Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Mna wivu sana!!
 
Mkuu kama hutojali hebu funguka kidogo kuhusu hiyo chui republic. Niliwahi kusikia habari yake wakati flan nikiwa mdogo ila memory ilifuta kwa sasa sikumbuki lolote
 
Thread inasema mkoa wa Mara watu wanaijadili musoma ili kutoa nyongo zao. Mkoa wa Mara uko vizuri kiuchumi ukilinganisha na mikoa mingine mingi tanzania kwa mujibu wa NBS sasa sijui tatizo lenu ni nini. Musoma kama wilaya changamoto zake kubwa ni location yake,hali ya hewa pamoja na kutokuwa na uwekezaji wa maana kwa muda mrefu. Mzunguko wa pesa ndani ya musoma ni mdogo sana ila sio kwamba watu hawawajibiki jamani!
 
Duh msonge dah ila kwa siro pale kaibakari pamebadilika
 
Tuambie wewe wakurya gani wana majungu maana siye tunajua mkurya ni mkurya tu.
 
Kabisa mkuu, yaani hadi inatia hasira kweli, watu hadi wanaogopa kwenda kwao, wa wakienda kwao kusalimia wanaingia usiku, na siku ya kuondoka ni hivyo hivyo! Shem on us Mara people.
Uliposema "Shem on us" nimekuelewa zaidi.
 
Kuhusu Wakurya Mimi binafsi hunidanganyi. Hawa watu ni wafitini na watu wa kujipendekeza na kuchongea wenzao makazini. Waulize Polisi sasa hivi wanavyolia kwa kuongozwa na Mkurya. Ni wanafiki kuliko kawaida.
 
Sina uhakika sana na hayo mnayoyasema ila ninachokijua na kukiamini ni transparence ndiyo inawasumbua hao jamaa halafu ni waoga ku missappropriate govt funds otherwise mwalimu angekuwa kama hawa wengine tunaowaona mkoa wa mara na hususani butiama kungekuwa kama yerusalemu mpya kabisa. 23 yrs in power halafu hata lami wala international hakuna? Subutu
 
Kuna kitu nimejifunza sana humu, watu tuna generalise mambo sana. Kuna mtu alileta mada humu ati Kigoma wako nyuma kumaendeleo sababu ya uchawi.

Kitu nimejifunza, watu wengi hawaijui Tanzania, Watanzania wote wako sawa- imani za kishirikina zimetamalaki nchi nzima ISIPOKUWA sehemu chache sana nako ni maeneo ya Uchagani labda kwa sababu ya elimu au Wamisionari kuweka kituo pale. Wachaga ushirikina wao ni matambiko wakati Watanzania wengi ulozi pia upo.

Mikoa yote iliyobakia ulozi unaaminiwa kwa jamii hizo na hiyo ni SABABU MOJAWAPO lkn kwa nyakati hizi SIO SABABU KUU. Sababu kuu ya kutamalaki umasikini ni serikali kuchelewa kupeleka huduma muhimu ktk hiyo mikoa, yaani elimu na miundombinu ya barabara, anagalia mikoa yote iliyochelewa kuunganishwa na barabara za lami iwe Rukwa, Mtwara, Lindi, Kigoma, Mara na Kagera , hiyo maendeleo yao yako nyuma. Ingawa lawama wanashushiwa wenyeji wa maeneo hayo ati wachawi nk huo ni uzushi tu, jamii gani za kiafrika hasa Wabantu hawaamini juu ya hayo mambo? Wengine wanasema wenyeji wa mikoa hiyo walio nje wakifanikiwa hawawekezi mikoani kwao, utawekeza sehemu ambayo haina faida na gharama zake ni kubwa? Hivi bei ya bati kule Musoma ni sawa na ya Dar? Watawekeza Mwanza kwa kwa kodi za nyumba ziko juu na zinalipa ingawa vifaa vya ujenzi vina gharama kubwa. Mnaobisha waulizeni wenzenu, bei ya kodi za vyumba Sumbawanga, Musoma, Kigoma, Lindi, Mtwara na Bukoba ni sawa na kodi ya vyumba kwa miji ya Arusha, Mwanza, Moro na miji mingine inayodaiwa imeendelea zaidi?

Kuna mambo ya msingi lazima serikali ifanye ili maendeleo sehemu husika yashike kasi. Chato muda si mrefu msishangae ikakua na kusitawi kwa kasi maana hayo mazingira yameandaliwa -barabara nzuri ya kuunganishwa na miji mingine pamoja na uwanja wa ndege.

Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…