Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Mbona umekazania kuhusu wivu? Unaweza kuthibitisha kwa hoja za kisomi?watu wachache wasikupe uhalali wa kuwanjia heshima wengine. Taja mkoa wako unaotokea ndipo tufanye ulinganishi.
Kwa haraka haraka nimehisi una chuki na mmoja wa watu wa Mara so unatafuta namna ya kujifariji.
Mara ni moja ya mikoa yenye makabila mengi, je inawezekanaje wote wakawa na wivu sawa kiasi unachodai?
Mna wivu sana!!
 
Kuchukiana imetokana na divide and rule policy ya Nyerere baada ya jaribio la kuanzisha Jamhuri ya Chui. Aliwagawa wakurya baada kuona ni watu hatari sana kwa utawala wake. Mojawapo ni kuwachonganisha kwa kuvuruga mipaka ya vijiji. Fanya research utajionea
Mkuu kama hutojali hebu funguka kidogo kuhusu hiyo chui republic. Niliwahi kusikia habari yake wakati flan nikiwa mdogo ila memory ilifuta kwa sasa sikumbuki lolote
 
Thread inasema mkoa wa Mara watu wanaijadili musoma ili kutoa nyongo zao. Mkoa wa Mara uko vizuri kiuchumi ukilinganisha na mikoa mingine mingi tanzania kwa mujibu wa NBS sasa sijui tatizo lenu ni nini. Musoma kama wilaya changamoto zake kubwa ni location yake,hali ya hewa pamoja na kutokuwa na uwekezaji wa maana kwa muda mrefu. Mzunguko wa pesa ndani ya musoma ni mdogo sana ila sio kwamba watu hawawajibiki jamani!
 
Nawashukuru kwa michango yenu ,ila kuna mambo nataka niyaweke sawa.Welema anatokea Kijiji kinaitwa kongoto wilaya ya Butiama,Mhongo anatokea Majita ,Mkono anatotokea Butiama na Eriakimu Maswi kwao ni tarime,Uliyeongelewa wakurya utakuwa hujafanya utafiti vzr,Hakuna kabila lenye husuda kwa mkoa wa Mara kama Wajita yego jaji, Suala la watu kujenga kwao inatengemeana ila siyo mambo ya kurongwa .Nenda kwao Jaji Warioba huwezi amini kuwa ndipo anatokea,Lkn kwao mke wake moshi mambo yako vzr,Hivyo hivyo kwao welema alijenga msonge tena baada ya wazee kukomalia kuwa huwezi kufikia kwenye nyumba mama yake mzazi,Kwahiyo suala la kujenga hata wanawake tunaoa wanaweza kuchangia mwanaume kushindwa kuwekeza nyumbani.
Duh msonge dah ila kwa siro pale kaibakari pamebadilika
 
Wewe sasa una matatizo yako
Hauwafahamu wakurya
Hizo ni fikra zako tu ndogo ndizo zinazokutuma kufikiri hivyo

Unaposema wakurya ni kama useme wachaga
Humo ndani yake kuna Wamarangu, wakibosho, wamachame n.k
na wakurya nao wapo hivyo hivyo
Humo ndani kuna wanchari, warenchoka, wakira, wanyamongo n.k

Sasa usipende sana ku generalize
Coz tabia za wamachame sio tabia za wachaga wote
Hivyo jifunze
Tuambie wewe wakurya gani wana majungu maana siye tunajua mkurya ni mkurya tu.
 
Kabisa mkuu, yaani hadi inatia hasira kweli, watu hadi wanaogopa kwenda kwao, wa wakienda kwao kusalimia wanaingia usiku, na siku ya kuondoka ni hivyo hivyo! Shem on us Mara people.
Uliposema "Shem on us" nimekuelewa zaidi.
 
Hapo Mnaongelea Musoma na vitongoji vyake, Tarime pako poa sana, ni mji ambao mgeni hata akifika hatamani kuondoka, fursa zipo kibao, na Yule aliyesema Wakurya wana husuda na fitina hawajui vizuri, labda anahisi Mkoa wote wa Mara wenyeji ni Wakurya, Musoma nature ya eneo ndio inapafanya pawe nyuma, ni peninsula, barabara ya kutoka na kuingia ni hiyo hiyo moja, hakuna shughuli yoyote ya maendeleo mbali na uvuvi ambao ni wa kusuasua ukilinganisha na maeneo mengine kama Bunda na Mwanza, hali ya hawa na ardhi sio nzuri kwa kilimo, wenyeji wake sio wafugaji, pale kupata maendeleo ni ngumu sana, ni bora hata Makao Makuu ya Mkoa wangepeleka Tarime
Kuhusu Wakurya Mimi binafsi hunidanganyi. Hawa watu ni wafitini na watu wa kujipendekeza na kuchongea wenzao makazini. Waulize Polisi sasa hivi wanavyolia kwa kuongozwa na Mkurya. Ni wanafiki kuliko kawaida.
 
Sina uhakika sana na hayo mnayoyasema ila ninachokijua na kukiamini ni transparence ndiyo inawasumbua hao jamaa halafu ni waoga ku missappropriate govt funds otherwise mwalimu angekuwa kama hawa wengine tunaowaona mkoa wa mara na hususani butiama kungekuwa kama yerusalemu mpya kabisa. 23 yrs in power halafu hata lami wala international hakuna? Subutu
 
Kuna kitu nimejifunza sana humu, watu tuna generalise mambo sana. Kuna mtu alileta mada humu ati Kigoma wako nyuma kumaendeleo sababu ya uchawi.

Kitu nimejifunza, watu wengi hawaijui Tanzania, Watanzania wote wako sawa- imani za kishirikina zimetamalaki nchi nzima ISIPOKUWA sehemu chache sana nako ni maeneo ya Uchagani labda kwa sababu ya elimu au Wamisionari kuweka kituo pale. Wachaga ushirikina wao ni matambiko wakati Watanzania wengi ulozi pia upo.

Mikoa yote iliyobakia ulozi unaaminiwa kwa jamii hizo na hiyo ni SABABU MOJAWAPO lkn kwa nyakati hizi SIO SABABU KUU. Sababu kuu ya kutamalaki umasikini ni serikali kuchelewa kupeleka huduma muhimu ktk hiyo mikoa, yaani elimu na miundombinu ya barabara, anagalia mikoa yote iliyochelewa kuunganishwa na barabara za lami iwe Rukwa, Mtwara, Lindi, Kigoma, Mara na Kagera , hiyo maendeleo yao yako nyuma. Ingawa lawama wanashushiwa wenyeji wa maeneo hayo ati wachawi nk huo ni uzushi tu, jamii gani za kiafrika hasa Wabantu hawaamini juu ya hayo mambo? Wengine wanasema wenyeji wa mikoa hiyo walio nje wakifanikiwa hawawekezi mikoani kwao, utawekeza sehemu ambayo haina faida na gharama zake ni kubwa? Hivi bei ya bati kule Musoma ni sawa na ya Dar? Watawekeza Mwanza kwa kwa kodi za nyumba ziko juu na zinalipa ingawa vifaa vya ujenzi vina gharama kubwa. Mnaobisha waulizeni wenzenu, bei ya kodi za vyumba Sumbawanga, Musoma, Kigoma, Lindi, Mtwara na Bukoba ni sawa na kodi ya vyumba kwa miji ya Arusha, Mwanza, Moro na miji mingine inayodaiwa imeendelea zaidi?

Kuna mambo ya msingi lazima serikali ifanye ili maendeleo sehemu husika yashike kasi. Chato muda si mrefu msishangae ikakua na kusitawi kwa kasi maana hayo mazingira yameandaliwa -barabara nzuri ya kuunganishwa na miji mingine pamoja na uwanja wa ndege.

Vv
 
Back
Top Bottom