya watu waliochaguliwa kwenda kwngu naona ndio tatzo kwani limekaa kisiasa zaidi
 
Hahaha kwani hujui aliyewalipia nauli.

Tunahitaji vijana kama wale wa Kenya wanaoweza kuiambia serikali nini cha kufanya sasa baada ya kuchochwa na mambo ya hovyo yasiyo na tija.
Kwanin kila msala mnataka vijana wakae frontline? Katiba tuliyonayo ni ya mwaka 77 vijana hawajazaliwa, sera mbovu na mifumo yote viliwekwa madogo bado hawajazaliwa wengine walikua watoto nyie mliokua watu wazima kipindi hicho kwanini hamkukinukisha? Mliogopa? Hamkujua kama mnaingizwa chaka? Kwanini mnataka vijana wajitoe muhanga frontline kwa uzembe/uoga wenu wa kushindwa kuzuia tatizo from the first place? Vijana, wakina baba, wakina mama na wazee wote twende frontline kuikomboa nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…