Dumas the terrible
JF-Expert Member
- Jan 20, 2021
- 4,779
- 9,999
Tukiacha Uchawa na kujipendekeza kama Kahaba aliyeona mkoba wa Dhahabu za Babylon kwenye chumba cha siri kwa kuhani wa mungu Murduk ndani ya hekalu la Enki.
Ile hotuba Madame kaharibu kabisaaaa badala ya kujenga anabomoa mpaka vumbi litimke,
Haiwezekani aisee jana naangalia nusu kidogo nirushe tonge la ugali kwenye Screen maana niliona kama mauza uza hivi.
Nikajiuliza kama watu ambao tunadhani Wana akili timamu na tumewapa dhamana kwa kuwaamini Wana akili zote ndio wanaandaa utumbo kama ule vipi mwenyekiti wangu wa mtaa huko Namtumbo ngumbaru aliyepita bila kupingwa si ndio atatoa maagizo ya mtu kutolewa bandama?
Ifike mahali kama nchi tujitafakari hawa tunaowapa dhamana Wana akili timamu kweli au ni vichaa waliochangamka!
anyway yawezekana Madame President alipitiwa maana kama binadamu tunakosea ila kama alikusudia akiwa na maana ya kupanic kutokana na yanayoendelea hapo inaonekana wazi Wapinzani wake wa kisiasa wamemuingiza kwenye 18 zao na kajaa bila kujua kawapa point 3 za bure na ligi ndio imepamba moto,
naombeni sana kama mnanisikia mtu mzima hua hakosei ndio siasa za Afrika zilivyo ila angalau mrekebishe mambo madogo madogo ambayo yanasababisha matatizo makubwa yatokee,
Haiwezekani useme kabisa 'zile Sheria za kipindi kile bado zipo na zinafanya kazi'
wakati hao hao ukiingia nao field kwa mahakama wanakugaragaza mchana kweupe mpaka mnapanic na kuwapiga Risasi mchana wa jua kali!
Najua mkitumia nguvu ndio mtawaweza ila kama Sheria hizi hizi za mkoloni thubutu watawaaibisha mchana kweupe,
Note: When a Wise man Rise, Wisdom taking place
Angalieni panapovuja msije sema hatukusema...